Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nilianza kuisikia zaidi Mloganzila mwakajana, wakati ndugu yangu akiwa amelazwa hapo. Naye hakuishi tena.
Kwa sasa kuna ndugu yangu anatibiwa hapo. Amefanyiwa upasuaji mara 3, hakuna mabadiliko makubwa. Siamini kuwa inatokana na ukubwa wa tatizo, uwezekano mkubwa ni huduma ya kiwango cha chini.
Majengo tulijengewa na Wakorea Kusini, ni mazuri, yanapendeza. Vifaa tiba navyo ni msaada, na vimejaa sana.
Baada ya kufuatilia kwa wataalam wa pale Muhimbili, taarifa nilizopewa na maprof. watatu tofaiti, ni kuwa hatuna wataalam wenye uwezo wa kuvitumia vifaa tiba vya kisasa vilivyopo pale.
Hata huyu prof. aliyeitoa hii taarifa, kama utakutana naye kama mtu binafsi, hatakosa kukuambia ukweli wa tatizo la Hospitali ya Mloganzila.
Bahati mbaya serikali yetu inaamini tuna uwezo wa kila kitu. Hatuna mipango ya kuwapeleka watu kwenda kujifunza nje ya nchi.
Jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Kikwete mpaka kupata msaada huu mkubwa toka South Korea, zimeshindwa kufikia matarajio yake.
Ukweli ni kuwa:
HOSPITALI YA MLOGANZILA INA VIFAA TIBA VINGI VYA KISASA AMBAVYO MADAKTARI WETU HAWANA UWEZO WA KUVITUMIA.
Kama serikali itaendelea na huu utaratibu wa kuzuia watu kwenda kusoma nje, yaliyopo Mloganzila, msitarajie yatabadilika.