Unachoongea si kweli, ufanisi anaoonesha JPM Tanzania hamna hata kiongozi mmoja wa upinzani mwenye uwezo huo. Tunahitaji viongozi wazuri, hayo mambo ya mfumo ni kujidanganya tu. Angalia nchi kama Malawi, Zambia, Ghana n.k kila siku wanabadili vyama lakini ni masikini wa kutupa.
Nchi kama Botswana inaongozwa na chama kimoja tokea uhuru wake lakini ina maendeleo makubwa. Ukiangalia hao watu wa upinzani kwenye uongozi wa chini hawana cha maana wanachofanya zaidi ya kupiga kelele. Shida yetu Afrika ni viongozi wabaya bila kujali wapo chama gani.
Leo ujidanganye eti Lowassa wa Chadema ni tofauti na Lowassa wa CCM wakati akili yake ni ile ile. Btw, Uhuru anachofanya ni kukopa China na kujenga barabara na reli kitu ambacho hata Ethiopia na nchi nyingine za Afrika wanafanya. Hana ubunifu wowote wa kufanya tuamini ni kiongozi mzuri zaidi ya kuendesha nchi kimazoea.
Wazimu ni yule anayefanya kitu kimoja muda wote na kutegemea matokeo tofauti, bora anayethubutu kujaribisha mapya. Hao Botswana hawana sababu za kubadilisha maana wanaona matokeo mazuri kwa kile wanachkifanya kwa muda wote, wale wa Ghana hongera kwao kwa kujaribu kuthubutu kubadilisha hadi pale watagonga penyewe.
Nyie hapo, mna nchi kubwa yenye kila kitu lakini maskini wa kutupwa miaka yote bado mnatajwa kwenye mataifa ya chini duniani. Halafu bado mnarudia kile kile, kuchagua chama kile kile na kutegemea matokeo tofauti. Sisi tuliishi hivyo, kwa kuwa na chama hicho cha tangu uhuru, lakini ilifika hatua tukaamua liwalo na liwe, tukathubutu na kubadilisha na tangia wakati huwa, hatujajutia hata siku moja. Kama kipindi kile tungemchagua rais Uhuru akiwa kwenye KANU, basi hata nyie pamoja na uzembe wenu mngetupita kiuchumi.
Halafu hilo la mikopo, cha msingi ni matokeo, fahamu kwamba mikopo haitolewi ovyo kwa kila nchi, kuna mengine yakuzingatia. Hujiulizi kwanini Uganda hadi leo bado hawajapewa mkopo wa reli ya SGR, hadi pale Kenya atakubali kuwa mdhamini.
Kuna nchi kama Japan mikopo yao to GDP ni 200%, hivyo sisi kuwa kwenye 50% sio mbaya sana ukizingatia mafanikio ya hio mikopo.
Rasi Uhuru amefanya mengi, tatizo nyie vijana wa Lumumba mnategemea sana taarifa za viblog uchwara mnapoijadili Kenya.
Wakati Uhuru anaingia kwenye uongozi mwaka wa 2013
Shule 8,000 zilikua zimeunga kwenye umeme, leo Uhuru ameongeza idadi na kuwa shule 20,450
Nyumba 2.3m ndio zilikua na umeme, leo hii amefikisha idadi na kuwa 4.1m ina maana zaidi ya Wakenya 50% wameunga
Tulikua na 1,660 megawatts za umeme, amefaulu kuongeza 600 megawatts
Transmission lines zilikua 2,200km ameongeza 600km
Amewapokeza Wakenya 2,322,913 hati miliki za viwanja na mashamba
Bajeti ya elimu ya msingi ilikua 8.96 billion yeye ameongeza hadi 14.1b
Bajeti ya elimu ya sekondari ilikua 19.2 billion ameongeza 32.5b
Ameongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu na kuwa 7.6b kutoka 5.5b
Mfumo wa Huduma Centres ameusambaza nchi yote, awali ilibidi kusafiri sana ili kupata huduma za serikali, leo hii unapata huduma zote ndani ya jengo moja tena wilayani.
Vijana na akina mama na walemavu wamefaulu kufungua biashara 80,000
Yaani kuna mengi nikiamua kuyaandika yote humu nitapoteza muda wa masaa kadhaa ambayo sina kwa sasa, na nina uhakika hayatakuingia maana nyie ni watu wa maajabu sana, kile mlikaririshwa na kuaminishwa ndio huwa mnakomaa nacho hadi kuzimu. Mnafanana na wale hujilipua kwa mabomu, huwezi kuwaambia chochote zaidi ya uzombi wa kujilipua.