Hospitali zote zaagizwa zihudumie wagonjwa ndani ya masaa matatu, je hospitali zetu zimejengewa uwezo huu?

Tulishauri Wizara ya afya iongozwe na wataalamu wa afya
Kadhalika elimu, ujenzi, kilimo nk
Wizara zikiongozwa na wataalamu wa maeneo hayo ni rahisi kushughulikia matatizo kwakuwa wamefanya kazi hizo wanajua changamoto zake
 
Masaa matatu si rahisi.

Unakuta Dr. Mmoja anaona wagonjwa hata 30 wa clinic kwa siku moja.
Kila mgonjwa akitumia dakika 10 kwa Daktari.
Kama wewe ulikuwa ni mgonjwa wa mwisho.
Hapo lazima utasubiri dakika 290 ili dr akuone
Hii ni sawa na karibia masaa matano.

Hapo sijaweka dakika za kwenye vipimo (maabara, utrasonography, x-rays ).
+ Pharmacy.

TUongeze wataalamu na vifaa vya kisasa.
 
30 mbona wachache?
 
Hii ni drama kama drama zingine.

Huyu atafeli asubuhi tena afadhali hata aliyetolewa..

Eti mgonjwa ahudumiwe ndani ya masaa matatu! Hivi amejiuliza hizo hospitali zina watumishi wa kutosha kama miongozo ya afta inavyotaka,? Zina vitendeaxkazi vya kutosha? Mifumo ya tehama tu iko duni kuhakiki kadi pekee mgonjwa anatumic zaidi ya saa moja. Hivi anajua kuwa maspecialist kwanza wanaanzia round wodini kuwaangalia wagonjwa wao waliolazwa hadi wamalize round tu na kuanza kuhudumia wagonjwa wa nje inachukua zaidi ya masaa matatu hapo bado mgonjwa hajafanya vipimo, hajaenda dirisha la dawa, hajachukua majibu ya vipimo.

Watu watasema afadhali aliyetoka kama hii ndio approach yake.
 
Masaa matatu ni mengi sana kusubiria kumuona daktari tu, inatakiwa ndani ya nusu.
hii hapana kaka, kuna emergency case, urgent case, na kadhalika. lazima wagonjwa wafanyie triage kisha ndio tutajua yupi anahitaji huduma mwanzo zaidi kwa kadri ya case yake.
 
Anaewaamini wanasiasa akapimwe ubongo hasa ccm
 
Bado tutajitibu kienyeji....hizo saa tatu bado ni kizungumkuti...!
 
Uwezo wanao, tena naamini wanaweza hata chini ya hapo, bila kuanza hivyo matatizo hayatojulikana. Jenista kawapa mwanzo mzuri.

hapa nipo na Jenista. Nnamuunga mkono 100% kwa hilo.

Iliyobaki hospitali zishindane kushusha muda huo badala ya kuzubaa.

Nashauri, mkurugenzi wa hospitali iyoyaweza hayo, afinywe tu kimyakimya, muuwaji huyo.
 
[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wapambane tu
 
Hili ndiyo tatizo la kumpa uwaziri F6 failure asiyekuwa na chembe ya taaluma ya afya.

Hata hajui kuwa kuna mgonjwa anaweza kusubirishwa kwasabb kinyesi/mkojo wake unatakiwa, au sampuli zake zinatakiwa kufanyiwa culturing.
Wavivu na magoi goi hamkosi sababu, ndio maana hapo unajifanya hujaelewa concern ya waziri unaokoteza okoteza tu vihoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…