SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
UTANGULIZI
Nikiwa wodini nauguza mgonjwa wangu katika moja ya hospitali kubwa ya Rufaa nchini, Nilimsikia daktari mmoja akitumia lugha ya kiingereza kuwaambia wanafunzi wanao somea udaktari ambao walikuwa wakitoa huduma kwa mgonjwa aliyekuwa kitanda cha pembeni na alicho mgonjwa wangu maneno haya nanukuu "MMEKOSEA, HAMKUTAKIWA KUMCHOMA SINDANO HIYO". Hakika nafsi yangu iliogopa sana, Nilihisi kana kwamba amefanyiwa mgonjwa wangu, hivyo niliwaza iwapo angekuwa ni mgonjwa wangu na nimesikia maneno yale ya daktari ningechukua hatua gani. Ilinifanya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mgonjwa yule tokea siku ile kwasababu nilikuwa pale kwa wiki moja nikimuuguza mgonjwa wangu, Baada ya siku moja nilipewa taarifa kuwa Mgonjwa yule alifariki Dunia.

Hospitali zetu za rufaa zimekuwa kimbilio kwa walio wengi katika suala zima la matibabu, hii ni kutokana na kuaminika kwamba zina wataalamu wa kutosha. Lakini pia zinaweza kutoa huduma za kibingwa. Kwa hapa kwetu Tanzania tumebarikiwa kuwa na Hospitali za rufaa za mikoa lakini pia tuna hospitali za rufaa za kanda kama vile HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KCMC, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO pamoja na hospitali kubwa ya taifa MUHIMBILI. Hospitali hizi za rufaa za kanda zina Vyuo ambavyo hutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya kama vile madaktari, manesi na wafamasia. Vyuo hivyo ni MUHAS,BUGANDO, MCHAS, na KCMCo pamoja na vyuo vingine vinavyopatikana katika hospitali za mikoa na Hospitali zingine za Binafsi na mashirika ya dini.

Wanafunzi hawa wa udaktari walioko wafunzoni wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa vitendo katika hospitali zetu jambo ambalo ni Zuri kwani linawajenga na kuwaimarisha vyema katika Sekta hiyo muhimu ya afya. Lakini pia wamekuwa wakirahisisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza wahudumu wa afya katika hospitali zetu ukizingatia kwamba vituo vingi vya afya pamoja na hospitali zetu Bado zina changamoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa Afya. Kwa ujumla wanataalamu hawa walioko mafunzoni hususani madaktari wanafanya kazi kubwa.

TATIZO LINAANZIA HAPA.
Kwa Bahati mbaya, hospitali zetu zimewaamini Wanafunzi hawa walioko vyuoni kupitiliza kiasi cha Kuwapangia Zamu za kuwaona wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu na kufanya matibabu kwa mgonjwa hata kwa wagonjwa ambao wako katika hali mbaya. Jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya ya mgonjwa. Hii imesababisha kutokea kwa vifo vingi kutokana na kwamba wanafunzi hawa wa afya hawajawa bado na Utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za afya kwa kiwango kinachostahili ukilinganisha na madaktari wazoefu.

CHANZO CHA TATIZO.
Ni kweli kwamba siku hizi Teknolojia imerahisisha ufanyaji wa kazi katika hospitali zetu.Teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya na Hospitali, na ndio maana utakuta Daktari anayeingia katika zamu ya usiku anaweza kumfahamu vizuri mgonjwa aliyelazwa wodini, matibabu aliyoyapata na matibabu anayotakiwa kuyapata hivyo kumrahisishia kuendeleza matibabu kwa mgonjwa. Lakini ukuaji huu wa Teknolojia usiwe Sababu ya kuwaachia majukumu yote wanafunzi wa udaktari walioko Vyuoni kwani waliowengi bado hawajapata maarifa ya kutosha katika kutoa huduma za kitabibu. Lakini pia wingi wa hawa wanafunzi katika hospitali zetu kisiwe kigezo cha madaktari wazoefu na wenye majukumu ya kutoa huduma za afya kusahau wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa. Wengi wa hawa wanafunzi wa udaktari wamekuwa wakitoa huduma kwa hisia ili tu kukamilisha matakwa ya kozi wanazosomea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo. na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

ATHARI ZITOKANAZO NA TATIZO HILI.
Utakubaliana nami kuwa Siku zote Mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, hata kama ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne au wa tano. Na sifa mojawapo aliyonayo mwanafunzi ni kutokujiamini kwa asilimia mia moja, hivyo kupelekea kufanya jambo kwa Jazba na Mihemko ilimradi tu kukamilisha takwa fulani. Hivyo nilazima uongozi wa hospitali zetu uwachukulie wataalamu hawa wa afya kama wanafunzi na kuwasimamia katika huduma zote za kitabibu katika hospitali zetu kwa manufaa mapana ya mgonjwa na mtoa huduma.

Kutokana na kuwatumia madaktari mafunzoni katika hospitali zetu hizi za rufaa, Huduma katika hospitali hizi zimekuwa zikishuka kadiri siku zinavyokwenda licha ya serikali Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizi, ikiwa ni pamoja na Ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma za afya, Uongezaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya. Jambo hili si zuri kwasababu linapunguza imani kwa wananchi hivyo kutumia gharama kubwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi.

Usalama wa mgonjwa awapo hospitalini ni muhimu sana. Muda mwingi mgonjwa hubaki na wataalamu wa afya kwa ajili ya matibabu. Hivyo ndugu jamaa na marafiki huamini kuwa Daktari au mtaalamu yeyote wa afya ana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya Mgonjwa. Wote tunaamini kwamba mtaalamu yeyote wa afya anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha katika kumhudumia mgonjwa ili kuokoa maisha yake. Iwapo mtaalamu huyo wa afya atakosa ujuzi na maarifa ya kutosha maisha ya mgonjwa yatakuwa hatarini, na hata kuwa ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Lakini pia kukosekana kwa maarifa ya kutosha kutamfanya mtaalamu huyo kushindwa kujiamini katika kazi yake.

HITIMISHO
Madaktari walioko mafunzo pamoja na wataalamu wengine wa afya wanafanya kazi kubwa na nzuri katika kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali zetu, Lakini Uongozi wa hospitali zetu kwa kushirikiana na vyuo vinavyotoa wataalamu hawa wa afya hauna budi Kuwasimamia ipasavyo wakati wote wanapotoa huduma kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwapanga pamoja na Madaktari wazoefu ili kuifanya huduma yao ya matibabu iwe salama na yenye kuleta matumaini kwa mgonjwa na Kuepukana na Vifo vinavyotokana na UZEMBE wa watoa huduma za afya.

Wenu
Mwita Ngutunyi Mohono
S.l.p 237 Mbarali- MBEYA
0762185894
mwitangutunyimohono@gmail.com
 
Upvote 49
Wanafunzi wa chuo au Interns?..kama ni mwanafunzi wa chuo hilo ulilolisema haliwezekani.

Intern huwezi kumwita ni mwanafunzi..maana baada ya mwaka huo anakuwa yupo tayari kupractice..sasa unamwitaje mwanafunzi??

Nakubali inatakawa wafanye kazi kwa uangalizi lakini ulivyoandika ni kana kwamba wao ndo wanawaona wagonjwa toka mwanzo..kitu ambacho sio kweli kwenye hizi refferal hospital..

Interns wanaachiwa tu treatment plan baada ya ward rounds ambazo wapo pia na specialists na wanasimamia utekelezaji wake..kitu ambacho sio kigumu kufanya.
Ahsante .mwanajukwaa kwa kusoma andiko hili.

Hapa tunazungumzia wanafunzi wa udaktari ambao bado wapo masomoni. n sio INTERNS.

Usimamizi wakutosha kwa wataalamu hawa ni muhimu kwasababu wanahusika na maisha ya watu. Hata interns, pamoja na kwamba wamekwisha hitimu ni lazima wapate usimamiz wa kutosha katika utoaji huduma.

Kwa ujumla wataalamu hawawanafanya KAZI NZURI sana na Tunathamini kwa kiasi kikubwa mchango wao katika KUTOA HUDUMA
 
Refferal hospital zote zina Interns siku zote za mwaka...MD 4 or 5 hawawezi kuachiwa wagonjwa na Interns wapo,residents wapo pia..ni kitu ambacho hakiwezekani kwenye hospitali ya Rufaa

Kwahiyo uzi wako umekosa mantiki maana huna uhakika na unachokiongea.
 
Siku zote jambo linapogusa kada yako lazima utatafuta namna ya kudefend.

Lakini tambua kuwa huo ndio uhalisia na ni lazima kama wataalamu Tuwe wepesi wa kukubali madhaifu yetu ili kutusaidia kuwa bora zaidi.

Wewe unasema hakuna kitu cha NAMNA Una uhakika?. Wanao hudumiwa katika hospitali zetu hizi ndio watuambie.

Lakini pia mwanajukwaa Tambua kuwa andiko halina lengo baya na ndio maana mchango mkubwa wa wataalamu wa afya UMETAMBULIWA katika andiko hili.
 
Ni kweli mwana jukwaa.nimepita katika hospitali zetu nyingi hususan zile zenye vyuo vya afya na katika utafiti wangu mdogo nimegundua wanafunzi wengi wanaachiwa majukumu na madaktari walioko zamu. Hii inasababisha mgonjwa kuandikiwa dawa ambazo wakati mwingine daktari anaye ingia zamu kuzikataa na kuandika zingine. Jambo hili lipo na linahatarisha sana huduma za afya katika hospitali zetu.
Hakuna mwanafunzi anaandika dawa acha kupotosha

Fomu yotote ya dawa lazima iwe na sahihi ya daktari ambae yuko registered
 
Tatizo kubwa ni tamaa za hawa madaktari bingwa kuwa na kazi zao za nje. Jaribu kufikiria kuna mgonjwa mmoja tulimpeleka hospital ya serikali tukaambiwa na muunguzi mmoja twende hospital ya binafsi pale msasani aisee cha ajabu yule Daktari bingwa wa hospital ya serikali ndio tukamkuta hapo msasani. Tulijuta kwa hiyo bei. Hawa madaktari wameshakuwa na tamaa.
 
hata sisi ni wananchi , hakuna mwanafunzi anayeachiwa mgonjwa hospitali ya rufaa
Kabisa, kisheria hakuna anaeruhusiwa kupractice bila kua na lisence ya udaktari, mwanafunzi anaezungumziwa hapa kama ni md4,5 sidhani kama jambo hili linawezekana kwa sababu ya mfumo uliopo. Kwenye mfumo wa afya kuna hierache, kuna super specialist, specialist, medical officer, intern dr, student. Kwenye hizi hospital wengi wao utawakuta wodini ni intern dr, ambao hawa wapo lisenced kupractice baada ya kumaliza masomo ya udaktari na kufaulu. Na wapo under tight supervision na seniors wao niliowataja hapo.
Kuna resident ambaye huyu ni daktari anaesomea shahada ya pili ya udaktari ambaye yupo kwa ajili ya kujifunza kuwa daktari bingwa huyu ni daktari full kabisa sema na anafanya kazi chini ya usimamiz vilevile, suala la kisema undergrataduate anaachiwa wodi sio la kweli. Na hata kama ikitokea, kuna mtu amempa maelekezo nini cha kufanya.
 
Hakuna mwanafunzi anaandika dawa acha kupotosha

Fomu yotote ya dawa lazima iwe na sahihi ya daktari ambae yuko registered
Asante kwa kusoma andiko hili mwanajukwaa.

Kama Utakuwa umesoma vyema andiko langu, linajieleza vizuri. Huwenda umesoma kichwa cha habari pekee. Nadhani ipo haja ya kuelewa andiko linawahusu watu gani.

Hii ya wanafunzi wa udaktari kuachiwa majukumu ipo katika hospitali zetu.. na hivyo ni lazima mahusika wachukue tahadhari.

Najua binadamu sio rahisi kukubali madhaifu yake hata kama yako. Hajui kuwa anapoambiwa madhaifu yake yanamfanya kuwa bora zaidi.
 
hata sisi ni wananchi , hakuna mwanafunzi anayeachiwa mgonjwa hospitali ya rufaa
Usitetee HOJA tu kwasababu wewe ni mmoja katika kada hii muhimu ya Afya. Kubali udhaifu wako ili ukufanye kuwa bora zaidi.
 
Tatizo kubwa ni tamaa za hawa madaktari bingwa kuwa na kazi zao za nje. Jaribu kufikiria kuna mgonjwa mmoja tulimpeleka hospital ya serikali tukaambiwa na muunguzi mmoja twende hospital ya binafsi pale msasani aisee cha ajabu yule Daktari bingwa wa hospital ya serikali ndio tukamkuta hapo msasani. Tulijuta kwa hiyo bei. Hawa madaktari wameshakuwa na tamaa.
Asante mwanajukwaa kwa kuliona hili hiyo ni moja ya sababu ya kuacha Majukumu yao ya msingi katika hospitali hizi na kuwaachia wengine. Ipo haja ya mamalaka husika kuliangalia hili ili na kuchukua hatua stahiki.
 
Kabisa, kisheria hakuna anaeruhusiwa kupractice bila kua na lisence ya udaktari, mwanafunzi anaezungumziwa hapa kama ni md4,5 sidhani kama jambo hili linawezekana kwa sababu ya mfumo uliopo. Kwenye mfumo wa afya kuna hierache, kuna super specialist, specialist, medical officer, intern dr, student. Kwenye hizi hospital wengi wao utawakuta wodini ni intern dr, ambao hawa wapo lisenced kupractice baada ya kumaliza masomo ya udaktari na kufaulu. Na wapo under tight supervision na seniors wao niliowataja hapo.
Kuna resident ambaye huyu ni daktari anaesomea shahada ya pili ya udaktari ambaye yupo kwa ajili ya kujifunza kuwa daktari bingwa huyu ni daktari full kabisa sema na anafanya kazi chini ya usimamiz vilevile, suala la kisema undergrataduate anaachiwa wodi sio la kweli. Na hata kama ikitokea, kuna mtu amempa maelekezo nini cha kufanya.
Laiti hospitali zetu zingefuata utaratibu huo mnao tuambia kusingekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi. Lakini pia wasingepeleka wagonjwa katika hospitali za gharama kubwa ili tu kuokoa maisha ya ndugu zao.

Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais wetu mama SAMIA imewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya katika hospitali zetu, kuongeza vifaa vya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya.

Hivyo ni lazima mamlaka za hospitali zitoe huduma bora kuendana na uwekezaji uliowekwa.
 
Endeleza utafiti huwe mkubwa maana aujashibisha andiko lako kututhibitisha kuwa kuna mwananfunzi asiye sajiliwa kaachiwa mgonjwa kwa sababu hospital zote zenye vyuo ni za serikali.

Labda wewe umeongezea chumvi au maneno yako kwamba mwananfunzi alipo kuwa na daktari ambaye ni mwalimu wake kwa bahati mbaya alikosea dawa aliyo ambiwa na dokta ambaye alikuwa anamtibu mgonjwa alafu mwananfunzi wake akakosea dawa na siyo kaachiwa mgonjwa kwa sababu mwanafunzi ajui chochote.

Alafu ukitaka kujua kwa nini wananfunzi wa udaktari wanakuwa karibu sana maeneo ya matibabu nenda ukajiunge na hivyo vyuo usome ili ujue kwanini wananfunzi wanakuwa karibu na madaktari kwenye kutibu wagonjwa lakini hakuna mwananfunzi anaye achiwa mgonjwa kaka.
Mkuu umenena vyema hawa wanatuchukuliaje kimfano, wasione tunavaa zile koti watu tunasota
 
Mkuu umenena vyema hawa wanatuchukuliaje kimfano, wasione tunavaa zile koti watu tunasota
Na hapa ndipo tatizo linaanzia mwanajukwaa. Nashindwa kuamini kuwa wewe ni mtaalamu wa afya kwa namna ulivyomjibu mwenzako.

Nyie ni watu muhimu sana katika jamii. Na kwakweli tunawapongeza na kuiomba serikali iendelee kuboresha mazingira yetu.

Tatizo linakuja pale mnapokataa madhaifu yaliyopo katika hospitali zetu ili ziweze kuwaweka vizuri sana na kutoa huduma bora.

Shida sio kuvaa koti na kusota. Wanannchi wanawapima kwahuduma bora mnazotoa.
 
Kabisa, kisheria hakuna anaeruhusiwa kupractice bila kua na lisence ya udaktari, mwanafunzi anaezungumziwa hapa kama ni md4,5 sidhani kama jambo hili linawezekana kwa sababu ya mfumo uliopo. Kwenye mfumo wa afya kuna hierache, kuna super specialist, specialist, medical officer, intern dr, student. Kwenye hizi hospital wengi wao utawakuta wodini ni intern dr, ambao hawa wapo lisenced kupractice baada ya kumaliza masomo ya udaktari na kufaulu. Na wapo under tight supervision na seniors wao niliowataja hapo.
Kuna resident ambaye huyu ni daktari anaesomea shahada ya pili ya udaktari ambaye yupo kwa ajili ya kujifunza kuwa daktari bingwa huyu ni daktari full kabisa sema na anafanya kazi chini ya usimamiz vilevile, suala la kisema undergrataduate anaachiwa wodi sio la kweli. Na hata kama ikitokea, kuna mtu amempa maelekezo nini cha kufanya.
Kuna haja ya kusoma makala hii upya ili uweze kuelewa mwanajukwaa.
 
Back
Top Bottom