Hospitali za private (binafsi) zatishia kutohudumia wagonjwa wanaotumia bima ya afya ya NHIF

Hospitali za private (binafsi) zatishia kutohudumia wagonjwa wanaotumia bima ya afya ya NHIF

Hizi hospital binafsi hawaongelei waliongezewa malipo ya ada kutoka elfu kumi na Tano 15000 Hadi elfu ishirini 20000 ambao ndo wengi hapa hili hawalioni tuache maneno wakati wa maboresho Mfuko ulihusisha wadau wote wakiwamo hao umoja wa wamiliki binafsi (APHTA )
 
Mfuko wa Bima ya Afya hawajakurupuka walikaa walipo Fanya maboresho ya kitita waliwashirikisha Wadau wote na waliangalia maeneo muhimu ikiwemo Ada ya Usajili na ushauri wa Daktari hapa ni kuweka usawa ada ya kumuona Daktari kwa kuzingatia taaluma wakaongeza kutoka elfu 15000 mpaka 20000 lakini huduma za dawa kukafanyika mabadiliko ya gharama kwa kuzingatia tafiti za Bei za huduma katika kinadi dawa cha MSD na maoni ya Wadau mfano Diclofenac 50mg ilikuwa 1300 lakini imefikia 1432 hili hawalioni kwa Kuna faida na ni dawa zote wao wanachongangania sijui ni kipi vituo binafsi bila shaka Kuna sehemu wameshikwa pabaya
 
Tunapozungumza kuwa hospital binafsi Kuna vitu wamevificha hawaviongelei na sijui ni kwanini sababu awali walikuwa wanavipigia kelele mfano kulikuwa na usumbufu kwa wanachama kunyimwa baadhi ya huduma kutokana na Bei ya kitita cha 2016 sasa limekuja suruhisho kitita Kipya kimeondoa usumbufu huo sasa Bei zote za dawa zimeainishwa kwenye Bei ya Soko lakini kupungua kwa Makato yasiyo ya lazima kutoka kitita cha 2023 sasa huku hakutakuwa hivi yaaaani Kila sehemu ni faida wanacholalamikia hawakisemi
 
Tunalalamika bure na kuacha kuangalia vitu Muhimu mfano hai kuongezeka kwa jumla ya dawa 124 katika Orodha ya dawa Muhimu ya Taifa sio hivyo tu kuweka mbadala wa dawa 309 katika kitita cha Mafao huku kukijumuishwa dawa zenye nguvu na muundo wa upatikanaji wa dawa katika Soko haya vituo binafsi hawaoni ila wanaangalia tu sehemu Yao ya kupata faida haipo
Gharama uendeshaji ni kubwa Sana kwa vituo binafsi itafika stage wataanza kukwepa watu NHIF hizo dawa ndio wameongeza Kama huko kwenye hospital hamna wamezuia kwenye Maduka ile form 2c siku hiz hamna. Kuna usumbufu mwingi. Ndio maana baadhi ya hospital zimeanza kuwapa kipaumbele wenye kadi za bima za kampuni binafsi.
 
nafikiri natitizo hapa ni kutumia makaratasi kitu ambacho kimepitwa na wakati lakini pia ni rahisi kupata taarifa zisizo na uhalisia (kuchakachua taarifa)
NHIF wanaweza kugawa vishikwambi vilivyounganishwa kwenye mfumo na watoa huduma wavinunue kwa bei ya huduma au basi watengeneze app ambayo kila Hospitali inakuwa na password yake ya kuingia na kuweka data (mbele ya mgonjwa); hata sijui wanakwama wapi?
Ni wazo zuri hili. Dunia imebadilika sana.
 
Back
Top Bottom