Tetesi: Hotel ya Ryan Bay Mwanza kubomolewa

Futa neno free! Breakfast lunch dinner includsive kwenye 100000 boarding rate!
 
tumeongea sana humu lakini wote hatuna uhakika kama hii Habari ni ya kweli au bado ni tetesi, tunaomba Habari kamili juu ya hili ili tusisugue akili zetu bure
 
Isije ikatokea kama ile issue ya Kituo cha mafuta?
Mpaka MTU anajenga,anakamilisha ujenzi anafungua biashara (Jiji/Wizara ya ardhi, Rahaco,TRA,Maliasili na utalii,) mlikuwa wapi?
Unless kama aliforge documents, lakini anapolipa kodi ya jengo,biashara n.k anatambulika kama nani huko wapi (plot no.....block.....),Je nyaraka zinaonesha nini?
 
I see..such a nice place... and investment.
 
Wanajukwaa kwa masikitiko makubwa, habari zisizo rasmi "tetesi" ni kuwa Hotel ya kitalii ya RYANS BAY iliyopo jijini Mwanza itabomolewa kupita eneo la Reli.

Mwenye habari kamili atuhabarishe...

Sidhani..maana iko mbali na reli bwana.ukitoka kituo cha reli unaenda nyumba nyingine mbele then ndo unafika hotelini hapo na hata upande wa kule ziwani bado iko mbali.pale yataliwa makazi ya Shafik,makaburi ya wahindi,upande wa kiwanda cha Vicfish na ile GBP kituo ya mafuta,matenki ya BP pia na si hiyo Ryans Bay Hotel.
 
Ni kweli jengo limepigwa xxx Bomoa lakini hijajulikana mwisho itakuaje,ni hali ya wasiwasi kwa wafanyakazi na mmiliki.
 
Mimi sishangai maana kipindi cha dhaifu....sheria zilienda likizo. Lakini hata sisi wananchi.....utawekeza kweli hayo mabilioni bila kujiridhisha jamani? Kama alivamia ardhi ya umma aondolewe tuu. Hakuna namna.
 
Hiyo reli itakuwa inaelekea wapi, maana kwa kumbukumbu zangu hotel hii iko pembeni ya stesheni ya reli Mwanza baada ya majengo mengi tu ndo unaifikia. Kutoka pale stesheni kuna reli inayoelekea bandarini maeneo ya Kamanga, sasa reli ya kupita Ryan hotel inaenda wapi? Au ni suala la mazingira maana iko mita chache sana kutoka ziwa Victoria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…