Hospitali ya Wilaya ya Hai, kumwambia Mama mjamzito anunue vifaa vya kujifungulia ni sahihi kweli au kawaida

Hospitali ya Wilaya ya Hai, kumwambia Mama mjamzito anunue vifaa vya kujifungulia ni sahihi kweli au kawaida

Nimeshangaa na sijaelewa sera ya Serikali kwa kina Mama Wajawazito, tuliambiwa Mama mjamzito kujifungua ni bure ana hudumiwa, sasa Hospitali ya WIlaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Mama mjamzito anaambiwa akanunue Pamba ile kubwa, Gloves na akanunue Vidonge vya kuongeza damu na dawa zingine eti wao hawana kweli????

Wizara ya Afya chini ya Doroth Gwajima na Mollel mjitathmini mnapo simama majukwaani na kujinadi kwamba mnatoa huduma ya kina Mama wajawazito bure, nilicho kifanya mimi kwakuwa nilikuwa naelekea Arusha nikaambiwa kuwa mdada anajifungua ambaye ni ndugu nilimpa sh elf6 ya Pamba, Gloves elf 1, Dawa za kuongeza damu elf 4,000 nikaambiwa kwakuwa siku zake bado kidogo anunue dawa zimsaidie mtoto asitoke kabla siku hizo chache anasubiri dawa Hawana zinauzwa elf15 x 3 sasa nikampa hela akaenda kununua.

Hivi Serikali haya maneno yenu kuhusu huduma bure kwa wajawazito iko wapi, ni hapa Wilaya ya Hai tu au na kwingine. Sasa nakumbuka mnavyo jinadi mnasema mnalipa watu Pensheni huku mnakwepa kuzungumzia Mafao ya walio na mwaka hawajalipwa wakiwemo Askari Polisi. Tunako kwenda Mtakubali tu kwamba mmezidiwa sera hazifanyi tena kazi.
Hiyo mimba ilitokea pasipo mpango? Mbona vitu basic sana hivyo?
 
20,000 ya kuanza clinic wapi hapo tena!
mama ndio system sasa hivi, ukianza andaa 15000 ultra sound sjui eneo uliopo ni bei gan ultra sound huku ni elf 15 kisha andaa kama 20,000 ya vipimo vya mwanzo kabisa kuanza clinic baada ya hapo unavoendelea ni bure na vifaa pia unanunua
 
Mke wangu laijifungua 2016, hatukununua chochote wala kulipia chochote.
mimi nilijifungua 2019 nilinunua vifaa kibaya zaidi huu mwaka 2021 ukianza na clinic unalipia vizuri sana na kila hospital ziko na gharama zake
 
yani laki tu unalialia huku, acha kupenda dezo UTAOLEWA.
Tatizo ni pale tunapotangaziwa huduma ni bure kwa watoto chin ya miaka 5 na wajawazito alafu ukienda unalipishwa si bora watangaze kiasi maalum ili mtu anatakiwa kulipa kuliko hii ya kushtukizana? na ukisoma comments za wadau hapo juu Kila mmoja ana kias chake alichotoa na wote tuko nchi moja na hospitali ni za serikali ww huoni kama ni tatizo?
 
Naona inategemea na uongozi nafikiri....ziko mahali mjamzito akifanyiwa operation unalipa utafikiri private uchwara zile za gharama nafuu
huyo mkewe kajifungua 2016 huko hizi mambo zimeanza hapa karibuni zamani pia naskia kulikua na bima bure kwa mama mjamzito haipo tena yan sasa hivi kila kitu unalipia hata ukitaka wahudumu wa kukuhudumia hospital kama malkia washikishe elf kumi yan watakufata fata
 
ndio umegundua hili leo?? ni kote atajifungua bure lakini vifaa unanunua na havizidi 20,000 labda sehemu uliopo
Huko kumbe hivyo vifaa bei nafuu, huku nilipo ni around 28,000 - 30,000
 
Mkuu kwani huyo ndo mwanao wa kwanza?

Mbona hayo mambo ya kawaida...

Hospitali zote iko ivo kasoro Muhimbili tuu.

Kwingine unaenda na vitu vyako, tena wakati kliniki mnaambiwa kabisa andaa hiki na hiki na kile.
Hadi Muhimbili wananunua vifaa, niliwahi kumnunulia Pamba mke wa jirani, maana mume hakuwa karibu na Hospital, mimi nilikuwa hapo Hospital Manesi waliniambia kanunue Pamba
 
Hadi Muhimbili wananunua vifaa, niliwahi kumnunulia Pamba mke wa jirani, maana mume hakuwa karibu na Hospital, mimi nilikuwa hapo Hospital Manesi waliniambia kanunue Pamba
Shida watz hawajiongezi... Wanataka hata hizo pamba za kufunga kama pedi baada ya kujifungua eti serikali nayo itoe.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Shida watz hawajiongezi... Wanataka hata hizo pamba za kufunga kama pedi baada ya kujifungua eti serikali nayo itoe.
Kosa sio letu, kosa ni hawa wanaotuambia bure.

Hiyo bure wanatakiwa watuambie mipaka yake. Sio wakisema bure, sisi tunashika kuwa ni bure kweli kweli
 
Ni kawaida hiyo mkuu.....yaani mimba uweke wewe halafu serikali ndio imuhudumie mkeo wakati wa kujifungua.......nini maana ya neno" kujipanga"
 
Tatizo ni pale tunapotangaziwa huduma ni bure kwa watoto chin ya miaka 5 na wajawazito alafu ukienda unalipishwa si bora watangaze kiasi maalum ili mtu anatakiwa kulipa kuliko hii ya kushtukizana? na ukisoma comments za wadau hapo juu Kila mmoja ana kias chake alichotoa na wote tuko nchi moja na hospitali ni za serikali ww huoni kama ni tatizo?
Huduma ni bure ila kwa wakati unahitaji Huduma kwa bahati mbaya vifaa havipo, je wakuache kukuhudumia au ujipapase mifukoni kwa kununua vifaa ili uhudumiwe!
 
15000 labda uondoe mpira, duka la jumla mpira ni 9000, gloves ni 900 kwa pair, weka blades, umbilical cord, uzi. Hiyo bei uliyosema umeipataje?
 
Back
Top Bottom