SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
UTANGULIZI
Nikiwa wodini nauguza mgonjwa wangu katika moja ya hospitali kubwa ya Rufaa nchini, Nilimsikia daktari mmoja akitumia lugha ya kiingereza kuwaambia wanafunzi wanao somea udaktari ambao walikuwa wakitoa huduma kwa mgonjwa aliyekuwa kitanda cha pembeni na alicho mgonjwa wangu maneno haya nanukuu "MMEKOSEA, HAMKUTAKIWA KUMCHOMA SINDANO HIYO". Hakika nafsi yangu iliogopa sana, Nilihisi kana kwamba amefanyiwa mgonjwa wangu, hivyo niliwaza iwapo angekuwa ni mgonjwa wangu na nimesikia maneno yale ya daktari ningechukua hatua gani. Ilinifanya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mgonjwa yule tokea siku ile kwasababu nilikuwa pale kwa wiki moja nikimuuguza mgonjwa wangu, Baada ya siku moja nilipewa taarifa kuwa Mgonjwa yule alifariki Dunia.

Hospitali zetu za rufaa zimekuwa kimbilio kwa walio wengi katika suala zima la matibabu, hii ni kutokana na kuaminika kwamba zina wataalamu wa kutosha. Lakini pia zinaweza kutoa huduma za kibingwa. Kwa hapa kwetu Tanzania tumebarikiwa kuwa na Hospitali za rufaa za mikoa lakini pia tuna hospitali za rufaa za kanda kama vile HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KCMC, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO pamoja na hospitali kubwa ya taifa MUHIMBILI. Hospitali hizi za rufaa za kanda zina Vyuo ambavyo hutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya kama vile madaktari, manesi na wafamasia. Vyuo hivyo ni MUHAS,BUGANDO, MCHAS, na KCMCo pamoja na vyuo vingine vinavyopatikana katika hospitali za mikoa na Hospitali zingine za Binafsi na mashirika ya dini.

Wanafunzi hawa wa udaktari walioko wafunzoni wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa vitendo katika hospitali zetu jambo ambalo ni Zuri kwani linawajenga na kuwaimarisha vyema katika Sekta hiyo muhimu ya afya. Lakini pia wamekuwa wakirahisisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza wahudumu wa afya katika hospitali zetu ukizingatia kwamba vituo vingi vya afya pamoja na hospitali zetu Bado zina changamoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa Afya. Kwa ujumla wanataalamu hawa walioko mafunzoni hususani madaktari wanafanya kazi kubwa.

TATIZO LINAANZIA HAPA.
Kwa Bahati mbaya, hospitali zetu zimewaamini Wanafunzi hawa walioko vyuoni kupitiliza kiasi cha Kuwapangia Zamu za kuwaona wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu na kufanya matibabu kwa mgonjwa hata kwa wagonjwa ambao wako katika hali mbaya. Jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya ya mgonjwa. Hii imesababisha kutokea kwa vifo vingi kutokana na kwamba wanafunzi hawa wa afya hawajawa bado na Utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za afya kwa kiwango kinachostahili ukilinganisha na madaktari wazoefu.

CHANZO CHA TATIZO.
Ni kweli kwamba siku hizi Teknolojia imerahisisha ufanyaji wa kazi katika hospitali zetu.Teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya na Hospitali, na ndio maana utakuta Daktari anayeingia katika zamu ya usiku anaweza kumfahamu vizuri mgonjwa aliyelazwa wodini, matibabu aliyoyapata na matibabu anayotakiwa kuyapata hivyo kumrahisishia kuendeleza matibabu kwa mgonjwa. Lakini ukuaji huu wa Teknolojia usiwe Sababu ya kuwaachia majukumu yote wanafunzi wa udaktari walioko Vyuoni kwani waliowengi bado hawajapata maarifa ya kutosha katika kutoa huduma za kitabibu. Lakini pia wingi wa hawa wanafunzi katika hospitali zetu kisiwe kigezo cha madaktari wazoefu na wenye majukumu ya kutoa huduma za afya kusahau wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa. Wengi wa hawa wanafunzi wa udaktari wamekuwa wakitoa huduma kwa hisia ili tu kukamilisha matakwa ya kozi wanazosomea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo. na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

ATHARI ZITOKANAZO NA TATIZO HILI.
Utakubaliana nami kuwa Siku zote Mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, hata kama ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne au wa tano. Na sifa mojawapo aliyonayo mwanafunzi ni kutokujiamini kwa asilimia mia moja, hivyo kupelekea kufanya jambo kwa Jazba na Mihemko ilimradi tu kukamilisha takwa fulani. Hivyo nilazima uongozi wa hospitali zetu uwachukulie wataalamu hawa wa afya kama wanafunzi na kuwasimamia katika huduma zote za kitabibu katika hospitali zetu kwa manufaa mapana ya mgonjwa na mtoa huduma.

Kutokana na kuwatumia madaktari mafunzoni katika hospitali zetu hizi za rufaa, Huduma katika hospitali hizi zimekuwa zikishuka kadiri siku zinavyokwenda licha ya serikali Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizi, ikiwa ni pamoja na Ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma za afya, Uongezaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya. Jambo hili si zuri kwasababu linapunguza imani kwa wananchi hivyo kutumia gharama kubwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi.

Usalama wa mgonjwa awapo hospitalini ni muhimu sana. Muda mwingi mgonjwa hubaki na wataalamu wa afya kwa ajili ya matibabu. Hivyo ndugu jamaa na marafiki huamini kuwa Daktari au mtaalamu yeyote wa afya ana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya Mgonjwa. Wote tunaamini kwamba mtaalamu yeyote wa afya anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha katika kumhudumia mgonjwa ili kuokoa maisha yake. Iwapo mtaalamu huyo wa afya atakosa ujuzi na maarifa ya kutosha maisha ya mgonjwa yatakuwa hatarini, na hata kuwa ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Lakini pia kukosekana kwa maarifa ya kutosha kutamfanya mtaalamu huyo kushindwa kujiamini katika kazi yake.

HITIMISHO
Madaktari walioko mafunzo pamoja na wataalamu wengine wa afya wanafanya kazi kubwa na nzuri katika kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali zetu, Lakini Uongozi wa hospitali zetu kwa kushirikiana na vyuo vinavyotoa wataalamu hawa wa afya hauna budi Kuwasimamia ipasavyo wakati wote wanapotoa huduma kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwapanga pamoja na Madaktari wazoefu ili kuifanya huduma yao ya matibabu iwe salama na yenye kuleta matumaini kwa mgonjwa na Kuepukana na Vifo vinavyotokana na UZEMBE wa watoa huduma za afya.

Wenu
Mwita Ngutunyi Mohono
S.l.p 237 Mbarali- MBEYA
0762185894
mwitangutunyimohono@gmail.com
 
Upvote 49

Ndugu wana jukwaa.. KARIBUNI kupitia andiko hili, kulijadili lakini pia KULIPIGIA KURA.. KATIKA SEHEMU ILIYO ANDIKWA VOTE.

TAFADHARI USIACHE KULIPIGIA KURA ANDIKO HILI.
 
Tuendelee kupitia andiko hili wanajukwaa
Mkuu, nimepitia andiko lako lote na nimekuja na vitu vifuatavyo;
1. Ni andiko zuri, liknakombusha wajibu wa madaktari na wahudumu wa afya katika kujali na kutibu wagonjwa mbalimbali kwa ufanisi. Hapo madaktari wanachakiijufunza kwa baadhi ya points ulizozitoa

2. Pamoja na hayo yote, uzi wako una udhaifu mmoja tu ambao, nadhani bado unashindwa kuelewa, nao ni huu; HAKUNA MWANAFUNZI ANAEACHIWA MGONJWA PASIPO SUPERVISION"

Mwanafunzi wa udaktari ni nani?
Kuna Wa mwaka wa kwanza ( Huyu hausiki kabisa wodini, au mambo ya wagonjwa, hutumia mwaka mzima kujifunza basic sciences za mwili wa binadamu na magonjwa mbalimbali)

Kuna wa mwaka wa pili ( Huyu yupo tu kama wa mwaka wa kwanza, yeye pia anasoma basic sciences hususani magonjwa ya binadamu na tiba zake).

Kuna mwanafunzi wa mwaka wa tatu, nne na tano!
Sasa huyu ndiye anayeruhusiwa kuingia wodini, huko atajifunza practically management za mgonjwa kwa lengo la kujifunza under supervision ya seniors wa medica fields. Nakuomba sana kaka yangu unielewe hapa, medical student, hawezi kuachiwa mgonjwa hata kidogo. Hawezi kumuandikia dawa mgonjwa wako, hawezi hata kuja kuongea na ndugu wa mgonjwa kuhusu hali ya mgonjwa wao.

Ukimaliza mwaka wa tano, unaendelea na internship ( Intern Doctor ), Intern Doctor amepewa majukumu ya kufanya prescription na kumuhudumia mgonjwa tofauti na Mwanafunzi wa udaktari! Lakini sasa na yeye anakuwa under supervision ya seniors Doctor.

3. Senior Doctors ni nani?
Kwa ngazi ya referral hospital, senior Doctors ni hawa
Medical Officer (MD) huyu ni daktari mzoefu ambaye anakua ameshafanya kazi kwa kipindi kirefu kidogo, hivyo ana experience ya kumguide huyo intern Doctor na kuwafundisha Medical students.
Specialist ( MD, MMED) huyu ni Daktari ambaye alipomaliza mafunzo ya internship na kupata experience za kupractice udaktari akaamua kusoma tena miaka 3-4 na kuwa bingwa kwenye sehemu fulani, mfano utakua umesikia Daktari Bingwa wa macho, Mifupa na Magonjwa ya ndani.

Mwisho kuna Superspecialist ( MD, MMED, MSC) huyu ndie Daktari aliyefika mwisho kabisa kwenye ngazi za mafunzo, yeye anakuwa bingwa kwenye eneo dogo zaidi, mfano Kwenye macho, yeye anadeal na Retina tu ( Sehemu mojawapo ya jicho) . Mara nyingi hawa ni wachache sana na wanapatikana kwa wingi pale Muhimbili.

4. Sasa Mkuu kuna steps ambazo Daktari anatoka mpaka anakuja kuwa Bingwa.
Mfano kutoka MD to MMED, na MMED to MSc.
Funny enough ni kwamba Kwenye medicine mtu akishakuzidi elimu haijalishi umri, kuna kuwa na ule umwinyi Fulani. Namaanisha hivi
-MD (Medical Officer wa kawaida) anaposoma ili kuwa Specialist ( Bingwa) huwa anakuwa regarded as mwanafunzi haijalishi uzoefu wake wa kazi kama Daktari wa kawaida. Jina maarufu huwa wanaitwa Resident Doctors.
Kazi za Residents, ni kuwahudumia wagonjwa, kuandika dawa, lakini kupita Ward round na Either Specialist au Superspecialist.

Vivyo hivyo Huyu Specialist akitaka kuwa Superspecialist lazima aje tena na yeye kusoma kwa miaka 2-3, na atakuwa chini ya Superspecialist na atakuwa treated kama mwanafunzi tena kwa sababu ya umwinyi uliopo kwenye Medical field.

5. Nataka nikueleze kuhusu Medical ward rounds.
Hapa utashuhudia jopo kubwa la madaktari kuanzia ( Medical students (MD3, MD4, na MD5), Intern Doctor, Medical Officer, Residents, Specialist, na mwisho Super Specialist), hawa wote huwa wanamzunguka mgonjwa kwa malengo makuu mawili, moja ni kufundisha hawa junior Doctors, na la pili ni kutoa huduma za kitabibu kwa mgonjwa.
Kwenye sehemu ya mafunzo sasa, wanafunzi ( MD3, MD4 NA MD5) huwa wanaambiwa wawe na taarifa za mgonjwa kabla ya ward round kwa kuongea mgonjwa na kujaribu kutumia mafunzo waliyopewa kung'amua ugonjwa wao na matibabu yake, hii huitwa clerkships. Hapa mwanafunzi atatoa taarifa za mgojwa, na kwamba yeye anadhani angemtibu vipi kulingana na ungonjwa wake na factor nyingine. Hapo akimaliza yule senior mkuu, Super Specialist au in his/her absence Specialist humpa critiques yaani positives na negatives zake. Kisha humgeukia Resident kumuuliza kwamba wao wanamtibuje kama hospital staff. Hapo huyo senior anaweza kuongeza Dawa, kubadlisha na kusugguest Kitu chochote huku akitoa mafunzo kwa hao junior Doctors.

6 . Kaka yangu hopefully hapo juu umegrab concept nivyojaribu kuainisha, Mwanafunzi wa udaktari kamwe hawezi kumtibu mgonjwa wako, yaani hii kitu nitakupinga mpaka nakufa, tena ulivyosema tu kwama walimpatia dawa huyu mgojwa jirani, ndio nikaamini kabisa umechanganya kusema waliokuwa wamemuandikia mgonjwa huyo ni wanafunzi.

7. Mwanafunzi anaweza akafanya vishughuli vidogo vidogo kama vile , kutoa damu kwa ajili ya vipimo, kukupa dawa ambayo imeandikwa na Daktari wako, procedure kama vile catheterization ( kuweka mpira wa mkojo), kuweka mpira wa kula, na vingine, lakini kamwe hii sio kwamba anaamua tu yeye mwenyewe, ni maelekezo ya senior wake.

8. Mwisho, nimeona wengi wamejaribu kukueleza ila bado ulikua umeamini hivyo mkuu.
Na kuhusu intern Doctor yeye huwa always anakua na supervisor wake, lakini kwa sababu ya ufinyu wa madaktari na wengi wao kujihusiha na shughuli zao nyingine, unakuta intern Doctor anaachiwa majukumu makubwa, hususani wale wa shift za usiku. Lakini pale ambapo anakutana na case nzito huwa lazima senior wake atafutwe. Pili, huyu mgonjwa kumbuka lazima atapresentiwa kesho kwenye Ward round kwenye jopo la madaktari, ndipo sometimes huwa kuna mabadiliko ya madawa kulingana na review ya Specialists, hapo hakuna hata medical student amehusika hata kidogo.

9. That's how medical field work kaka, hususani kwenye big referral hospitals zenye university.
 
Ahsante kwa kupitia andiko hili mwanajukwaa. Asante pia kwa maelezo hayo ambayo binafsi nimeyapokea.

Lakini naomba nikuambie kuwa nipo pamoja na watoa huduma za afya na nathamini kazi yao kubwa wanayofanya.

Tatu, Naomba uelewe kiini cha andiko langu ambalo huwenda hujaelewa na ndio maana ya kunipa ufafanuzi.

Title inasomeka" HOSPITALI ZA RUFAA KUWAACHIA MAJUKUMU YOTE YA KITABIBU WANAFUNZI WA UDAKTARI- CHANZO CHA VIFO VINGI.

Lengo kuu la uzi huu ni kuonesha kuwa pamoja na kazi kubwa wanayofanya wataalam wa afya. Bado iko shida katika hospitali zetu hizi, wanafunzi kuaminiwa kiasi cha kupitiliza. Najua wewe kama mhusika katika kada hii ya afya unaweza USIKUBALI kwasababu inakulenga moja kwa moja. Lakini mambo haya yapo na wananchi wanalalamika.

Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha Fedha katika miradi ya afya hivyo ni SHARTI huduma inayotolewa na hospitali zetu hizi iendane na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali yetu, chini ya Rais wetu mama SAMIA.

Mtu anauguza wodini, Anaandikiwa dawa na daktari Huyu mwingine akija jioni anazikataa, mwingine akija naye anakuja na YAKE. hii inaongeza gharama zisizo na SABABU.

tusifanye hospitali zetu zikawa biashara badala ya kutoa huduma. Hizi hospitali zinatumiwa na wananchi wa kipato cha chini. Hivyo uzembe wowote ni sharti ukomeshwe.
 
Asante kwa majibu mazuri kiongozi.
Uzi huu umebeba uhalisia wa huduma katika hospitali zetu hizi kubwa. BIG UP kwa mwandishi.
 
Nakuelewa fika mwana jukwaa mwenzangu. Nimefanya utafiti na ndio maana nimeamua kuandika andiko hili. Jambo kubwa ambalo unatakiwa kulifahamu ni kwamba SI PINGI hata kidogo utaratibu wa madaktari mafunzoni kutoa huduma za afya kwasababu ni njia mojawapo ya wao kusoma kwa vitendo ni kama kwa walimu, wahandisi na nk. na ndio maana katika andiko langu nimepongeza kazi kubwa wanayoifanya ya kurahisisha utoaji wa huduma za afya. Lakini pia nimesisitiza kuwa wao ni muhimu sana kwasababu wanaongeza watumishi wa afya katika hospitali zetu.

Lengo kuu la andiko langu nikuonyesha kwamba pamoja na wanafunzi hao wa udaktari kufanya kazi kubwa na ya maana. Mamlaka za hospitali zetu hizi za rufaa zisiwaachie majukumu Asilimia zote katika kuwahudumia wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu. Kwasababu watu wengi wanalalamikia Huduma duni katika hospitali zetu hizi licha ya serikali yetu kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa.

Jaribu nawe kufanya utafiti katika hizo hospitali kubwa zenye vyuo utakubaliana nami kuwa wengi wa wanafunzi hawa ndio wanatoa huduma za afya mawodini.
Umefanya utafiti katika hospitali ngapi
 
Umefanya utafiti katika hospitali ngapi
Nadhani kama ukisoma vizuri andiko utagundua mwanajukwaa. Naomba upate muda tena w kulisoma.

Huwenda nawe pia uliwahi kusikia au uliwahi kuexperience.
 
Ni n
Wanafunzi wa chuo au Interns?..kama ni mwanafunzi wa chuo hilo ulilolisema haliwezekani.

Intern huwezi kumwita ni mwanafunzi..maana baada ya mwaka huo anakuwa yupo tayari kupractice..sasa unamwitaje mwanafunzi??

Nakubali inatakawa wafanye kazi kwa uangalizi lakini ulivyoandika ni kana kwamba wao ndo wanawaona wagonjwa toka mwanzo..kitu ambacho sio kweli kwenye hizi refferal hospital..

Interns wanaachiwa tu treatment plan baada ya ward rounds ambazo wapo pia na specialists na wanasimamia utekelezaji wake..kitu ambacho sio kigumu kufanya.
Ni ngumu hawezi kukuelewa....

Hata usiumize kichwa

Mambo ya afya ni magumu sana kwa mtu wa kawaida kuelewa system zake zlivyokaa
 
Nadhani kama ukisoma vizuri andiko utagundua mwanajukwaa. Naomba upate muda tena w kulisoma.

Huwenda nawe pia uliwahi kusikia au uliwahi kuexperience.
Naomba tutambue kuwa lengo kubwa la andiko hili sio kubeza huduma zinazotolewa na wataalamu wetu wa afya.

Bali ni kuonyesha palipo na udhaifu ili kufanya huduma katika Hospitali zetu hizi kubwa ziwe bora zaidi
 
Ni n

Ni ngumu hawezi kukuelewa....

Hata usiumize kichwa

Mambo ya afya ni magumu sana kwa mtu wa kawaida kuelewa system zake zlivyokaa
Siku zote ubora wa huduma hupimwa na WATEJA...ifike mahali tuwe na tabia ya kukubali madhaifu yetu ili yatufanye kuwa bora zaidi.
 
Wewe sio mteja....

Hakuna kitu kinaitwa mteja kwenye afya
Ndo maana nakwambia tena kuna mengi huyajui
Mwanajukwaa sina lengo la kuibishana nadhani ukielewa lengo la andiko hili..hutapata tabu kufafanua.
 
Back
Top Bottom