Hospitali ya Taifa Muhimbili yajibu hoja za Wana JamiiForums kuhusu vifo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila

Nchi gani unayofahamu watu kwenda kupima bila ugonjwa? Yaani unakwenda hawa wanafunzi tunaowasema watafute ugonjwa mwilini?? Are you serious?

Ukipunguza mihemuko karibu tujadiliane,..,sasa hivi walaaa humpati Becky... yaani unashangaa kabisa watu kupima bila ugonjwa????????????duh ndio maana kazi ni rahisi sana kwa CCM kuongoza ... mweeeehhhhhh mashikolo mageni
 
85% wagongjwa mloganzila na MN1 ni rufaa....tuangalie hilo nalo !! Wameshindikana huko chini wa naenda kujaribu rufaa.....!! Professionalism vs sihasa Vs Ukweli
 
Huyu Professor amejikaanga kwa kutumia takwimu kujitetea. Na hajasema vifo vingapi vikitokea ndipo atakubali kuna tatizo!

Sifa ya MNH iliporomoka pale walipompasua kichwa mgonjwa badala ya goti! Hakukuwa na taarifa kama wahusika waliwajibishwa.

Hili la madokta vijana walionyoa viduku na kuonekana wana-gossip mbele ya wagonjwa halijibiki kwa takwimu!

Wananchi wanalalamika kwasababu Muhimbili na Mlonganzila ni tegemeo lao kuu kimatibabu. Serikali nayo imewekeza fedha na raslimali nyingi ikitegemea taasisi hii iwe na kiwango cha kimataifa kweli!

Lakini kama ndio hivi mtu akipoteza mpendwa wake akishangaa anajibiwa kwa takwimu, hatufiki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha.. Ni "combi" zote wanapewa "nyanya" siku hizi au Ni hyo PcB tuu??
 
Mkuu what is your advice then?
Shall we dwell on the past in our entire life?
Kama kulikuwa na vipimo duni lakini sasa kuna unafuu mkubwa, kwa hivyo bado tuendelee kutokwenda kupima afya yetu mara kwa mara kabla ya kuugua na kuzudiwa?
Kuna magonjwa mengi sana yanauwa watu ambayo kama wahanga wangeenda mapema hospital yalikuwa yanatibika.
 
Tunahitaji uwekezaji wa kutosha kwenye vifaa tiba kuanzia ngazi za zahanati na vituo vya afya. Sehemu kubwa ya magonjwa yanayotusumbua yanatibika vizuri sana kama yatapata vipimo sahihi na kwa wakiti, lakini huku makwetu hali siyo shwari kabisa kwa upande wa vipimo na vifaa tiba kwa ujumla ikiwemo na tatizo sugu la madawa. Tutatue changamoto hizi kwani watu watapata tu mwamko wa kwenda kupima kama huduma hizo zinapatikana kwa urahisi huko waliko. Kuna vituo vya afya na zahanati zina majengo mazuri sana lakini unakutana na incharge anakuambia tunatumia uzoefu na maelezo ya mgonjwa kujua anachoumwa.
 
Nimepitia maelezo na comments zote jibu rahisi sana kwa wastani ni kwamba yale maelezo ya hospital huyu prof. amepika kwa kiwango cha juu zaidi yaani zaidi.

Nashkuru wadau kwa hizi taarifa tuwajuwao tutawatahadharisha na hii hospitali. Kwamba kila wagonjwa 200 wagonjwa 10 hufariki kwa mujibu wa taarifa zao na ukija kwenye uhalisia hii hospitali inatisha haifai. Na hawa wagonjwa 200 hawa ni jumla jamala kwamba kuna wanaoumwa flue, kahoma, kichwa, jino, tumbo la kuharisha nk.

Kuna shida kubwa sana kwenye hii hospitali.
 
Na huu ndio ukweli. Siasa ndio inaua watu. Mloganzila haikua tayari kupokea wagonjwa kwa ukubwa huu wa sasa hali ya kuwa haina wafanyakazi. Madaktari bingwa na wale wa muhimbili, wahudumie muhimbili na mloganzila ambapo wengi hawataki kwenda mloganzila kwanza mbali na madaktari bingwa wote wana visehemu vyao vya kuhudumia mjini hapa. Walishazoea muhimbili, part time zao katika hospital zingine then anaenda kutulia kwenye kituo chake.

Na pia kama wameweka mgomo baridi cause they all know the purpose ya mloganzila haikua hii aliyoifanya mzee baba. Haya ndio matatizo ya nchi zetu hizi kila anaekuja anataka kuanzisha kitu chake kipya na sio kuendeleza vision za aliepita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa MUHIMBILI, JKCI na MOI kidogo Naona wako serious na kazi..

Typed Using KIDOLE
 
Sibariki ku cramm sababu sikufanya hivyo

Ila uliposuggest kutumia kiswahili kwenye medical synom umeniacha hoi sana mkuu

Mawazo mengine upo sahihi ila hili haliwezekani
Kwa hio unabariki ku cramm?! Mageni Haya!
 
Sibariki ku cramm sababu sikufanya hivyo

Ila uliposuggest kutumia kiswahili kwenye medical synom umeniacha hoi sana mkuu

Mawazo mengine upo sahihi ila hili haliwezekani

Mbona Wachina, Warusi wanatumia lugha zao katika kufundishia?
 

Hebu jibu hayo maswali kama hujapata sufuri kenge wewe
 
Wakati mwingine inabid tuelewe hospital ya rufaa ya taifa haziendi malaria na Uti, wagonjwa wenye terminal illness ni wengi lazima mortality itasoma high, tusilaumu sana.

Samsung A50
 
Kwanza hakuna chochote kipya hapo. Asingeweza kubali hayo madai. Halafu upuuzi zaidi hivi ni lazma wagonjwa wakiongezeka na vifo viongezeke!? Hapo kuna walakini. Siku zote Maelezo marefu ni uongo. Prof fungua kichwa.
 
Wakati mwingine inabid tuelewe hospital ya rufaa ya taifa haziendi malaria na Uti, wagonjwa wenye terminal illness ni wengi lazima mortality itasoma high, tusilaumu sana.

Samsung A50
Hili neno mortality ndo mumelitumia sana kwenye maelezo yenu nadhan hapo ndo mumepika zaidi, mbona hamjajibu hoja za wagonjwa waliopelekwa wiki hii lakin daktari anakuja kumtembelea wiki ijayo? na kuna madaktari 52 bingwa zaidi

Hakuna ulazima wa kila wagonjwa 400 wagonjwa 20 wafe izi ni takwimu za kupika pika tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…