Hosteli za Magufuli kutumika kama karantini za kuweka wageni kutoka nchi zilizoathiriwa na Corona

Hosteli za Magufuli kutumika kama karantini za kuweka wageni kutoka nchi zilizoathiriwa na Corona

We ulitaka hiyo program iendeshewe wapi? Kwenye hotel mnalia ghalama sasa serikali ifanye nini? Kuhusu wanafunzi ondoa shaka kwani kabla hazijajengwa hizo walikuwa wanalala wapi? Pale kuna majengo mengi hawatakosa sehemu ya malazi
 
Kila jitihada inabd ifanyike ili kuhakikisha raia wanakuwa salama, suala la hosteli kugeuzwa matumizi halijaanza leo kuna memgine tunageuza kuwa madarasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujumbe huu umfikie nanihii
IMG-20200405-WA0030.jpg
 
Hii ndio Bongo bana,

Serikali inafunga shule na vyuo kama tahadhari dhidi ya Corona nakuacha mipaka wazi, kupokea wageni kutoka nchi zilizoathirika na kuwaweka kwenye hostel za vyuo walivyofunga kama tahadhari.

Yaani hii ni kama kuacha milango na madirisha wazi huku ukiwaficha watoto uvunguni wasiumwe na mbu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli amehamia Dodoma kwa nini lile jengo la Ikulu ya zamani lisitumike kama kituo cha kushikilia wagonjwa wa korona kwa muda? Hizo hostel ni hatari kwa sababu wanafunzi watarudi kuishi humo
Ikulu anakaa Rais na familia yake pamoja na wafanyakazi wachache tu. Sasa sehemu hiyo itawezaje kuhifadhi watu wengi? Mbali na hayo, Ikulu itabakia kuwa ikulu, sawa na sasa kulikuwa na Ikulu ndogo mikoani wakati Rais akiwa anaishi Magogoni. Tusifanye mzaha kusema Rais asipokuwepo basi nyumba anayokaa tuipangishe kwa mgeni mwingine. Hostel ziko kwa ajili ya watu wengi na ni sawasawa tu na vyumba vya hoteli au gesti. Mmoja akiondoka haichukui muda kukiandaa chumba kwa mgeni mwingine. kwa hiyo ni sawa kabisa kuzitumia hostel kwa karantini wakati vyuo vimefungwa na wanafunzi hawapaswi kuwa humo.
 
Kwani wagonjwa wa korona wako wengi mkuu? Majengo yote yale ya magogo yanshindwe kuhifadhi watu 1000?
 
Inasikitisha
Hii ndio Bongo bana,

Serikali inafunga shule na vyuo kama tahadhari dhidi ya Corona nakuacha mipaka wazi, kupokea wageni kutoka nchi zilizoathirika na kuwaweka kwenye hostel za vyuo walivyofunga kama tahadhari.

Yaani hii ni kama kuacha milango na madirisha wazi huku ukiwaficha watoto uvunguni wasiumwe na mbu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe tangu Magufuli akutumbue akili zimekuruka,ameungua kaugonjwa kanakoitwa pinga pinga,but haisaidii, utaendelea hivyo hivyo hadi kaburini.
Tuko seriuos kiasi cha kutosha?

Yaani wenzetu wanafunga mipaka na viwanja vya ndege alafu sisi tunaendelea kuwapokea wageni!!

Kwa umasikini wetu, kujikinga kwa gharama yoyote ndio ponepone yetu maana hata mataifa makubwa yanaelemewa na huu ugonjwa ndio sembuse sisi.

Na je, huu si ushahidi kuwa vyuo bado sana kufunguliwa?

Kingine nachojiuliza, ni nini yatakuwa madhara ya kutumia hizo hostel ambazo zitakuja kutumiwa na mamia ya wanafunzi endapo kuna vimelea vitasalia baada ya karantini kwisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni Nyumbu wa Ufipa. Lazima apinge lolote linalofanywa na serikali. Ajabu, kama serikali ingesema wakae Kempiski kwa gharama zao, angepinga na kusema kwanini wasiwekwe Magufuli Hosteli kwakuwa wanafunzi hawapo. Sasa wanapelekwa huko anapinga! Labda anataka wapelekwe kwenye Makao Makuu ya Chadema Ufipa!

Una hoja za hapa na pale boss. Ila kimsingi ukiangalia hili jambo ni kama serikali haina mbinu sahihi. Jana Makonda kaongea kwa nyodo, anasema watu watoke wakafanye kazi kwani watakufa kwa njaa. Leo anasema kuanzia kesho watakamatwa wote watakaoingia mjini kama hawana kazi maalumu, je umejiuliza hao watakaokamatwa watawekwa wapi? Je kama kuna mwenye maambukizi itakuwaje?
 
Nahisi karantin inatakiwa angalau ijitenge na makazi pia ukaribu wa watu kupita, niliwaza sana hivi yale majengo yapo kule Mbagala kuu ile barabara ya kutokea Kibada yanakazi gani kwa sasa? Kwanini karantin centres zisiwe huko pametulia na mbali na makazi ya watu.Kwanini serikali isiwaze kuweka huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom