Hospitali ya Wilaya ya Hai, kumwambia Mama mjamzito anunue vifaa vya kujifungulia ni sahihi kweli au kawaida

Hospitali ya Wilaya ya Hai, kumwambia Mama mjamzito anunue vifaa vya kujifungulia ni sahihi kweli au kawaida

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Nimeshangaa na sijaelewa sera ya Serikali kwa kina Mama Wajawazito, tuliambiwa Mama mjamzito kujifungua ni bure ana hudumiwa, sasa Hospitali ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Mama mjamzito anaambiwa akanunue Pamba ile kubwa, Gloves na akanunue Vidonge vya kuongeza damu na dawa zingine eti wao hawana kweli?

Wizara ya Afya chini ya Doroth Gwajima na Mollel mjitathmini mnapo simama majukwaani na kujinadi kwamba mnatoa huduma ya kina Mama wajawazito bure, nilicho kifanya mimi kwakuwa nilikuwa naelekea Arusha nikaambiwa kuwa mdada anajifungua ambaye ni ndugu nilimpa sh elf6 ya Pamba, Gloves elf 1, Dawa za kuongeza damu elf 4,000 nikaambiwa kwakuwa siku zake bado kidogo anunue dawa zimsaidie mtoto asitoke kabla siku hizo chache anasubiri dawa Hawana zinauzwa elf15 x 3 sasa nikampa hela akaenda kununua.

Hivi Serikali haya maneno yenu kuhusu huduma bure kwa wajawazito iko wapi, ni hapa Wilaya ya Hai tu au na kwingine. Sasa nakumbuka mnavyo jinadi mnasema mnalipa watu Pensheni huku mnakwepa kuzungumzia Mafao ya walio na mwaka hawajalipwa wakiwemo Askari Polisi. Tunako kwenda Mtakubali tu kwamba mmezidiwa sera hazifanyi tena kazi.
 
Ukiwapa ma nesi iyo hela wanakupa vifaa hapo wanavyo sasa wao wanavitoa wap
ndio umegundua hili leo?? ni kote atajifungua bure lakini vifaa unanunua na havizidi 20,000 labda sehemu uliopo
 
Mkuu kwani huyo ndo mwanao wa kwanza?

Mbona hayo mambo ya kawaida...

Hospitali zote iko ivo kasoro Muhimbili tuu.

Kwingine unaenda na vitu vyako, tena wakati kliniki mnaambiwa kabisa andaa hiki na hiki na kile.
Mhimbili ni Hospitali ya serikali hawafanyi hivyo na hospitali zingine za serikali kwanini Hawafanyi kama Muhimbili au kna madaraja kwenye hizi hospitali
 
Vifaa vya kujifungulia havizidi 20,000. Nunua. Peleka Mama akajifungue hospitali.
 
Vifaa vya kujifungulia havizidi 20,000. Nunua. Peleka Mama akajifungue hospitali.
Nyio ndio mnaisapoti serikali kwamba huduma ni bure basi waseme ni kulipia
 
Mhimbili ni Hospitali ya serikali hawafanyi hivyo na hospitali zingine za serikali kwanini Hawafanyi kama Muhimbili au kna madaraja kwenye hizi hospitali
Mkuu, kama ulikuwa siasa zenye siasa ndo jua kuanzia leo, kinachohubiriwa na wanasiasa majukwaani ni tofauti na kilichopo kwa ground.

IMG_20200122_062537.jpg
 
Mkuu kwani huyo ndo mwanao wa kwanza?

Mbona hayo mambo ya kawaida...

Hospitali zote iko ivo kasoro Muhimbili tuu.

Kwingine unaenda na vitu vyako, tena wakati kliniki mnaambiwa kabisa andaa hiki na hiki na kile.
Mimi wanagu wote walizaliwa Marekani siwezi zaa kwa sasa huyo mtoto ni wa ndugu flan hivi nimempa hela akanunue
 
Huu utaratibu wa kujinunulia upo nchi nzima,alafu ndo kulikuwa na mbuzi anawadanganya watanzania wafyatue tu wakati hospital hazna dawa na vifaa
 
Mimi wanagu wote walizaliwa Marekani siwezi zaa kwa sasa huyo mtoto ni wa ndugu flan hivi nimempa hela akanunue
Enhee vzr sana, hebu tupe experience Marekani wanafanyaje?

Nachojua huko kila kitu kinapatikana hospitali, na mwisho wa siku baada ya huduma mtu akipewa bill analipa bila longolongo.

Ila bongo wanasiasa wanajinadi majukwaani kwamba huduma ya mama mjamzito na watoto chini ya miaka 5 ni bure, lakini unakuta hakuna fungu lililopelekwa kucover hayo matibabu ya mama na mtoto, mwisho wa siku unakuta hospitali hawana chochote, hivyo option inayobaki ni mgonjwa kuambiwa kanunue vitu moja, mbili tatu uhudumiwe la sivyo hupati huduma. Na wahudumu hawana namna nyingine zaidi ya hiyo.

Hivyo wa kulaumiwa siyo hospitali bali wanaoexecute sera zilizowekwa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mbona kama unamfokea hivi??
Utadhani mm ndo mtunga sera[emoji23]

Nampa mpaka evidence lkn hataki kuamini ndicho kinachofanyika kwa ground, ila huko majukwaani wanahubiri vitu tofautiii.
 
Mimi wanagu wote walizaliwa Marekani siwezi zaa kwa sasa huyo mtoto ni wa ndugu flan hivi nimempa hela akanunue
Watoto wako wanaweza kuzaliwa marekani,lakini wewe mwenyewe ni masikini wa kutupwa,achilia mbali elimu kukupiga chenga maana hata kuandika tu mtihani............yaani umtie mimba mwanamke wako,serikali ije kukulipia?...acha ujinga basi
 
Back
Top Bottom