Hospitali zaanza kutafuta wagonjwa mitandaoni, Wasanii wahusishwa!

Kutangaza ni sawa ila ikija kuwa hospitali bogus baadae wasijifiche maana tumeona hospitali nyingi majengo mapya ila waganga hakuna wengine hata kusoma vipimo shida na wengine walifukuzwa serikalini kwa ulevi wameenda private

Ila kama watafanya vizuri well and good
 
Hujachunguza vizuri, Muhimbili, Bugando na Benjakin Mkapa wamekuwa wakifanya matangazo kwenye kificho cha kuboresha huduma.

Muhimbili hata jana walikuwa kwenye media kutangaza huduma ya kupandikiza Uboho, ambayo ilitangazwa sjku nyingi na Benjamin Mkapa.

Nikajiuliza kwa mtindo huu, kwanini siku moja wasitangaze matangazo ya kuboresha motuary?
 
Hii ni biashara kama zilivyo biashara zingine kama za majeneza au magari ya kusafirisha maiti.

Hivyo sioni ubaya kujitangaza maana mtu amefanya uwekezaji ili apate faida na si vinginevyo
Usilazimishe upumbavu wako kwenye mambo ya kitaalamu.
 
inasemekana mtanzania,mtu wa kwanza anayemsikia na kumsikiliza ni,msaniiii 😄

ova
 
Kwa mantiki hiyo muuza majeneza nae asitangaze biashara yake maana itamaanisha anataka watu wafe?

Hakuna tatizo katika kutangaza biashara hata ikiwa ni hospitali. Mwisho wa siku dhamira kuu ya kuanzisha biashara ni upate wateja ili uingize faida. Mteja wa hospitali ni mgonjwa hivyo ni hadhira sahihi kutangaziwa.
 
Mfanyabiashara wa majeneza kaenda kwenye nyumba ya ibada ili aombewe kwakuwa biashara yake ya kuuza majeneza haiendi vizuri
 
Huyo msanii naye kachemka Bora angejifanya anaumwa Yuko humo kapumzishwa drip zinatiririka kwenye mishipa Kisha akaweka caption kwa kuitaja hiyo hospital.
 
View attachment 3002436

Shilole ameonekana akitangaza hospitali hiyo hapo kwenye picha na kusisitiza wagonjwa waende na kwamba ni hospitali Bora.

Kimaadili si sawa, ni kama hospitai hiyo inataka kupata watu waumwe ili wakatibiwe huko na ni muhimu sana kujua kwamba ni kama ndvyo basi bwana mochwari naye aombee ajali na vifo ili apate wateja.

Ummy Mwalimu, Jafari Liana na wahusika wengine tunaomba mshughulikie na mtupe watanzania msimamo kuhusu kutangaza hospitali kwenye media.
Katika nchi nyingi, hospitali na vituo vya afya vinaweza kukutana na vikwazo au marufuku kuhusu kujitangaza kwa sababu mbalimbali. Sababu hizi zinaweza kujumuisha zifuatazo:-

Maadili ya Matibabu: Katika tamaduni za Tanganyika na mifumo ya afya, matangazo ya hospitali yanaweza kuonekana kama yasiyo na maadili kwa sababu huduma za afya zinachukuliwa kuwa za kipekee na zinapaswa kulenga zaidi huduma bora kwa wagonjwa kuliko faida za kibiashara.

  1. Kuzuia Upotoshaji: Hospitali hupigwa marufuku kujitangaza ili kuepuka madai ya upotoshaji au matangazo yanayoweza kuwa na habari za kupotosha kuhusu uwezo wao wa matibabu au matokeo yanayotarajiwa. Hii ni muhimu kwa sababu afya ya wagonjwa iko hatarini, na matangazo yasiyo sahihi yanaweza kusababisha madhara makubwa.
  2. Usawa na Upatikanaji: Marufuku ya matangazo inaweza kusaidia kudumisha usawa katika upatikanaji wa huduma za afya. Hospitali kubwa zenye rasilimali nyingi zinaweza kuwa na uwezo wa kutangaza kwa wingi, na hivyo kuvutia wagonjwa wengi zaidi, huku hospitali ndogo zenye rasilimali chache zikibaki nyuma.
  3. Uangalizi wa Gharama: Matangazo yanaweza kuongeza gharama za uendeshaji wa hospitali, ambazo zinaweza kupitishwa kwa wagonjwa kupitia ada za juu za matibabu. Kuzuia matangazo kunasaidia kuhakikisha kuwa rasilimali za hospitali zinatumika moja kwa moja kwa huduma za wagonjwa badala ya matumizi ya masoko.
  4. Kanuni za Serikali na Sera za Afya: Serikali na vyombo vya udhibiti vya afya vinaweza kuweka sheria zinazodhibiti matangazo ya hospitali kama sehemu ya sera za afya za umma. Lengo ni kuhakikisha kuwa huduma za afya zinatolewa kwa usawa na kuzuia ushindani usiofaa kati ya watoa huduma za afya.
MWISHO:Watanganyika wenzangu, kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.Kwa wanawake wa DAr waliopitia uzazi ambao kidogo mifuko yao ni mirefu wanamjua dokta fulani gynocologist mzuri sana, ana asili ya kule nanii, hakuna asiye mjua, hana tangazo popote ila anatafutwa usiku na mchana, sababu kuu ni uwezo wake wa kazi.
Tukiruhusu wajitangaze ni mvurugano.

Da' Ummy Mwalimu, wewe ni Waziri mchapa Kazi , naomba uchukue hatua kali, lakini pia matangazo ya waganga wa kienyeji kwenye media wakijinasibu kutibu magonjwa fulani na kuwakataza wagonjwa wasiende hospitali.
We akili yako ndogo sana, ni sawa sawa kusema, wa Japan walaumiwe kutengeneza magari yenye speed 200km/hr, kwa vile ni speed kubwa, na, speed kubwa zinaua watu Afrika!,
Kwanza hatuendi hospitsri kutibiwa tu, tunaenda pia kwa ajili ya check up, kuna hospitsri hazina vifaa vya kisasa, tunaenda kufata huduma,
Kama upo dar nenda Aghakan hospital , harafu ulinganishe na uchafu wa mloganzila au Muhimbili,
 
Hiyo biashara hairuhusiwi kutangazwa. Nashauri rungu hilo lihamie na kwa watu wa tiba asili, wamekuwa matapeli sana.
 
Zama zimebadilika hata Fundi majeneza wanajitangaza sasa hivi!
 
We akili yako ndogo sana, ni sawa sawa kusema, wa Japan walaumiwe kutengeneza magari yenye speed 200km/hr, kwa vile ni speed kubwa, na, speed kubwa zinaua watu Afrika!,
Kwanza hatuendi hospitsri kutibiwa tu, tunaenda pia kwa ajili ya check up, kuna hospitsri hazina vifaa vya kisasa, tunaenda kufata huduma,
Kama upo dar nenda Aghakan hospital , harafu ulinganishe na uchafu wa mloganzila au Muhimbili,
Kwahiyo , Bi. Ummy anakosea kuzuia matangazo ya Hospitali?
Huenda hiyounayosema ni bora ndio inaongoza kwa uzembe wa madaktari.
 
Haya mahospitali ni mabalaa na mikosi tu, yanafaa yakose wagonjwa, ugonjwa ni hali mbaya kiafya kwa mtu ni karibu na kifo. Sasa nani anataka kufa?
 
Back
Top Bottom