Hoteli ya Sugu: Wafanyakazi wa Serikali wanavyoisaliti Serikali ya Magufuli

Hoteli ya Sugu: Wafanyakazi wa Serikali wanavyoisaliti Serikali ya Magufuli

Sugu aliwadharau sana watendaji sasa ajipande kwenye kodi maana hawatamuacha salama ajaiita rais huku analialia kushukuru rais og.

Aliifanya mbeya yake upepo umegeuka atulie sindano iingie
Ukifuata sheria ya kodi hutababaishwa na TRA. Ninavyoamini lakini.
 
Fafa
Miswahili ni mijitu yenye roho mbaya sana. Yaani haitaki yenyewe ifanikiwe, inataka mkose wote, Basi tu wanafurahi sana wote mkiwa mafukara
Fafanua hili la Miswahili...ni watu wa Aina gani Hawa..wanapatikana wapi hapa Tanzania? Wanawakilisha Watanzania wote?!
 
Unaweza kuwa na ukweli fulani , lakini mara kadhaa Magufuli ameshangilia wapinzani kukomolewa .

Kwa Mfano , DC aliyeharibu shamba la kisasa la mboga la Mbowe kule Hai aliyeitwa Byakanwa alipewa bakhshishi ya kupandishwa Cheo na kuwa RC wa Mtwara , Magufuli mwenyewe alimsifia na kumpongeza aliyekuwa Mkurugenzi wa NHC Bilionea Mchechu kwa kuvunjilia mbali Club Billicanas iliyomilikiwa na Mbowe , hili alilifanya wakati akizindua ujenzi wa ghorofa za Magomeni .

Ninazo taarifa kwamba Serikali yenyewe ndio ilipanga njama za kubomoa hotel ya Sugu Mbeya ili kummaliza kiuchumi , maana inafahamika kwamba siku yoyote utakapofanyika uchaguzi huru Sugu anarudi bungeni , sasa baada ya kubaini kwamba hotel ile imejengwa kihalali kwa nyaraka zilizonyooka ndio wakaona kuivunja kutaharibu taswira ya nchi kwa wawekezaji wengine , ndio maana unaona Chalamila kaja na kinachoitwa maagizo ya Rais .

Ninayo mengi sana kuhusiana na njama hii ya Hotel ya Sugu na njama zingine kuwahusu wapinzani na hasa Chadema , ila kwa leo naishia hapa
 
Hili sakata la kutaka kufunga Hoteli ya Sugu huko Mbeya limeleta hisia nyingi.

Lakini baya zaidi ni lile la the dark side ya watu fulani ndani ya Serikali...
Serikali ya Tanzania haitaki wazawa wawe matajiri, hii ni moja ya Sera ya chama tawala tokea enzi za Nyerere.

Ndio maana unaona kila mzawa anayechipukia kuwa tajiri serikali lazima impige figisu kumdhoofisha.

Ila ikiwa mhindi fresh Tu hamna Noma!

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mwezako sugu alikuwa nashukuru rais kuwa yeye amefuata sheria
Magufuli ndiye aliyetaka kuvunja hiyo hotel lakini alipoona anazomewa kila kona akabadilisha nia yake na kumtuma Chalamila apooze hasira za wananchi!
 
Hili sakata la kutaka kufunga Hoteli ya Sugu huko Mbeya limeleta hisia nyingi.

Lakini baya zaidi ni lile la the dark side ya watu fulani ndani ya Serikali.
Serikali inaendeshwa na watu.
Na watu hao maafisa ndiyo waliotaka watumie mgongo wa Serikali kubomoa Hoteli hiyo.

Kwa wafanyabiashara tunajua kuna watu-maafisa, wenye mamlaka na wana wivu, au kinyongo na maendeleo ya wananchi, hasa wafanya biashara.

Nimeambiwa huko Mbeya kuna viongozi wa ajabu sana.
Pengine Magufuli atembelee Mbeya kujionea vioja cha maafisa au viongozi wake.

Miaka ya 2017 uwekezaji wa maparachichi ulitiwa misukosuko.
Mwekezaji mzalendo wa ufugaji samaki kule Tukuyu-Kiwira badala ya Serikali kumtia moyo, kupitia DED wakamfungia mradi karibia miaka miwili bila sababu za msingi.
Waliposikia Magufuli anatembelea Mkoa wa Mbeya, wakamfungulia mradi.

Hili ni kielelezo cha watu ndani ya Serikali wenye roho mbaya, na ni mbaya kwa wawekezaji.

Watu wa aina hii wako wengi na idara tofauti kuanzia ma DED, TRA, NEMC, hata baadhi wakuu wa Wilaya.

Hili sakata la Hoteli ya Sugu ni kielelezo tosha cha Watu wasioitakia mema serikali ya Awamu ya Tano.

Maafisa hawa wana msimamo wa kukomoa wafanyabiashara au wawekezaji.

Serikali kupitia Rais anasema hili, wakati baadhi ya maafisa wa Serikali wanatekeleza matakwa yao.

Rais Magufuli kwa kweli inabidi aelezwe tu kwamba kuna wafanyakazi/maofisa ndani ya Serikali yake wanamhujumu.
Wanaiga tabia yake
 
Mkuu una roho ya korosho na uko narrow minded.
Mimi simtetei Sugu kama Sugu kwa vile mimi si mwanasiasa wala wa chama chake.

Wewe una roho ya kukomoana, kisasi kilichondani yako kitakuangamiza mwenyewe.
Mtanzania mwenzako akiwekeza, feel proud na uone unavyoweza kumsaidia katika matatizo yaayo kabili.
Kupigwa mada mradi wako hakukuongezei shibe wala kipato.
Roho yako mbaya ndio itaridhika na kuchekelea, cheza na shetani, atakumaliza muda ukifika.
Hao ndio wanaowaabudu weupe na kukandamiza weusi wenzake.Nakumbuka marehemu Mengi aliandamwa sana weusi wenzake hawakupenda awe tajiri!
 
Hii mechi iko halftime tu, huko mbele yatakuwa makubwa zaidi, tabia ya panya huuma na kupuliza.

Sugu angekuwa na akili kubwa apauze tu, akawekeze kwingine.
Kweli nyoka anauguza kidonda akipona atakuja na hasira,naunga mkono auze huu utawala sio.
 
Hao ndio wanaowaabudu weupe na kukandamiza weusi wenzake.Nakumbuka marehemu Mengi aliandamwa sana weusi wenzake hawakupenda awe tajiri!
Tuwataje kwa majina waliomuandama Mengi.
Na je wao wametajirika?
 
Roho mbaya inaanzia kwake . kumbuka aliwahi kuapa kuwa atahakikisha matajiri watageuka kuwa mashetani.
Huu nao ni ujinga mwingine unaoishushia JF heshima yake. Kauli ya rais ilikuwa very specific ni watu gani aliwalenga. Ingekuwa general kihivyo asingefanya vitendo kama vipe kumpa Bakhresa shamba la ekari elf 10 bure. Hizi ID za kificho zinatoa uhuru watu kupost ujinga.
 
Back
Top Bottom