Hospitali ya Wilaya ya Hai, kumwambia Mama mjamzito anunue vifaa vya kujifungulia ni sahihi kweli au kawaida

Sasa bahati mbaya afanyiwe operation si ndo utachanganyikiwa
 
Hospitals nyingi tuu hivyo vifaa wazazi wananunua. Mimi binafsi wanangu wote nimenunua package ya kujifungulia .
 
Wanasiasa wachonganishi sana wanatangaza huduma kwa mama mjamzito kuanzia clinic ni bure.
Mama mjamzito akianza clinic kwanza kabisa akatoe photocopy ya kadi then mambo mengi yaendelee.kupima VVU,fetalheart,umri wa mimba na mrdt hivyo bure kabisa.
Hb,mkoja wa kutambua protein na sukari,kaswende hivyo mama lazima na siyo chini ya elfu 15-20.
Bado siku ya kujifungua vifaa vichache wanaojifungua ni wengi hapo ndio unapokuja mtihani.Mwisho wa siku waganga na wauguzi wanatupiwa lawama.
 
Wife alijifungualia hospitali ya serkali Magunga kwa operation nililipa karibu lake nzima
 
Na siku ya kujifungua ukitaka huduma nzuri pia shikisha nurse ata efu10 tena
 
Wilaya ni kubwa. Hai sehemu gani ? Ili tufikishe ujumbe vizuri
 
ndio umegundua hili leo?? ni kote atajifungua bure lakini vifaa unanunua na havizidi 20,000 labda sehemu uliopo
Mke wangu laijifungua 2016, hatukununua chochote wala kulipia chochote.
 
Nchi jirani apo 🇰🇪 wanaposema huduma ya mama mjamzito na mtoto ni bure wanamaanisha! Yaan hata ufanyiwe operation private hospital ukiwa na ile Linda mama yao wao wanaiita, hutoi ata ten bob na haisumbui ata kumshika nurse mkono wala Dr na wako smart kiasi chake kwenye huduma
 
Bado nashangaa ni wapi huko? Mbona mm mke wangu alipojifungua hatykulipa chochote?
Naona inategemea na uongozi nafikiri....ziko mahali mjamzito akifanyiwa operation unalipa utafikiri private uchwara zile za gharama nafuu
 
Watoto wako wanaweza kuzaliwa marekani,lakini wewe mwenyewe ni masikini wa kutupwa,achilia mbali elimu kukupiga chenga maana hata kuandika tu mtihani............yaani umtie mimba mwanamke wako,serikali ije kukulipia?...acha ujinga basi
Shkamoo blaza[emoji850]
 
Ukiendekeza siasa hii nchi utakufa..
Kwa experience yangu hakuna huduma inayotolewewa bureee kabisa.. labda kupima HIV..

Ukiwa na mgonjwa hata kama ni mtoto wa miezi miwili. Andaa pesa yako ya kutosha tu kwa ajili ya matibabu la sivyo mwanao atakufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…