Hotel aliyofikia Lema jijini Dar es Salaam yazingirwa na Polisi, alikuwa aongee na Wanahabari

Hotel aliyofikia Lema jijini Dar es Salaam yazingirwa na Polisi, alikuwa aongee na Wanahabari

Askari wa Polisi wamezingira Hotel aliyofikia Mikocheni, Dar es Salaam, wakimtafuta Waziri Kivuli wa Wizara ya mambo ya ndani na Mbunge wa Arusha mjini kwa sababu ambazo hazijajulikana. Mhe. Lema alikuwa azungumze na vyombo vya habari leo jijini D'Salaam kumjibu DPP

Polisi hao wenye silaha, wasiokuwa na sare za Polisi, wako ndani ya gari na wengine mapokezi ya Hotel ya Regency Park. Wamelazimisha uongozi wa hotel ufungue chumba cha Godbless walivyojibiwa ni kinyume cha taratibu, wamewaonya wafanyakazi iwapo hawatampata Mbunge huyo.

======

Habari za asubuhi? Mkutano wa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema (Mb) na waandishi wa habari, umeahirishwa, hivyo hautafanyika leo, kwa sababu amelazimika kuanza safari kuelekea Singida kwa kupitia Arusha kwa dharura. Tutawataarifu waandishi wa habari siku ambayo Lema atafanya press conference, kuhusu suala hilo. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote. Asante.

Makene
Dunia ya teknolojia hii kurekodi dukuduku lako hakuna ulazima wa kuita waandishi wa habari mbunge anashindwa kuwa na kamera? Ajirekodi hata kwa kamera ya simu avitumie mzigo hivyo vyombo vya habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli polisi hawana mambo mengine ya kufanya zaidi ya kudeal na chadema tu kila
siku, inaboa kishenzi yaani
Ili polisi apande cheo njia rahisi ni kuishambulia chadema
 
Back
Top Bottom