DOKEZO Hospitali za Serikali wanagoma kuwapa dawa wagonjwa wanaotumia bima za NHIF

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Salama tu mkuu hospitali yoyote inatakiwa iwe na duka la dawa kwa wagonjwa wa NHIF linalojitegemea ambalo haliingiliani na wagonjwa wanaolipia huduma kwa cash. Jambo kubwa toka tarehe 1.3.2024 kuna mabadiliko ya bei ya dawa kwa wagonjwa wa NHIF mfano Amoxclav adult dose kwa muda wa siku 7 hapo awali walilipa tsh 17500/= lakini sasa hivi ni tsh 6258/= vilevile dawa nyingi zimetolewa kwa wagonjwa wa NHIF so ukiziandika ujue umekula hasara. Serikali inabidi iwajibike kwa hili suala .

 
Hata Aghan wana hii tabia wanatakiwa wanyang'we leseni.
 
Waziri Ummy Mwalimu anatolewa chambo/kafara kwenye hili. Maamuzi ya Ummy siyo yake binafsi bali haya mambo yalishajadiliwa kwenye ngazi ya Baraza la mawaziri ambalo raisi ni mwenyekiti.
Unataka kutuaminisha hz sarakasi kati ya Bima na hospital Raisi hazijui wala hajazisikia?
 
Hapo wametukataa kwa mlango wa nyuma.
Kiukweli hata Mimi binafsi naona 50400 kwa mwaka ni ndogo sana. Ila ilibidi kama wanaona hailipi waongeze kiasi cha mchango ila siyo kusitisha huduma na kuleta ujanja ujanja wa kupitia mashuleni
 
Huyu ummy mwalimu sijui kilitumika kigezo Gani Hadi kupewa uwaziri nyeti kama huu.
Ni mmama mweupe Sana kichwani .
Ni mjanja mjanjasana.
Mwingine ni mhagama.

KWAMBA HII NCHI HAMNA WATU SMART HADI TULETEWE AKINA UMMY KWELI!!
 
Hapo wametukataa kwa mlango wa nyuma.
Kiukweli hata Mimi binafsi naona 50400 kwa mwaka ni ndogo sana. Ila ilibidi kama wanaona hailipi waongeze kiasi cha mchango ila siyo kusitisha huduma na kuleta ujanja ujanja wa kupitia mashuleni
Kabisa mkuu,,nimefatilia sana wanasema option ya kwanza ni kufunguwa NHIF kupitia mashuleni,,
Lakini Shule 99% hawana bima yeyote..
Na lazima wanafunzi waliosajiliwa NHIF shuleni hapo wafike idadi kuanzia 100 ndy shule inaweza ikawa na sifa za kufungua bima ya NHIF,.,ni jambo ambalo haliwezekani.

Badala yake mmeweka kifurushi cha NHIF family ambayo ni sh 314,000 kwa mwaka..
Hivi kweli Watanzania wa hali ya chini wataweza kwl?

Atleast wangeweka hata sh 100,000 au sh 150,000 kwa mtoto lakini sio kuweka kima kikubwa kiasi hicho..314000 tz sh seriously?

Mbaya Zaidi hata ukiweza kulipia hicho kifurishi cha 314000 lakini bado unapaswa kununuwa baadhi ya dawa kwa cash na sio kutumia bima..

Africa kwann hatuna utu wala ubinaadamu?
Ikumbukwe kuwa watoto wadogo ni malaika wa MUNGU,,na ndy wahanga wakubwa sn wa magonjwa ya mara kwa mara...
Serikali mna malengo gani na watoto wetu sisi masikini?

Inasikitisha sn kwa kwl., serikali kugeuza kitengo cha bima ya afya kama chanzo cha mapato.
 
Nasikia bima za Afya zipo nyingi ,ni uhuru wako wa kuchagua ,achana na NHIF nenda strategy
 
Muwe mnapitia habari mbalimbali mitandaoni mbona muongozo ulitoka wa dawa ambazo hamtopata kwa Bima ila Cash.
 
Nasikia bima za Afya zipo nyingi ,ni uhuru wako wa kuchagua ,achana na NHIF nenda strategy
Hii sijaijuwa bado,,ila uzuri wa NHIF ina hospital nyingi sn na ni ya serikali tofauti na hzo za binafsi.
 
Wewe ulitoka kuandamana au unamlaumu nani?
 
Unataka kusema mh rais ndio mwenye
shida?

Holy crap
 
Yani daktari aandike dawa mfano paracetamol kwenye fomu ya bima!,halfu ukiipeleka pale pharmacy Wanakuambia dawa hamna,ila ambaye ameandikiwa dawa hiyo hiyo lakini kama amelipia cash dawa anaambiwa ipo?
Unaishi wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…