Hospitali za private (binafsi) zatishia kutohudumia wagonjwa wanaotumia bima ya afya ya NHIF

Hospitali za private (binafsi) zatishia kutohudumia wagonjwa wanaotumia bima ya afya ya NHIF

Ni aibu kuchelewesha malipo kwa wadau wa afya. Hii inazorotesha huduma katika vituo binafsi, ama NHIF wanataka hospitali binafsi zife ili wafungue wao!

nafikiri natitizo hapa ni kutumia makaratasi kitu ambacho kimepitwa na wakati lakini pia ni rahisi kupata taarifa zisizo na uhalisia (kuchakachua taarifa)
NHIF wanaweza kugawa vishikwambi vilivyounganishwa kwenye mfumo na watoa huduma wavinunue kwa bei ya huduma au basi watengeneze app ambayo kila Hospitali inakuwa na password yake ya kuingia na kuweka data (mbele ya mgonjwa); hata sijui wanakwama wapi?
 
Yaani ni mtihani mkubwa.

Na hiyo bima ya afya kwa wote ili hali isipokuwa kwa wachache nanga zilipaaa sembuse kwa wote?

Tutarajie mbilingembilinge kama za Tanesco kupeleka umeme vijijini bila mkakati Sasa wanakwama?!
 
Yaani wangeenza kuboresha kwa wachache kwanza,

Sasa wachache ilishindikana kutoa huduma bora kwa wakati sembuse kufanya kwa wote wote?

Unatarajia nini kwa mfano?
 
Afya za watanzania zinabishaniwa na watoa huduma na serikali. Tutakufa tu ili mubaki na pesa zetu tunazochangia huu mfuko
 
Afya za watanzania zinabishaniwa na watoa huduma na serikali. Tutakufa tu ili mubaki na pesa zetu tunazochangia huu mfuko
Msife jamani, mkifa mfuko utakosa michango, michango ikikosekana tutashindwa kununua gari mpya ya mkurugenzi😬
 
Hii ada ya kumuona daktari kwa kweli ingefaa ifutwe kabisa!!!
Kwani si ana mshahara, ama hiyo ada ndio inatumika kumlipa mshahara?
Kama vipi ingewekwa ada pia mzazi akitaka kuonana na mwalimu alipe, ukiingia ofisi yoyote lipia!!!
Umeuliza swali na kukujibu mwenyewe majibu sahihi kabisa.
 
Mbadala wa serikali unayotaka kuiangusha ni nini?

Ni vyama hivi hivi vya upinzani?

watanzania wenye akili na uwezo wa kuongoza hii nchi na ikapata maendeleo kwa haraka wapo wengi sana mitaani humu

Hatuhitaji vyama vya siasa au wanasiasa kuongoza hii nchi, tunapaswa kufanya mapinduzi ya kiraia na kuunda baraza la mpito litakalohusisha watanzania wote, kuanzia nyaishozi, kishumundu, kemakolele, kitele, Nanyamba mpaka kule Ileje nk... Kupitia Baraza hilo tutapiga marufuku wale wote wahuni waliofikisha hii nchi hapa na hawa wanasiasa wa upinzani kujihusisha na siasa na baadala yake utawekwa mfumo utakaosimamia chaguzi zote na kila mtanzania tajiri na masikini awe na uwezo wa kusimama kwenye jukwaa la siasa, kunadi sera zake na kusikilizwa na maamuzi huru ya watanzania yaheshimiwe..

SHIDA KUU YA HII NCHI NI CCM NA WATU WAKE WANAOAMINI KATIKA GIZA.
 
Huduma za Afya zinabishaniwa na watoa huduma, NHIF na Madaktari, Wapokea huduma wao nani anawasemea kero zao? Au kuna niia ipi ya kusikilizwa katika hivyo vikao vyenu?
 
Duh!! kati ya jambo baya basi ni hili,NHIF kama wamefilisika watuache wanachma hasa waajiriwa tuchague mifuko ya kutuhudumia,huu ni uhuni ambao unaenda kufanya majaribio kwenye afya zetu,binafsi niko tayari kukatwa hata laki nane kwa mwaka toka kwa salary yangu ilimradi tu nipate hudumu bora,sasa,hili la kung'ang'ania wanachama huku wakipata huduma mbovu ni jambo baya sana na linalenga kuweka rehani afya zetu .

Haiiwezekani huduma zingine ziko juu harafu wao NHIF wnakuja na mapendekezo ya kuvibana vItuo vya afya vya binafsi,kama wanaona inafaa hilo punguzo lifanyike kwa hospital za government na sio kwenye biashara za watu.


Mungu tusaidie waja wako
 
Serikali ya CCM ilisha wahi kufanikisha jambo gani? Hi Bima lazima itakufa au itazorota tu hivo hivo mpaka raia waikimbie wenyewe.
Huwezi kuikimbia mkuu ikiwa waajiriwa tunaunganishwa na mfuko bil ridhaa yetu,kama wamefirisika wajitoe au watuache wanachama tujichagulie mifuko ya kutuhudumia
 
Umeuliza swali na kukujibu mwenyewe majibu sahihi kabisa.
Hii ada ya kumuona daktari kwa kweli ingefaa ifutwe kabisa!!!
Kwani si ana mshahara, ama hiyo ada ndio inatumika kumlipa mshahara?
Kama vipi ingewekwa ada pia mzazi akitaka kuonana na mwalimu alipe, ukiingia ofisi yoyote lipia!!!
Mfano ukaenda bure , ila kichwa kinauma, miguu haina nguvu na joto liko juu ila akukuambia hauna shida yoyote nenda tu nyumbani utajisikiaje?
 
Mfano ukaenda bure , ila kichwa kinauma, miguu haina nguvu na joto liko juu ila akukuambia hauna shida yoyote nenda tu nyumbani utajisikiaje?
Kwahiyo hiyo pesa ni Kwa ajili ya daktari kumweleza mgonjwa kinachomsumbua?
 
Tunalalamika bure na kuacha kuangalia vitu Muhimu mfano hai kuongezeka kwa jumla ya dawa 124 katika Orodha ya dawa Muhimu ya Taifa sio hivyo tu kuweka mbadala wa dawa 309 katika kitita cha Mafao huku kukijumuishwa dawa zenye nguvu na muundo wa upatikanaji wa dawa katika Soko haya vituo binafsi hawaoni ila wanaangalia tu sehemu Yao ya kupata faida haipo
 
Back
Top Bottom