Hot story

Hot story

*****SORY MADAM*****(65)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
Nilimuuliza Dorecy na kumfanya Phidaya kunitazama kwa jicho kali lililo jaa hasira
"Ndio, ila kuna ishu Khalid alitaka kukufanyia wewe na Phidaya akaiingilia kati na kuwa adui mwengine wa Khalid"
"Jambo gani hilo?"
Hata kabla Dorecy hajanijibu tukasikia milio mingi ya risasi kwenye kordo yetu huku kelele za watu wagonjwa na manesi wakike zikisikia jambo lililo tushtua sote ndani ya chumba
ENDELEA
Milio ya risasi ikaendelea kurindima nje ya chumba tulichopo na kuzidi kutupagawisha sote tuliopo ndani ya chumb hichi, wasiwasi mwingi ukawa kwa Dorecy ambaye fika anaoenekana kuchanganyikiwa
"Eddy hao ni watu wa mume wangu"
Dorecy alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, nikapiga hatua za haraka hadi dirishani na kuchungulia chini ambapo kuna umbali wa ghorofa mbili kwenda chini.
"Hatuwezi kutoka humu ndani"
Nilizungumza huku nikiwatazama Dorery na Phidaya
"Itakuwaje sasa?"
Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika kwa wingi.Nikapiga hatua hadi mlangoni, nikachungulia kwenye sehemu ya kuingizia funguo, nikamshuhudia jamaa mmoja akitandika risasi ya kichwa mzee mmoja aliye ambiwa alale chini ila akaleta kiherehe cha kujinyanyua, ndipo akakutana na maafa hayo ambayo ni yakinyama sana.
Gafla simu ya Phidaya ikaita na kutufanya sote kumgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao, kwa kiwewe alicho nacho akashindwa hata kuikata na kujikuta akiiachia na kuanguka chini, nikachungulia tena kwenye tobo la kuingizia funguo na kumuona jamaa aliye muua mzee, akiutazama mlango wetu kwa umakini.
"Ingieni bafuni"
Nilizungumza kwa sauti ya chinichini, Dorecy akamshika mkono Phidaya na kukimbilia kwenye bafu liilopo humu ndani ya chumba changu.Jamaa akapiga hatua hadi ulipo mlango uku bunduki yake aina ya ‘short gun' ikiwa mkononi mwake.Nikajibanza nyuma ya mlango, huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwani bado sijaiamini afya yangu kwa kiasi kikubwa kutokana na majeraha ya risasi yaliyopo mwilini mwangu.Mlango taratibu ukafunguliwa, nikaanza kuona kiatu cheusi kikitangulia mbele, jamaa akasimama kwa muda, gafla simu ya Phidaya iliyo anguka chini ikaanza kuita tena na kumfanya jamaa kupiga hatua za taratibu hadi sehemu ilipo anguka simu na kuiokota.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, kwani endapo jamaa atageuka nyuma nilazima ataniona.Akaitazama simu ya Phidaya kwa muda na kuitupa chini na kuchanguka, akatazama mlango wa kuingilia bafuni ambapo ndani yake yupo Phidaya na Dorecy
Simu ya jamaa ikaita, akaitoa kwenye koti lake, akaipokea nakuiweka sikioni mwake, akazungumza kwa lugha ya kiarabu, nikastukia kumuona jamaa akichomoka kwa kasi, ndani ya chumba pasipo kuniona nyuma ya mlango, ving'ora vya gari za polisi, nikaanza kuvisikia na kunifanya nishushe pumzi nyingi, na kujikalia chini, huku jasho jingi likimwagika.Ndani ya dakika kadaa askari kadhaa wakawa wameingia katika sehemu tulipo, Dorecy na Phidaya wakatoka bafuni, askari na madaktari walio salimika katika vamizi la majambazi hawa
***
Wagonjwa tulio salimika tukahamishwa kwenye hospitali moja, inayo milikiwa na jeshi la nchi ya Philipines, matiibabu yangu hayakuchukua muda mrefu sana, nikaruhusiwa kutoka hospitalini na kuhamia kwenye hoteli ambayo Phidaya anaishi kwa siri sana, na amelipiwa gharama zote na Dorecy ambaye tayari amerudi kwa mume wake.
"Phidaya,itatubidi turudi Tanzania"
Nilizungumza huku macho yangu yakimtazama Phidaya aliye jilalia kiuvivu kwenye kitanda, huku akiwa tumbo wazi akilichezea chezea kwa kiganja chake tumbo lake lenye kiumbe ndani
"Si usubiri niweze kujifungua kwanza"
"Hatuwezi kuishi hapa, pasipo sisi kuwa na kazi, unadhani tutayamudu vipi haya maisha?"
"Sawa mume wangu, je tukirudi huko Tanzania, tutafikia wapi wakati umesha sema kwamba mama yako alitekwa na baba yako mkubwa"
Nikamtazama Phidaya kwa muda, kwani kitu alicho kizungumza kinamaana kubwa sana kwangu, isitoshe sijajua ni hali gani inayo endela kati ya mzee Godwin na mama yangu.Nikanyanyuka taratibu na kuisogelea computer iliyopo kwenye meza humu chumbani kwetu, ambayo imeunganishwa na huduma ya Internet.Nikaiwasha taratibu, baada ya muda nikafungua mtandao wa Google
"Unataka kufanya nini?" Phidaya alizungumza huku akipiga hatua na kuja kukaa kwenye kiti nilicho kikalia mimi
"Kuna mtu nataka kumtafuta"
"Nani?"
"Baba yangu mzazi, anaishi Afrika kusini"
"Mmmm sawa"
Nikaliingiza jina la baba yangu mzazi kwenye sehemu ya kutafutia, kwenye mtandao huu ambao unasadikika ndio mtandao mkubwa duniani kote, ulio kusanya mambo mengi sana, ndani ya sekunde kadhaa nikawa nimefanikiwa kulipata jina la baba yangu mzazi pamoja na historia yake, cha kumshukuru Mungu nikakutana na taarifa nyingine iliyo nipendezesha moyoni mwangu, kwani ameingia kwenye orodha ya matajiri kumi nchini Afrika kusini huku yeye akiwa nafasi ya nne kutoka juu.
"Inabidi twende nyumba ni kwa baba"
"Sawa mume wangu"
Phidaya hakuwa na pingamizi na maamuzi yangu niliyo yachukua, nikaanza kufwatilia hati za kusafiria kuelekea Afrika kusini, kutuokana na pesa ambazo Dorecy anatusaidia, sikupata tabu sana katika kukamilisha maswala usafiri wa ndege.Siku ya pili tukakusanya kila kitu kilicho chetu kwenye hoteli ambayo tunaishi, tukakodi Tanksi hadi uwanja wa ndege, muda wa kupanda ndege ulipo wadia, tukaungana na wasafiri wengine na kuingia ndani ya ndege, na taratibu safari ikaanza, huku moyoni mwangu nikimuomba Mungu atufikieshe salama, kwani kumbukumbu za ajali iliyo tokea nchini Kenya kipindi nikitokea Afrika Kusini, inaendelea kuzunguka ndani ya kichwa changu kama mkanda wa filamu.Phidaya kwa kudeka muda wote kichwa cheka amekilaza kifuani mwangu, huku akiimba nyimbo za kunibembeleza kwa sauti ya chini
"Baby" Nilimuita kwa sauti ya upole
"Mmmmm"
"Naomba niende msalani"
"Sawa, ila usichelewe mume wangu"
Phidaya alinijibu taratibu huku akijinyanyua, kifuani kwangu taratibu, nikasimama, na kuanza kupiga hatua za kuelekea chooni, nikaingia ndani ya choo na kumaliza haja zangu zote, nikanawa uso wangu ili kuutoa uchovu na usingizi unao ninyemelea usoni mwangu.Nikafungua mlango, gafla nikastulia kitu chenye ncha kali kikinikita mgongoni mwangu, na sauti ikasikika kutoka nyuma yangu
"Tulia kama ulivyo upo chini ya ulinzi, Mr Eddy"
****Je ninani aliye aliye muwekea Eddy kitu chenye ncha kali, mgongoni mwake, wakiwa ndani ya ndege.Ungana nami kwenye toleo lijalo*****
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(66)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA

ILIOISHIA
"Sawa, ila usichelewe mume wangu"
Phidaya alinijibu taratibu huku akijinyanyua, kifuani kwangu taratibu, nikasimama, na kuanza kupiga hatua za kuelekea chooni, nikaingia ndani ya choo na kumaliza haja zangu zote, nikanawa uso wangu ili kuutoa uchovu na usingizi unao ninyemelea usoni mwangu.Nikafungua mlango, gafla nikastulia kitu chenye ncha kali kikinikita mgongoni mwangu, na sauti ikasikika kutoka nyuma yangu
"Tulia kama ulivyo upo chini ya ulinzi, Mr Eddy"

ENDELEA
Mwili ukanisisimka na kujikuta nikitulia kimya, huku kwa mbali mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio, ila sauti niliyo isikia nyuma yangu haikuwa ngeni masikioni mwangu, nikatamani kugeuka na kutazama nyuma ila sikuwa na uwezo kutokana nipo chini ya ulinzi wa mtu huyu.
"Oya wewe ----- kweli, kijiko pia kinakutisha"
Mtu aliye nyuma yangu alizungumza huku akizunguka na kuja mbele yangu, macho yangu yakakutana na John, rafiki yangu wamuda mrefu tangu tukiwa shule ya sekondari, akiwa amevalia mavazi maalumu kama watumishi waliopo kwenye hii ndege, nikashusha pumzi nyingi na kubaki tukitazamana.Tabasamu likatawala usoni mwa John na mimi pia nikajikuta nikitabasamu na kukumbatiana naye huku tukipigana pigna migongoni kwani, nimiaka kadhaa imepita pasipo sisi kuonana
"Eddy mwanangu, aahaa nikitambo sanaa"
Johna alizungumza kwafuraha huku tukiachiana
"Kweli mwanangu, haya mbona huku tena kwenye ndege?"
"Ndugu wee acha tuu, maisha mwanangu yanabadilika"
"Ndipo unapofanyia kazi?"
"Nipo training(mafunzo), napata pata ujuzi"
"PCB wewe umekuwaje, umekuja kwenye ndege huku, au ndio hiyo elimu ya Tanzania, HKL anakuwa mkaguzi wa fedha, wakati Mathematics amenyoosha mswaki?"
Nilizungumza kwa utani huku nikiwa nafuraha usoni mwangu
"Ahaaa kaka, ndio maana yake, huku tumeingia hivyohivyo tuu, tena kwa masaada wa mama yako ndipo aliniunganisha huku"
Taarifa ya John ikanistua kidogo nakujikuta nikaanza kumfkiria mama yangu
"Mama yangu yupi?"
"Haaa kwani Eddy wewe una mama gani mwengine?"
"Hapana nimekuuliza hivyo kutokana nina maana yangu?"
"Mama yako ambaye kwa sasa ni waziri wa usafirishaji, ametoka kwenye kitengo cha Afya"
"Unataka kuniambia kwamba mama yangu yupo hai?"
"Ndio yupo hai, tena yeye anakutafuta wewe"
"John umeniacha njia panda hemb…….."
Sikuimalizia sentesi yangu, msichana mmoja aliye valia mavazi kama John, alimuita John kwakutumia lugha ya kingereza
"Am coming"(Ninakuja)
John alimjibu msichana aliye muita huku akimtazama usoni mwake
"Sasa Eddy, ngoja mimi nikaendelee na majukumu ndugu yangu"
"Sawa ila kaka nahitaji tuzugumze zaidi"
"Usijali kwani wewe unaelekea wapi?"
"Afrika kusini, kwa mzee"
"Mzee gani tena, kwa maana baba yako amefungwa?"
"Eheee"
"Kwani Eddy ulikuwa wapi siku zote"
"John"
Sauti ya msichana aliye muita John mara ya kwanza ilisikika tena, ikimuita kwa msisitizo
"Kaka baadaye"
John aliondoka kwa kupiga hatua za haraka kwenda katika sehemu alipo itwa, nikashusha pumzi kwa mara nyingine, huku kichwa changu kikiingia mawazo mapya katika maisha, kwani kwakipindi hichi, nilichokaa mbali na nchi yangu sikujua ni mambo yapi yaliyo endelea kwenye nchi yangu, na pia sikujua ni kitu gani lilichotokea kati ya mama yangu na mzee Godwin, baba yangu mkubwa ambaye kwa mara ya kwanzi nilidhani kwamba ni baba yangu mzazi.Nikarudi kwenye siti yangu, huku nikiwa nafuraha usoni mwangu
"Mbona umechelewa kurudi ulikuwa na nani?"
Phidaya aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, nikajikuta nikitabasamu kwa furaha na kumtazaka usoni mwake
"Mke wangu, ninafuraha wee acha tuu"
"Furaha gani tene hiyo?"
"Kwanza nimekutana na rafiki yangu wa kipindi kirefu sana"
"Nani?"
"Nitakuambia tukitulia"
"Ahaaa eheee, sawa bwana"
Phidaya alizungumza kwasauti yakudeka huku akigeukia uapande wapili wa siti yake, nikaupitisha mkono wangu mmoja kwenye kiuno chake na kumvuta karibu yangu na kichwa chake akakilaza kifuani kwangu taratibu
"Umekasirika?"
"Ndio"
"Nisamehe mke wangu"
"Sikusamehe, hadi uniambie umekutana na nani?"
Nikamuadisia Phdiaya, historia fupi kati yangu na John, nikamuelezea kuhusiana na maisha ya mama yangu japo hakunieleza kwa undani, sana kuhusiana na maisha yaliyo jitokeza kwenye familia yangu ila moyoni mwangu kidogo nikipata matumaini yakumuona mama yangu, hadi namaliza kumuadisia Phidaya, mwenzangu tayari usingizi umepitia nakulala fofofo.Baada yamasaa kadhaa, sauti ya msichana ilisikika kwenye vipaza sauti vilivyomo ndani ya ndege, akituomba tufunge mikanda kwani ndege ipo karibuni kutua katika uwanja wa ndege wa ‘Johannesburg'.Ndani ya dakika kadhaa ndege ikatua kwenye uwanja na abiria wakaanza kushuka mmoja baada ya mwengine, John akafika hadi kwenye siti yetu, ambapo ametukuta tunatoa toa mabegi yetu katika sehemu ambayo tumeyaweka
"Huyu ndio, John ambaye nilikuwa nikikuambia"
Nilimtambulisha John kwa Phidaya
"John huyu ni mke wangu, anaitwa Phidaya"
"Ahaaaa, habari yako shemeji"
Phidaya na John wakasalimiana kwa muda huku wote wakiwa wanafuraha, John akatuomba tumsubiri nje ya uwanja, yeye nawezake wakimalizia hatua za makabidhiano ya ndege, nawahudumu wengine ambaoa watarudi kwenye safari ya mzunguko wa ndege hiyo.Tukakaguliwa mimi pamoja na mke wangu Phidaya, tukatoka nje ya uwanja wa ndege na kutafuta sehemu yakukaa, Ndani ya dakika kumi na tano John akaja katika sehemu tuliyo kaa, kutokana ipo wazi sana kwa watu kutuona
"Jamani, sijui nyinyi wezangu munaelekea wapi?" Jonh alituuliza
"Sisi tunasafari yakuelekea kwenye Cap town"
"Munaonaje tukafikizia Hotelin leo, kisha kesho muweze kwenda kwakutumia usafiri watreni za umeme"
John alitushauri, sikuwa nakipingamizi kutokana hatukumaliza mazungumzo na John juu yakitu ambacho kimetokea kwenye maisha ya miaka michache iliyo pita, tukakidisha taksi iliyotupeleka kwenye hoteli moja iitwayo ‘Mondior Concorder' iliyopo pembezoni mwa barabara ya Albetina Sisulu, tukafanikiwa kupata vyumba viwili vyenye hadhi nzuri kwawageni kulala
"Baby mimi najisikia kuchoka, nitapumzika zangu ndani"
Phidaya alizungumza mara baada ya kuingia katika chumba tulicho chukua
"Kwanini?"
" Kuna chakwanini wakati nimekuambia kwamba nimechoka, hivi unadhani hili jitoto lako humu ndani halinichoshi?"
"Mmmm mke wangu na wewe kwakudeka, haujambo"
"Nini"
"Yaishe mama kijacho"
"Wewe niudhi tuu"
Phidaya alizungumza huku akijilaza kitandani taratibu, kwa jinsi mwili wa Phidaya ulivyo umbika, umekuwa nikivutio kizuri kwangu ambacho sichoki kikitazama kila muda na dakika zake zinavyo zidi kukatika
"Kweli hapa nimepata mke"
Nilijisememea kwasauti yachini chini, nakumfanya Phidaya kunitazama kwamacho makali, akaachia msunyo mkali na kujiweka vizuri kitandani, kutoka tayari kumeshaanza kupambazuka, sikuona haja ya mimi kuendelea kulala kitandani, kusimama kwenye dirisha la chumbani chetu lenye kioo kikubwa, na kuaanza kuuangalia mji huu jinsi ulivyo jengeka kwa majengo yaliopo kwenye mpangilio mzuri
"Huji kulala hapo umesimama kama mshumaa wapasaka, maana yake ni nini?"
Phidaya alizungumza huku akitumbulia macho yake, makubwa kiasi
"Mke wangu saa hizi, saa kumi na mbili na nusu, nitalala nini?"
Phidaya akajifunika kwashuka gubigubi, kwa jinsi ujauzito wa mke wangu ulipo fikia, unampelekesha kama mtoto mdogo kwani kila analo lifanya nikituko kwangu.Asubuhi namapema nikakutana na John kwenye mgahawa uliopo chini ya hoteli hii, akaanza kuniadisia kila kitu amcho kilitokea kwapindi kizima nilipokuwa sipo nchini Tanzania
"Mama, yupo salama kabisa na nijuzi kati tu, hapa nilikuwa naye kwenye ndege yetu inayo elekea Tanzania, alikuja huku kwa mambo yake binafsi"
"Ehee ilikuwaje?"
"Siku ambayo ilikuwa ni graduation(mahafali) yakumaliza kidato cha sita ndipo, siku ambayo nilikutana na mama wakati wausiku.Ile siku nakumbuka ilikuwa nijumamosi, wakati wausiku nilikuwa na demu mmoja sidhani kama utakuwa unamfahamu"
"Alikuwa ni mwanafunzi?"
"Ndio, anaitwa Catherina?"
"Simkumbuki"
"Nahisi alihamia kipindi wewe, umeshaondoka, kama unavyojua mwanangu maisha ya shule, tuliamua usiku kwenda sehemu yakujificha kule msituni, ambapo tulianza, kufanya yetu kwenye kichaka"
"Mmmm, hukuwa na pesa ya chumba nini?"
"Ahaaa hoteli zote zilijaa wageni, waliokuja kwenye sherehe, kipindi tunafanya yetu, kwa mbali tulianza kusikia vishindo vya watu wakitembea kwenye eneo tulilopo, ikatulazimu kukatisha mautamu yetu, nakujikuta tukijificha kwenye kichaka chetu"
"Tuliwashuhudia watu hao wakiitupa miili ya watu wawili, huku wote wakibishana nakudai kwamba watu hao tayari wameshafariki, walipo watupa, wakaondoka zao na kutuacha sisi, tukiwa tunatetemeka"
"Sasa mulikuwa munatetemeka nini?"
"Weee, Eddy wewe unazungumza tuu, kukutana na watu kama wale si kitu kidogo, mbona Catherina alijikojolea kwa woga"
"Dooooo" Nilijikuta nikicheka
"Sijui hata ujasiri niliupatia wapi, nikajikuta nikipiga hatua za kwenda kutazama sehemu walipo tupwa watu wale, japo Catherina alikuwa na wasiwasi, kufika ile sehemu, nikastukia kuona mmoja wao akistuka na kutoa ukelee, kumcheki vizuri wapili naye nikagundua kwamba yupo hai, ambaye ni mama yako, Ila miili yao ilikuwa imedhohofika sana, tena sana, ilinilazimu kwenda kumuomba, Lucas gari lao"
"Lucas nani?"
"Lucas Martin, tuye jamaa wa HKL aliyekuwa anajisikia sana"
"Ahaaa nimemkumbuka"
"Alikuwa anatembeala na gari ya baba yake, aliyokuja nayo kwenye mahafali, basi tuliwapeleka kwa bibi yangu aliyepo pale pela Arusha yeye ni nesi, ila nilifanya nisiri sana watu wasijue kutokana mazingira tuliyo wapata, yalikuwa nihatarishi sana.Bibi yangu alianza kuwafanyia matibabu hadi afya zao zikawa salama"
"Huyo mtu wapili alikuwa ni nani?"
"Ni Sheila, ambaye kwa sasa, anaishi kwa mama"
"Ahaa sasa ilikuwaje kwa mzee Godwin"
"Sasa hapo ndipo nilipopata kujua kwamba, mchongo wote wakutekwa kwa mama yako, aliyesababisha kutekwa kwake ni Mzee Godwin ambaye kwa sasa, ananyea debe gerezani"
Habari aliyo nipa John, ikajenga furaha iliyojawa nashauku yakutaka kutaka kumuona mama yangu,
"Kwenye ndege umesha ajiriwa au bado?"
"Ndio ninamalizia mafunzo,"
"Kwa nini umekuwa muuhudumu wa ndege wakati, mipango yetu ilikuwa ni kuwa madaktari bingwa?"
"Kaka, PCB mbaya mwanangu, nilizungusha"
"Ulizungusha…..!!?"
"Ndio ndugu yangu, nilipata zero, ila sijutii sana kwani muda mwingi niliutumia sana na Catherina"
"Na huyo Catherina alipata ngapi?"
"Ahaaa naye pia alizungusha, japo alikuwa HKL, ila alizungusha"
"Poleni sana"
"Asate, eheee na wewe umemtolea wapi huyu bibie muarabu si muarabu, mzungu si mzungu?"
Nikaanza, kumuadisia John mkasa mzima wa maisha niliyo pitia kuanzia siku nilipokuwa nikitafutwa Tanzania na kukimbilia nchini Kenya ambapo ndipo, safari yangu yakwenda nchini Iraq ilipo anza, nikamuelezea jinsi nilivyokutana na Phidaya, na alivyokuwa msaada mkubwa sana kwenye masha yangu
"Ninampenda sana Phidaya"
"Unauhakika?"
"Ndio, asilimia mia"
"Mmmmm ni yule Eddy ninaye mjua mimi, au kwa maana wewe ulikuwa mzee wa Gologolo"
"Hahaaaa, nimkekuwa mtu wangu, hapa nipo kwenye majukumu yakuitwa baba"
"Safi ndugu yangu, ila nakutobolea siri moja?"
"Siri gani?"
"Sheila anakupenda sana, na hapa yupo anakusubiria wewe"
"Mmmmm,"
Nilijikuta nikiguna, huku mapigo yamoyo yakianza kunienda mbio, mwili mzima ukaanza kusisimka, na nywele kichwani zikaanza, kunisisimka, jambo ambalo kwenye maisha yangu halikuwahi kutokea siku hata moja.Nikasimama haraka huku akilini mwangu nikmfikiria Phidaya
"Eddy unakwenda wapi?"
"Chumbani"
Nilizungumza huku nikizidi kupiga hatua za haraka, nikaingia kwenye lifti pamoja na John, ambaye alikuwa akinifwata kwa nyuma, ikasimama kwenye ghorofa ya tatu, kama jinsi nilivyo minya batani ya ghorofa hii ambayo niyatatu, nikaanza kukimbia kuelekea chumbani kwangu, nilipo muacha mke wangu akiwa amelala, wasiwasi mwingi ukiwa umenitawala, nikafika kwenye mlango wachumba changu, nikaufungua kwa nguvu, kitu cha kwanza kutazama nikitandani, nikastuka kukuta mke wangu hayupo huku shuka jeupe lililo tandikwa juu yakitanda likiwa limejaa damu nyingi, jambo lilizozidi kustua mimi na John

ITAENDELEA
 
****SORY MADAM*****(67)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA
"Chumbani"
Nilizungumza huku nikizidi kupiga hatua za haraka, nikaingia kwenye lifti pamoja na John, ambaye alikuwa akinifwata kwa nyuma, ikasimama kwenye ghorofa ya tatu, kama jinsi nilivyo minya batani ya ghorofa hii ambayo niyatatu, nikaanza kukimbia kuelekea chumbani kwangu, nilipo muacha mke wangu akiwa amelala, wasiwasi mwingi ukiwa umenitawala, nikafika kwenye mlango wachumba changu, nikaufungua kwa nguvu, kitu cha kwanza kutazama nikitandani, nikastuka kukuta mke wangu hayupo huku shuka jeupe lililo tandikwa juu yakitanda likiwa limejaa damu nyingi, jambo lilizozidi kutustua mimi na John
ENDELEA
Nikakimbilia kwenye mlango wa kuingilia bafuni, ila sikufanikiwa kumuona Phidaya, joto kali la mwili likaanza kuambatana na woga ambao tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kuupata siku hata moja, nikatizama kila shemu ya chumba hadi chini ya uvungu ila sikumuona mke wangu, machozi kwa mbali yakaanza kunilenga lenga, huku nikijaribu kutafakari ni nini nifanye
"Kwani alikuwa humu ndani?"
Nilijikuta nikiachia msunyo mkali, baada ya John kuniuliza swali ambalo jibu analo kichwani mwake, kwani muda nilipokuwa ninatoka nilikuwa nipo mwenyewe, na sote tumekuta damu juu yakitanda iweje aniulize kwamba alikuwepo humu ndani, nikatoka kwa hatua za haraka, huku shati nililo livaa likiwa linavuja jasho jingi, sana
"Sasa Eddy unakwenda wapi?"
John aliniuliza huku akinifwatwa kwanyuma tukielekea zilipo lifti za ghorofa hili, sikumjibu John chochote kwa maana ninahisi, hatambui nini umuhimu wa mke, isitoshe mke mwenye kiumbe change tumboni, kupotea katika mazingira yakutatanisha, tukaingia kwenye lifti ambayo kuta zake nne zina vioo, nikawa na kazi yakujitazama jinsi macho yangu yanavyo tiririsha machozi yanayotoka pasipo kuwa na kilio, huku wekundu ukiwa umetawala kwenye macho yangu, John akanipa kitambaa chake ili nikisaidie kufuta machozi
"Nimepata wazo, hembu twende kwenye chumba cha ulinzi kwa maana humu ndani kuna kamera za ulinzi kila kona"
John alizungumza huku akinitazama usoni, wazo lake kidogo likarudisha ufahamu kwani kitu ninacho kifikiria ni Phidaya na kiumbe change, kitarajiwa
"Samahani dada"
John alizungumza na muhudumu mmoja kwa kingereza, mara baada ya sisi kutoka kwenye lifti iliyo tufikisha chini kabisa katika eneo tulilokuwepo
"Bila samahni?"
"Ninaomba kuuliza ni wapi kwenye chumba cha CCTV camera"
"Kwani kuna tatizo?"
"Ndio lipo, kuna dada mmoja, ni mjamzito amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, mume wake alimuacha chumbani akiwa amelala ila tulipo kwenye hatujamkuta"
"Mmmm kuseme ukweli, mimi sijaona dada mjamzito akitoka, labda chakuwasaidia nyinyi, nikuwapeleka kwa meneja na yeye ndio atatoa idhini ya nyinyi kupelekwa kwenye hicho chumba"
"Asante dada"
Sikuchangia neon lolote zaidi yakuwasikiliza John na muhudumu jinsi wanavyo zungumza, huku macho yangu yakitazama kila upande wa sehemu tulipo simama, nikastukia nikuvutwa mkono na John ambao tayari walishaanza kuondoka na kuniacha mimi nikiwa nimesimama kama sanamu, lakuongozwa na betrii
"Kaka, usijali shemeji atapatikana, ninaimani hawezi kuondoka humu ndani ya Hoteli kwa hali ile"
John aliendelea kuzungumza huku tukipiga hatua tukimwafwata dada, huyu kwanyuma, tukaingia kwenye moja ya chumba ambapo macho yangu hayakuwa ngeni kwa mtu aliye kaa kwenye kiti hichi huku akionekana kwamba ndio meneja wa hii hoteli
"Meneja kuna, hawa wageni wa….."
Meneja wake akainua mkono, kwa ishara ya kumkatisha mfanyakazi wake, na meneja wake akapiga hatua za haraka hadi sehemu nilipo simama mimi, huku akiwa ametabasamu usoni mwake, akanikumbatia kwa furaha, hapa ndipo nikapata uhakika kwamba ni mlinzi wa baba, ambaye kuna kipindi alinipeleka kwenye benki, nikatoe pesa kwa ajili ya kununulia siku ila ndipo nilipokutana na Sheila baada ya jamaa kumkuta akiminyana na Sheila aliyekuwa amechanganyikiwa
"Eddy umekuwa mkubwa mdogo wangu"
Jamaa alizungumza huku akitabasamu, na mimi nikajikaza niweke tabasamu lakinafki ili mradi tu nisalimieane naye
"Eddy mbona kama umepoteza furaha usoni mwako, unatatizo gani?"
Nikamuelezea jamaa jambo linalonisumbua,bila kupoteza muda akaniomba tuelekea chumba maalumu chenye video nyingi zinazoonyesha maeneo mbalimbali ya hotel, tukaanza kuonyeshwa matukio yaliyo pita muda mchache kwenye eneo la chumba chetu kilipo, tukashuhudia kumuaona mwanake aliye valia baibui lililo mficha sura yake akiingia ndani ya chumba change, muda mchache baada ya mimi kutoka, ndani ya dakika kadhaa akatoka akiwa amembeba mke wangu, kwenye mikono yake huku akiwa amemfunika kwa shuka jeupe, kama mtu aliye uwawa.
"Peleka mbele kidogo"
Jamaa alizungumza na kumfanya muongozaji wa video hizi kupeleka picha za video mbele kidogo, ambapo tukamshuhudia mwanamke huyo ambaya hadi sasa, hivi sura yake hatukuiona, akimuingiza mke wangu kwenye gari yawagonjwa na kuondoka naye, pasipo watu kumshuhudia
"Ujinga huu, ulipo kuwa unafanyika mulikuwa wapi?"
Jamaa alizungumza huku akimfokea mfanyakazi wake anaye ongoza mitambo ya kamera za ulinzia, mwili mzima ukaanza kunitetemeka na kujikuta nikizidi kuchanganyikiwa pasipo kujua ni kitu gani ambacho, nilimemkosea huyu mwanamke aliye mteka mke wangu, kila mmoja akabaki kimya akimtazama mwenzake asijue nini chakufanya
"Sasa hapa itakuwaje?"
John alizungumza na kumfanya jamaa, ambaye hadi sasa hivi jina lake silifahamu kutokana sikuwa na mazoea naye sana kipindi yupo nyumbani kwa baba, akatoa simu yake na kuminya baadhi ya namba na kuiweka simu yake sikioni, akaanza kuzungumza lugha ya kizulu, ambayo kwangu si ngeni sana japo siifahamu.Akamaliza kuzungumza na simu na kututazama
"Nimewasiliana na makao makuu ya polisi hapa ‘Johannesburg' na wameniambia wanaanza kulifanyia kazi muda huu"
"Sa..sa umesema wanafanyia kazi?"
Nilizungumza kwa kiwewe kikubwa huku nikimtazama jamaa
"Ndio wameshaanza kulifanyia kazi, kwani nimewatajia hadi namba za gari kuhakikisha wanalinasa gari husika"
Jasho halikuacha kunitiririka japo kuwa ndani ya chumba hichi kuna baridi nzuri yajutosha, jamaa akamuomba mtu wake azitume picha za gari na mwanamke hukyo makao makuu ya polisi kupitia mtandao(internet), ili kuzidi kuwarahisishia kazi askari polisi
"Eddy usiwe na wasiwasi, kama tukio limefanyika kwenye hoteli hii basi, muhalifu aliye mteka mke wako atapatika tu"
"Ila mke wangu atakuwa amesha fariki"
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, twasira za sura ya mke wangu masaa machache ya nyuma yaliyo pita zikaanza kunisumbua kichwani mwangu, nikajikuta nikianza kujilaamu nikwanini nilitoka chumbani kwangu na kumuacha Phidaya wangu akiwa amelala peke yake, jamaa akasogea pembeni na kuzungumza na simu, sikujua anazungumza na nani, baada ya muda akarudi tulipo
"Eddy nilikuwa nikizungumza na baba yako, na yupo njiani anakuja"
"Baba yake!?"
John aliuliza huku akiwa ameshangaa, sikutaka kumjibu kitu chochote zaidi ya kujikalia zangu kwenye kiti huku mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio, ndani ya dakika ishirini, mlango ukafunguliwa na akaingia baba akiwa na walinzi wake wanne walio valia suti nyeusi pamoja na miwani, nikanyanyuka kwenye kiti na kukumbatiana na baba huku akionekana kuwa nafuraha usoni mwake, kwani hakuamini uwepo wangu, jamaa akaanza kumuelezea baba kila kitu kilicho tokea na kumuonyesha baadhi ya video hizo za mwanamke aliye mteka mke wangu
"Pole sana Eddy"
Baba alinipa pole na mimi nikaiitikia kwa sauti ya chini, tukatoka ndani ya chumba nikiwa nimeongozana na baba pamoja na walinzi wake, huku jamaa na John wakifwata kwa nyuma, tukakuta polisi wakiwa wanafanya vipimo kwenye chumba change
"Mumefikia wapi?"
Baba alimuuliza mmoja wa polisi
"Hii damu, inaonekana si damu ya mauaji"
"Kivipi?" Baba aliuliza tena
"Inaonekana mtekaji alimwaga damu kwenye shuka kutoka kwenye pakti za kuhifadhia damu"
Askari alituambia huku akituonyesha pakti mbili za kuhifadhia damu, walizo zitoa ndani ya chumba changu baada ya kukifanyia uchunguzi sana
"Ila mtekaji atapatikana kwa maana inaonekana hajatoka mbali sana na hapa"
Polisi alizungumza, ila moyo wangu haukuwa na furaha hata kidogo japo wanadai kwamba ni damu ndizo zilizo mwagwa kwenye shuka la chumbani kwetu, tukatoka na baba hadi sehemu ya kupumzikia, ukimya ukatawala kati yetu, hapakuwa na aliye zungumza kitu chochote zaidi ya mimi kutazama tazama mandhari yaliyomo humu ndani
"Eddy, ulikuwa wapi mwanangu?"
"Baba, ngoja hayo mazungumzo tutayazungumza baada ya kufikia muafaka kutambua ni wapi alipo mke wangu"
Nilizungumza kwasauti nzito iliyo jaa hasira ndani yake, baba alinielewa na kukaa kimya hakutaka aendelea kunigusia kuhusiana na kitu cha aina yoyote.Simu ya baba ikaita na akaanza kuzungumza na mtu aliye mpigia
"Eddy twende sehemu, lile gari lawagonjwa limepatikana"
Baba aliniambia mara baada ya simu kukata, nikawa wakwanza kunyanyuka kwenye kiti na kuanza kuongozana, tukaingia kwenye gari huku John akiingia kwenye gari ya jamaa ambaye ni meneja wa hoteli.Tukatembea umbali wa kilomita kumi, tukafika pembezoni mwa mlima na kuwakuta polisi wengi wakiwa wamelizingira gari lawagonjwa, kwa umbali kidogo ambalo pembeni limezungushiwa mabomo yakutega yapatayo sita, bomo moja nikaliona likiwa limebakisha sekunde hamsini huku zikiendelea kurudi nyuma taratibu
"Phidaya"
Nilianza kukimbia kuelekea lilipo gari lawagonjwa polisi wakanidaka, na kunizuia nisiendelee kwenda mbele, gafla mlipuko mkubwa ukalipuka kwenye gari na kusababisha polisi walio nikamata kuniangusha chini na kunifunika na miili yao waliyo valia nguo maalumu zinazo zuia kuadhirika na vipande pande vya vyuma vitokanavyo na mabomu endapo vitawaangukia
"Phidayaaaaaaaaaaaaaaaaaa"
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku machozi ya uchungu yakinimwagika usoni mwangu, huku nikilishuhudia gari alilopo mke wangu likiteketea kwa moto mkali

ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(68)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA

ILIOISHIA
Nilianza kukimbia kuelekea lilipo gari lawagonjwa polisi wakanidaka, na kunizuia nisiendelee kwenda mbele, gafla mlipuko mkubwa ukalipuka kwenye gari na kusababisha polisi walio nikamata kuniangusha chini na kunifunika na miili yao waliyo valia nguo maalumu zinazo zuia kuadhirika na vipande pande vya vyuma vitokanavyo na mabomu endapo vitawaangukia
"Phidayaaaaaaaaaaaaaaaaaa"
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku machozi ya uchungu yakinimwagika usoni mwangu, huku nikilishuhudia gari alilopo mke wangu likiteketea kwa moto mkali

ENDELEA
Askari wa kikosi cha zima moto wakaanza kulishambulia gari la wagonjwa kwa kutumia mipira mirefu inayotoa maji kwa kasi kiasi kwamba, moto ukaanza kupunguza makali yake ya kuteketea, amchozi yalizidi kunitoka huku askari wakiendelea kunizuia nisikaribie eneo ambalo lipo gari, wakanikabidhi kwa walinzi wa baba, ambao waliendelea kunishika.Si mimi tu ambaye nipo kwenye huzuni, ila hata rafiki yangu John, machozi yalianza kumtoka, na kuzidi kunizidishia hisia ya kumwagikwa na machozi mengi
"Eddy, jikaze mwanangu"
Baba alizungumza huku akinikumbatia, akiendelea kunipigapiga mgongoni ikiwa ni ishara ya kunituliza hasira na uchungu ambao nimeupata, askari wengine wakaanza kazi ya kuchambua kama kuna kitu kilicho salia kwenye gari, ikiwemo kupata udhibitisho wa kama kuna mwili wa mtu ambaye alikuwepo ndani ya gari, mwili mzima ukazidi kunitetemeka kwa woga, kila ninapojaribu kutazama gari lililo teketea kwa moto, dua yangu kubwa ni kumuomba Mungu aweze kutenda miujiza Phidaya asiwepo ndani ya gari hilo.
Askari mmoja akatufwata sehemu nilipo simama mimi pamoja na askari wa baba, huku mkononi mwake akiwa ameshika kibegi kidogo, na viganjani mwake akiwa amevaa gloves nyeusi.Akamsalimia baba, kasha akatusalimia na sisi, akamuomba baba wazungumze pembeni, baba akatii ombi la askari huyo, sikusikia kitu ambacho wanakizungumza
Mlio wa simu ya John, ukanistua kutoka katika dimbwi kubwa la mawazo na kujikuta nikimgeumkia na kumtazama kwa macho yaliyo jaa huzuni nyingi, John akaitazama simu yake kwa muda huku akiwa amekunja ndita, akaipokea na kukaa kimya
"Nani mwenzangu?"
John alizungumza baada ya sekunde kadhaa ya simu yake kuwa sikioni
"Hapana, mimi ninawapa watu wengi namba yangu, kwahiyo usipo taja jina lako mimi siwezi kutambua kwamba wewe ni nani?
John alizungumza kwa sauti ya ukali huku macho yake akiya pepesa pepesa
"Wee mwendawazimu nini, usinichangenye"
John alizungumza huku akiachia msunyo mkali na kukata simu yake, nikaanza kupiga hatua kulifwata gari lililo teketea ambapo kuna askari, pamoja na madaktari wakiendelea kufanya uchunguzi na vifaa vyao maalumu.Nikafanikiwa kufika pasipo mtu yoyote kunishika mkono, nikakuta wakiyapiga picha, mafuvu mawili ya watu, yaliyo tekete kwa moto, ikiashiria kwamba miili yao, imesha teketea, nikajikuta nikianguka chini kama mzigo, kutokana na kuishiwa na guvu za mwili wangu.
Madaktari wakaniwahi kunipa huduma ya kwanza, ikiwemo kuniwekea mashine ya kunisaidia kuhema, japo fahamu hazijanipotea, ila sikuwa na uwezo wakuuamuru mwili wangu kufanya kitu, ambacho ninakihitaji, machozi yakaanza kunichuruzika, kumbukumbu za gari kulipuka dakika chache zilizo pita zikaanza kunijia kichwani mwangu, nikaanza kuisikia sauti ya Phidaya kwa mbali ikiniita masikioni mwangu, nikataka kunyanyuka, ila madaktari wakanizuia nisinyanyuke
"Mwanangu atapona?"
"Ndio mzee atapona, ni mstuko tu, ndio umempata ulio pelekea yeye kuishiwa na nguvu, kidogo na uwezo wa moyo wake ulishindwa kudunda kama inavyo paswa ufanye"
Daktari mmoja nilimsikia akimjibu baba, huku wezake wakiniinyanyua kwenye machela, waliyo kuwa wameniweka wakinipatia huduma ya kwanza na kuniiingiza ndani ya gari.John akawahi kuingia ndani ya gari la wagonjwa, lililokuja muda mchache baada ya mimi kuanguka chini.
"Eddy"
John aliniita, na kumtazama taratibu, pasipo kumjibu kitu chochote, kwani hata kuzungumza kumenishinda kabisa
"Mungu, atasaidia kila kitu kitakuwa sawa"
John alizungumza kwa kunifariji tu, kwani ukweli halisi nimeshaujua, kwamba Phidaya sipo naye tena duniani, kwani mafuvu mawili ni yawatu ambao nimeyakuta kwenye gari, yanaashiria kwamba ni mke wangu ni marehemu.
Wakanishusha kwenye gari, wakaniweka kwenye kitanda cha kusukuma, manesi wawili wakaanza kukisukuma kitanda nilicho lalia hadi kwenye moja ya chumba na kuniingiza humu, nikakuta madaktari wawili wakiwa ndani ya chumba wakiwa tayari kwa kunihudumia.Wakanichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto sehemu ya mshipa wa damu, kasha waniwekea baadhi ya vifaa kifuani kwangu, ambavyo sikuelewa kazi yake ni nini.Wakamaliza kufanya kazi yao, ya kunihudumia na kutoka ndani ya chumba, msongamano wa mawazo ukazidi kunipelekesh, huku sura ya mke wangu Phidaya ikiwa haichezi mbali na fikra zangu
"Eddy I love you"(Eddy ninakupenda)
Sauti ya Phidaya ikaendelea, kusikika kwenye masikio yangu, nikajitahidi kuyazungusha macho yangu kila pande ya chumba kutazama kama nitaweza kumuona mke wangu ila sikufanikiwa, kuiona sura yake.Baada ya masaa manne mlango ukafunguliwa na akaingia baba pamoja na John, kila mmoja anaonekaa kuwa na huzuni, baba akasimama pembeni ya kitanda change, huku John akikaa sehemu ndogo ya kitanda nilicho lalia
"Unajisikiaje mwangu"
"Safi"
Nilimjibu baba kwa sauti ya chini, iliyo jaa mkwaruzo
"Baba, yale mafuvu yapo wapi?"
Baba hakunijibu zaidi ya kumtazama John, kisha wakanitazama hakuna aliye jibu swali langu, ila macho yao nikatambua kwamba yanakitu wanacho kijua ila wananificha
"Ahaa…., inabidi kwamba…… Ahaaa kesho urudi nyumbani, ukapumzike kwa muda kidogo ili uwe sawa"
Baba alizungumza kwa kubabaika, nikamtazama John, akatizama chini baada ya macho yangu kukumbana na macho yangu.Simu ya baba ikaita ikambidi atoke nje kwenda kuipokea
"John niambie ukweli mke wangu amekufa?"
"Eddy………………"
John aliniita, nikabaki nikimtazama pasipo kumuitikia.Ukimya ukatawala, kama dakika mbili John hakunijibu swali langu nililo muuliza.Kijimlio kifupi kikasikika kwenye simu ya John iliyopo mfukoni, ikamlazimu kuitoa simu yake, mfukoni.Akasoma meseji aliyo ingia, akanitazama kwa jicho la kuiba na kuitazama tena meseji anayo isoma
"Kaka hembu soma hicho kilicho indikwa"
John akanipa simu, kabla sijaisoma meseji iliyopo kwenye simu, baba akaingia ndani akiwa ameongozana na madaktari walio, nitibu muda mchache ulio pita, wakafika kwenye kitandani nilicho lala.Daktari mmoja akanitoa vifaa walivyo niwekea kifuani,
"How do you feel?"(Unajisikiaje?)
Daktari mmoja aliniuliza
"Najisikia powa"
Daktari wa pili akaniwekea kifaa kigo cha kusikilizia mapigo ya moyo, akamtazama baba
"Kwa sasa yupo salama, tunaweza kumruhusu kurudi nyumbani"
"Shukrani daktari"
Baba alizungumza, huku akimpa mkono dokta, wakanipa vidonge vya kuupa mwili wangu nguvu, nikaruhusiwa kutoka hospitalini, tayari giza lilisha anza kutawala anga, kwa mbali, ikiwa ni majira ya jioni, tukaingia kwenye gari moja mimi pamoja na John, huku baba akiwa katika gari lake jengine
"Uliisoma ile meseji?"
"Ngoja noisome"
Nikaitoa simu mfukoni na kumpa John anitolee namba za siri alizo ziweka kwenye simu yake upende wa meseji kisha akanirudishia
{KAA MBALI NA HII VITA KATI YANGU MIMI NA EDDY, UTAUMIA}
Nikairudia kuisoma tena meseji kwa msisitizo, kisha nikamtazama John, huku mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio
"Nani aliye ituma hii meseji?"
"Mimi wala sijui, kutoka hata namba yenyewe haionekani"
"Mmmmmm, ulimuonyesha mtu mwengine tofauti yang?"
"Pale ilipokuwa inaingia, ndio nikakukabidhi hiyo simu"
Nikashusha pumzi kubwa huku nikiendelea kumtizama John machoni, nikajaribu kuipiga namba iliyo tuma hii meseji ila haikenda zaidi ya kukatika.Tukafika nyumbani kwa baba, mazingira nikayakuta yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana, kuanzia nje hadi ndani, sikumkuta yule mama wa kambo aliyekuwa akinisumbua akili yangu kipindi nilipokuja kwa mara ya kwanza
"Una mpango gani, juu ya hili Eddy?"
Baba aliniuliza mara baada ya mimi, kukaa kwenye moja ya sofa lililopo hapa sebleni, nikakaa kimya kwa muda kabla sijamjibu baba, kwani akili yangu ikaanza kutafakari juu ya meseji aliyo tumiwa John, inavyo onekana mtu huyo ananijua mimi vizuri ndio maana ameamua kunifanyia unyama wa kumuangamiza mke wangu
"Sijajua baba"
Jibu langu, likamfanya John kunitazama kwa mashangao
"Ngoja tupate ripoti ya polisi juu ya muhusika, wa tukio zima kisha tutajua nini cha kufanya"
"Sawa baba"
Baba alizungumza na kuanza kupandisha ngazi kuelekea ghorofani, nikasikia sauti ya kike ikizungumza na baba, ikanilazimu kusimama kutazama ni nani anaye zungumza naye, macho yangu yakakutana na macho ya mototo wa mama wa kambo, ambaye kipindi ninakuja kwa mara ya kwanza nyumbani kwa baba, yeye alikuwa chuo akisoma
"Waoooo kaka Eddy"
Alinikimbilia na kunikumbatia kwa furaha, sikuamini macho yangu kwani mimi na yeye kidogo kuta tofauti zilizo tokea kipindi cha nyuma, hususani swala la mimi kumpiga mama yake
"Za huku utokapo?"
"Si salama"
Nikamuona John akimshangaa huyu dada yangu, akataka kumpa mkono ila akasita, ikanilazimu nimtambulishe mimi
"Dada huyu ni rafiki yangu anaitwa John, na John huyu ni motto mwengine wa baba yangu"
"Nashukuru kukufahamu"
John alizungumza huku akimpa mkono dada yangu
"Eddy unatabia mbaya"
"Kwa nini dada?"
"Hadi leo hulitambui jina langu"
"Ahaaa"
Nilibaki nikitabasamu tu, kwani ni kweli jina lake sikuwa ninalikumbuka vuzuri
"Mimi ni Victori"
"Ahaaa, kama lilikuwa likinijia kwenye akili yangu vile?"
"Kwenda kulee, ulikuwa hulijui"
Alizungumza kwa utani, huku akiichezea chezea mikono yangu, tukatizamana kwenye macho kwa sekunde kadhaa, sote tukajikuta tukiwa kimya
"Mama yupo wapi?"
Nilimuuliza na kumfanya apooze gafla, akaniachia mikono yangu na kwenda kukaa kwenye moja ya sofa, huku machozi yakimlenga lenga, akainyanyua sura yake kidogo na kunitazama
"Mama, amesha fariki"
Alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakianza kumtoka, nikapiga hatua hadi alipo kaaa, nikamkumbatia, huku na mimi hisia za mke wangu kufa, zikaanza kunijia kichwani
"Eddy kwa nini unalia?"
"Mke wangu amekufa"
"Weeee"
Victoria alistuka baada ya kusikia maneno haya
"Amefariki lini?"
"Leo"
"Leoooo?"
"Ndio"
"Kwa nini?"
"Amefariki kwa mlipuko wa bomu baada ya kutekwa, na mtu asiye julikana"
John akabaki akitutizama jinsi tunavyo zungumza mimi na dada yangu, Victoria akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kunibembeleza kwa hisia kali, tukaachana na stori za kufa kwa mke wangu, tukaendelea kuzungumza kuhusiana na mambo mengine, muda wa chakula ukawadia na sote tukakaa kwenye meza maalumu ya chakula, nikagundua kitu kutoka kwa John, wakati wote alikuwa na kazi ya kumtazama Victoria kwa macho ya kumtamani.Tukamaliza kula mimi na John, tukaelekea kwenye chumba change
"John mbona ulikuwa unamtazama sana Victoria?"
"Hapana"
"Mmmmm john wewe hakuna cha hapana, au umempenda nikuunganishine"
"Ahaaa Eddy, ila ngija kuna kitu ninakichunguza, kikikamilika nitakuambia"
"Kitu gani?"
John akautazama mlango wa kuingilia humu ndani ya chumba change, akapiga hatua za taratibu huku akiniomba ninyamaze kuzungumza, akaliweka sikio moja kwenye mlango, huku mkono wake mwingine ukishika kitasa cha kufungulia mlango, akaanza kuufungua taratibu, mimi nikawa na kazi ya kumtazama jinsi anavyo fanya.Akauvuta kwa nguvu, macho yetu yote yakakutana na Victoria akiwa amevalia nguo ya kulalia, inayo onyesha nguo yake ya ndani
"Vicktoria vipi?"
Nilimuuliza Victoria baada ya yeye kushindwa kuzungumza kitu kinacho mfanya asimame nje ya mlango wetu, akaanza kuvunja vinja vidole vyake kwa aibu, akamtazama John, ambaye hakuwa amezungumza kitu cha aina yoyote, akamshika John shati lake, kisha akamvuta karibu yake na kumpiga busu la mdomo na kunifanya nibaki nikiwa ninamshangao
"I need you John"(John, ninakuhitaji)
Victoria alizungumza huku akimsukumia John ndani ya chumba, changu, kama simba mwenye njaa Victoria akamsukumiza John kitandani na kuanza kumvua shati, lake, kwa aibu ikanilazimu mimi kutoka ndani ya chumba nikawaacha waendelee na mambo yao
****Ni maamuzi gani atakayo yachukua, Eddy kwa mtu aliye husika na kifo cha mke wake, usikose kufwatilia simulizi hii ya kusisimua hapa hapa kwenye ukurasa wa Story Za Eddy****
ITAENDELEA
 
*****SORY MADAM*****(69)

AGE....................................................................18+
WRITER.............................................................EDDAZARIA G.MSULWA

ILIOISHIA
Nilimuuliza Victoria baada ya yeye kushindwa kuzungumza kitu kinacho mfanya asimame nje ya mlango wetu, akaanza kuvunja vinja vidole vyake kwa aibu, akamtazama John, ambaye hakuwa amezungumza kitu cha aina yoyote, akamshika John shati lake, kisha akamvuta karibu yake na kumpiga busu la mdomo na kunifanya nibaki nikiwa ninamshangao
"I need you John"(John, ninakuhitaji)
Victoria alizungumza huku akimsukumia John ndani ya chumba, changu, kama simba mwenye njaa Victoria akamsukumiza John kitandani na kuanza kumvua shati, lake, kwa aibu ikanilazimu mimi kutoka ndani ya chumba nikawaacha waendelee na mambo yao
ENDELEA
Nikaelekea moja kwa moja jikoni, nikachukua maji ya kunywa kwenye friji lililopo humu jikoni, kisha nikakaa kwenye kiti kirefu ambacho nacho kipo humu ndani ya chumba.Mawazo yakaanza kurudi upa juu ya mtu aliye mteka mke wangu na kumuua kinyama kwa kumlipua kwa bomu
"Nilazima nilipize kisasi kwa yoyote aliye husika katika hili"
Nilijiapiza kimya kimya huku nikiyatazama maji yaliyopo kwenye glasi niliyo ishika mkononi mwangu, nikaitazama saa ya ukutani na kukuta ikionyesha ni saa sita kasoro dakika ishirini, usiku
"Hawamalizi na sasa hivi"
Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye kiti na kutoka nje, na kuwakuta walinzi wakizunguka zunguka kaimarisha ulinzi wa jumba hili la baba yangu, sikutaka kuzungumza na mtu wa aina yoyote zaidi ya kubatazama mandhari mazuri yalipomo kwenye eneo hili
"Hei"
Nilimuita mlinzi mmoja aliye kuwa anakatiza karibu yangu
"Ndio bosi"
Kwa bahati nzuri mlinzi huyu alinijibu kwa Kiswahili
"Ninaweza pata usafiri muda huu"
"Kivipi?"
"Nina maanisha ninaweza kupata gari, lolote lenye funguo"
"Unataka kwenda wapi usiku huu?"
"Kuna sehemu ninahitaji kwenda"
"Kwa hapo, ndugu siwezi kukusaidia kwani bosi hajatoa ruhusa ya mtu yoyote kutoka na usafiri, tena muda huu wa usiku"
"Ahaa powa asante"
Nikaachana na mlinzi na kurudi ndani, nikafika hadi mlango wa kuingilia chumbani kwangu, nikaweka sikio la upande wa kulia, nikasikia miguno ya mahaba ikiwa inaendelea ndani ya chumba change.
"Mmmm kazi kweli kweli"
Nikapata wazo la kwenda chumbani kwa Victoria japo kuegesha kichwa change kidogo, hii ni kutokana na uchovu mwingi.Nikaingia na kuwasha taa, kitu cha kwanza nikakutana na mwanga wa simu ya Victoria, ikionyesha ni muda mfupi kuna meseji au simu ilipigwa.Nikapiga hatua hadi kitandani ilipo, nikaichukua na kutazama, na kukuta missed call na namba ambayo haikuwa na jina lolote.Nikafungua kipochi chake kilicho kuwa pembezoni mwa simu, nikakuta noti kumi za dola mia mia
"Yess, kazi yangu imeanza kukamilika"
Nikazichomoa noti hizo, na kuzidumbukiza kwenye mfuko wa jinzi langu, ambapo kuna simu ya John, aliyo nikabidhi muda wa mchana.Nikatazama salio kwenye simu ya Victoria nikakuta lipo lakutosha, nikaiweka mfukoni, nikafungua kabatini kwake na kukuta makoti mengi makubwa ya baridi.Nikachukua koti jeusi na kulivaa, nikachukua kofia ya kuzuia baridi na kuivaa, nikatoka nje ya chumba cha Victoria.Kutokana ni mzoefu sana wa jumba hili la baba haikuwa, ngumu sana kwangu kutoroka pasipo walinzi kunioa, nikatoka nje ya ukuta wa jumba hili, kwa kuuruka, nikaanza kutembea kuelekea barabara kuu, kwa bahati nzuri nikapata taksi
"Nipeleke kwenye uwanja wa ndege, wa ‘Johannesburg', itakuwa ni bei gani?"
"Dola mia"
"Sawa"
Kutokana nina kiasi cha kutosha cha pesa, sikuwa na haja ya kumbembeleza dereva huyu, japo ninatambua amenipiga kizinga, kutokana na ugeni wangu, tukatumia dakika ishirini kufika uwanja wa ndege.
"Unaweza kunisubiri?"
"Bili shaka"
Nikampa dereva taksi pesa yake, nikaelekea sehemu ya huduma kwa wateja, na kuwakuta dada kadhaa wakiwa wamejipanga wakizungumza na baadhi ya abiria waliopo kwenye eneo hili
"Samahani dada"
"Bila samahani, nikusaidie nini?"
"Juzi usiku, kuamkia jana nilifika hapa na ndege ya shirika la nchini Philipines, kuna kitu ninahitaji kukipata kwenye kwenye safari ile"
"Kitu gani?"
Dada huyo alinijibu kwa umakini, huku akinitazama usoni
"Nahitaji video zilizo rekodiwa kwenye safari nzima, kutoka Philipines hadi hapa South Africa"
"Eheeeee, kaka yangu, mbona hiyo ni kazi kubwa sana, na kwakitengo changu, mimi siwezi kukusaidia"
"Unaweza, nitakupa pesa yoyo……"
Mngurumo(vibration) wa simu ya Vivtoria, ukaanza kutetemesha mfuko wangu, ikanilazimu kuitoa simu yake na kukuta meseji ikiwa imeingia, nikaifungua ila nikakutana na batani nyingi zikiniomba niiingize neno la siri ili niweze kuifungua meseji hiyo
"Akhaaaa"
Nilijisemea mwenye baada ya kushindwa kuifungua meseji hiyo, nikamgeukia dada niliyo kuwa nikizungumza naye, nikakuta akimalizia kumnong'oneza rafiki yake, aliye kaa kiti cha pembeni yake
"Niambie sasa dada, inawez……"
Akanikatisha mazungumzo yangu, kwa kunikonyeza kwa jicho lake kubwa kiasi, akanionyeshea ishara kwa macho nitazame juu yangu, nikakuta kameta ya ulinzi ikinirekodi
"Nifwate"
Alizungumza kwa sauti ya chini, akajinyanyua kwenye kiti alicho kalia, akatoka kwenye chumba walichopo nikaanza kuongozana naye kuelekea anapo kwenda yeye, tukapandisha kwenye ngazi, sikujua ni wapi ananipeleka.Tukafika kwenye moja ya ukumbi wenye viti vingi, vya kupumzikia.Akatafuta sehemu iliyo tulia na kuniomba nikae
"Eheee kaka ulikuwa unasemaje?"
Nikamuelezea nini ninacho kihitaji, akaniomba nimsubiri kama dakika kadhaa atarudi na kitu ambacho ninahitaji, ila akaniomba nimpatie malipo ya awali, na tulikubaliana nimpatie dola mia tano kwa kazi atakayo nifanyia.Nikaito simu ya John na kufungua upande wa picha, nikajikuta nikistuka baada ya kuzikuta picha za John na Victoria wakiwa pamoja, kwenye fukwe za bahari, ila sikujua ni nchi gani.Nikazidi kwenda mbele na kukuta picha nyingi wakiwa pamoja, hapa ndipo nikagundua kuna mahusiano ya kimapenzi kati ya John na Victori
"Ahaaa, ndio maana nilivyo kuwa ninawatambulisha John alistuka, kumuona Victori…."
Nilijisemea mimi mwenye, kimoyo moyo, huku nikiendelea kuzitazama picha walizo piga pamoja, nikaingia upande wa namba za simu na kuanza kuandika jina la Victoria na kukuta likiwa limeandikwa ‘MY WIFE V', Nikajaribu kuipiga namba, ikaingia kwenye simu ya Victoria na kutokea jina la ‘BABY JOHN'
"Wamejuana juana vipi?"
Ni moja ya swali lililo anza kuniumiza kichwa change, kabla sijajipatia jibu kichwani mwangu, muhudumu akarudi akiwa ameshika laptop ndogo mkononi mwake.
"Chukua hii, nenda chooni, katazame kuna video nimeiiba ndani kwenye chumba cha mawasiliano"
"Powa"
"Fanya haraka mimi ninakusubiria hapa, nenda moja kwa moja kwenye ile kordo kunja kulia, utakuta vyoo"
Nikanyanyuka katika sehemu nilipo kaa, moja kwa moja nikaelekea katika sehemu alipo nielekeza muhudumu huyu, nikaingia kwenye choo cha wanaume, nikaifungua laptop aliyo nipa na kukuta faili moja lili andikwa video, nikalifungua
Nikaanza kuona mkanda wa video, katika ndege ya shirika la Philipines, video hii imerekodiwa kwa kamera za ulinzi lilizipo kwenye ndege tulio kuja nayo, nikaanza kuona abiria wakiingia, ikiwemo mimi na Phidaya.Ikanilazimu kuisimamisha video mara moja baada ya kumuona Victoria akiingia ndani ya ndege hii, ila alikaa siti ya nyuma kabisa, pamoja na abiria mwengine.Katikati ya safari nikamuona John akiwa anazungumza mara kwa mara na Victoria, pia nikaona jinsi John alivyokuwa akizungumza na mimi.Hadi ndege inafika, na sisi tunatoka kwenye ndege nikaumuona John akizungumza na Victoria, wakakumbatiana kwa pamoja na kila mmoja akaondoka zake
Kwa kamera zilizopo nje ya uwanja wa ndege, nikamuona Victoria akiingia kwenye moja ya gari jeusi na kuondoka huku, mimi na Phidaya tukiwa tumekaa katika sehemu tuliyo kuwa tumekaa na kuondoka pamoja na John.Nikashusha pumzi nyingi, nikapata kumbukumbu za haraka kuhusiana na gari ambalo aliingia Victoria kwani nililiona likiwa kwenye maegesho ya hoteli tuliyo kuwa tumefikizia.
Nikaifunga laptop, na katikti yake nikaweka noti tatu za dola mia mia, ili kukamilisha malipo ya dola mia tano, kutokana tayari nilisha mlipa dola mia mbili kama utangulizi wa kazi, nikarudi na kumkuta akiwa ananisubiri.Nikakaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia, wakaingia askari wawili ndani ya ukumbi tuliopo, wakatutizama kwa umakini mimi na muhudumu na kuanza kupiga hatua za kuja sehemu tulipo kaa
Nikastukia kumuona muhudumu akinishika mashavu yangu, akaanzak kuinyonya midomo yangu, huku macho yake yakiwatazama askari wanao karibia kufika kwenye meza yetu
"Mmgghhh"
Askari mmoja aliguna na kumfanya muhudumu huyo kuniachia taratibu, akatabasamu na kuwafanya askari hao watabasamu, akazungumza nao kizulu
"Sizibuna ukuthi kungani muna?"(Mbona munatabasamu?)
"Sibona lapho nabasekweni"(Tunaona upon na shemeji)
"Yebo, nabasemzini zakho lokhu"(Ndio shemeji yenu huyu)
"Siyakubongela thina kudlule"(Hongera sisi tunapita)
"Esizayo efanayo"(Sawa baadaye)
Askari wakaondoka na ku kutuacha sisi tukiwatazama
"Haita jirudia tena"
Muhudumu alizungumza huhu akijifuta mdomo wake, kwa kitambaa
"Pesa yako nimeibananisha katikati ya laptop, asante"
"Sawa"
Nikanyanyuka na kuondoka, nikatoka nje ya uwanja wa ndege na kuingia katika taksi niliyo kuja nayo, nikamuomba dereva anipeleke ilipo hoteli tuliyo fikizia, njia nzima moyo wangu ukawa na maswali mengi kati ya John na Victoria wamejuana vipi
"Ahaaa, ila inaweza kuwa ni mambo ya kidunia"
Nilijisemea mwenyewe na kumfanya dereva taksi kunitazama, tukafika kwenye hoteli, tukasimama kwenye maegesho yamagari, nikashuka kwa bahati nzuri nikaliona gari alilo ondoka nalo Victoria, nikapiga hatua hadi lilipo na kuchungulia kwenye dirisha, lake, sikukuta mtu ndani.Mlio wa mbwa na tochi za walinzi zikanistua, wakaniamuru nisimame kama nilivyo huku mikono yangu nikiinyoosha juu
Wakafika katika sehemu nilipo simama na kunza kunikagua, ila askari mmoja akastuka baada ya kuniona, akawanong'oneza wezake, ambao walikuwa wameninyooshea bunduki zao, wakazishusha chini
"Samahani bwana bosi"
Askari huyo alizungumza huku akijaribu kutengeneza tabasamu la kinafki usoni mwake, huku akionekana kutahayari kwa kitendo walicho nifanyia
"Hii gari ni yanani?"
"Ahaa, hili gari ni la mkurugenzi Victoria"
"Yeye yupo wapi?"
"Alikuja nalo juzi usiku, ila kutokana sikuingia mchana zamu sijajua aliondoka vipi"
Nikajaribu kuuvuta mlango wa gari upende wa dereva na likafunguka.Nikaufunga mlango nikaondoka na kuwaacha walinzi wakiulizana maswali kadhaa, nikafika kwenye chumba cha kurekodia video zote zinazo chukuliwa na kamera za ulinzi.Sikuamini macho yangu baada ya kuwakuta wafanya kazi wawili wa chumba hichi, wakiwa uchi wa mnyama, wakifanya mapenzi na msichana, anaye onekana ni kahaba
*****Ni maamuzi gani Eddy atayachukua juu ya wafanyakazi wa hoteli ya baba yake, ungana nani katika sehemu ya 70 katika simulizi hii*********
ITAENDELEA
 
Duh!! Kweli nimekamatika na hii story si mchezo...
 
Story imeishia hapo, na mtunzi inamchukua 2 to 3 weeks kumaliza episode moja kwa sababu ana story zingine nyingine anatunga. Tulieni zitakuja.
 
Nahisi wewe ndio umejichanganya, pasipo mimi unadhani ungeisoma hiyo story au unaropoka tu, unatambua hatimiliki ya hiyo story nikiamua kumchukulia hatua aliye ipost huku, unadhani anaweza kufurukuta katika sheria, kama hujui chanzo cha kitu wewe kaunsha
Aliyekwambia sisi tunamtafuta mwandishi ni nani?
Mbona unajichanganya ndugu, hapa tunachotaka ni hadithi, nani kaiandika sisi haituhusu
 
Nahisi wewe ndio umejichanganya, pasipo mimi unadhani ungeisoma hiyo story au unaropoka tu, unatambua hatimiliki ya hiyo story nikiamua kumchukulia hatua aliye ipost huku, unadhani anaweza kufurukuta katika sheria, kama hujui chanzo cha kitu wewe kaunsha

Mimi sion sababu ya wewe kukasirika coz umejitangazia jina ,heshima uliyoipata hapa si ya kitoto, Leo tukijua kitabu xhako kinauzwa wapi lazima tununue, we kaka mkali
 
Nahisi wewe ndio umejichanganya, pasipo mimi unadhani ungeisoma hiyo story au unaropoka tu, unatambua hatimiliki ya hiyo story nikiamua kumchukulia hatua aliye ipost huku, unadhani anaweza kufurukuta katika sheria, kama hujui chanzo cha kitu wewe kaunsha
Nakupa pongezi sana Hakika unakipaji
 
Back
Top Bottom