Hospitali zaanza kutafuta wagonjwa mitandaoni, Wasanii wahusishwa!

Kutangaza ni sawa ila ikija kuwa hospitali bogus baadae wasijifiche maana tumeona hospitali nyingi majengo mapya ila waganga hakuna wengine hata kusoma vipimo shida na wengine walifukuzwa serikalini kwa ulevi wameenda private

Ila kama watafanya vizuri well and good
 
Hujachunguza vizuri, Muhimbili, Bugando na Benjakin Mkapa wamekuwa wakifanya matangazo kwenye kificho cha kuboresha huduma.

Muhimbili hata jana walikuwa kwenye media kutangaza huduma ya kupandikiza Uboho, ambayo ilitangazwa sjku nyingi na Benjamin Mkapa.

Nikajiuliza kwa mtindo huu, kwanini siku moja wasitangaze matangazo ya kuboresha motuary?
 
Hii ni biashara kama zilivyo biashara zingine kama za majeneza au magari ya kusafirisha maiti.

Hivyo sioni ubaya kujitangaza maana mtu amefanya uwekezaji ili apate faida na si vinginevyo
Usilazimishe upumbavu wako kwenye mambo ya kitaalamu.
 
inasemekana mtanzania,mtu wa kwanza anayemsikia na kumsikiliza ni,msaniiii 😄

ova
 
Kwa mantiki hiyo muuza majeneza nae asitangaze biashara yake maana itamaanisha anataka watu wafe?

Hakuna tatizo katika kutangaza biashara hata ikiwa ni hospitali. Mwisho wa siku dhamira kuu ya kuanzisha biashara ni upate wateja ili uingize faida. Mteja wa hospitali ni mgonjwa hivyo ni hadhira sahihi kutangaziwa.
 
Mfanyabiashara wa majeneza kaenda kwenye nyumba ya ibada ili aombewe kwakuwa biashara yake ya kuuza majeneza haiendi vizuri
 
Huyo msanii naye kachemka Bora angejifanya anaumwa Yuko humo kapumzishwa drip zinatiririka kwenye mishipa Kisha akaweka caption kwa kuitaja hiyo hospital.
 
We akili yako ndogo sana, ni sawa sawa kusema, wa Japan walaumiwe kutengeneza magari yenye speed 200km/hr, kwa vile ni speed kubwa, na, speed kubwa zinaua watu Afrika!,
Kwanza hatuendi hospitsri kutibiwa tu, tunaenda pia kwa ajili ya check up, kuna hospitsri hazina vifaa vya kisasa, tunaenda kufata huduma,
Kama upo dar nenda Aghakan hospital , harafu ulinganishe na uchafu wa mloganzila au Muhimbili,
 
Hiyo biashara hairuhusiwi kutangazwa. Nashauri rungu hilo lihamie na kwa watu wa tiba asili, wamekuwa matapeli sana.
 
Zama zimebadilika hata Fundi majeneza wanajitangaza sasa hivi!
 
Kwahiyo , Bi. Ummy anakosea kuzuia matangazo ya Hospitali?
Huenda hiyounayosema ni bora ndio inaongoza kwa uzembe wa madaktari.
 
Haya mahospitali ni mabalaa na mikosi tu, yanafaa yakose wagonjwa, ugonjwa ni hali mbaya kiafya kwa mtu ni karibu na kifo. Sasa nani anataka kufa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…