Hotels za Tanga acheni huu upuuzi, mnatia kichefuchefu


Zanzibar kuna hotels hawaweki ndala wala mswaki πŸ€”πŸ€”

Nilichokaje?

Hotel ya shilingi 150,000/- kwa usiku mmoja.

Hakuna kandambili wala mswaki na dawa ya meno.

Na wako na amani wala hawajistukii hata kidogo,
Sijui jamaa wako na matatizo gani aisee.
 
Wale jamaa ndo hovyo sana. Hata suala la usafi kwao ni gumu na Hotels zao ni ghali sana.
 
Watakuja washamba watakuambia hiyo ni ya 15,000 umeongeza sifuri moja. Ni sababu hawajawa na exposures ya haya mambo.
 
Unaweza kuwa umelipa 120,000 KWA usiku ila uliyeenda naye anaweza kuwa ana njaa ya ndala za 3,000.
Sure, nililipa 35k tu..ila niliyekua nae aliondoka na miswaki miwili na baadhi ya vitu..

Alikuja kuniambia, nilivipenda nikaondoka navyo,na akakazia kabisa hata wahudumu lazima wahisi ni mimi tu mtoto wa kike.

Wanawake wanapenda sana vitu vidogo vidogo.
 
Nilishangaa sana hotel ya laki na nusu nimeenda hakuna dawa ya mswaki, mswaki wala ndala, nilipopiga simu wakasema wao hawatoi hivyo vitu, na ni hotel kubwa tu pale mjini unguja

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 


Hotel za Zanzibar nazi ni bei ghali kuanzia hiyo 80,000/- lakini Hata ndala hakunaga.
Hakuna ndala za kuogea, hakuna mswaki wala Sawa ya meno πŸ‘ŒπŸ‘Œ

Mimi naona tuwe tunazitaja hadharani humu ili wajirekebishe.

Very disappointing
 
Weka majina tafadhali
 
Mkuu angalia hizo sifuri vizuri. 80,000=sio hoteli ya watu wa chini kwa mji Kama Tanga, hata Dar for that matter. Otherwise tutajie jina ya hizo guest house na sehemu zilipo.
Kubali tu ulilala gesti za makorora za elfu nane au za kule Mnyanjani self 12,000.
 
Kuna watu wanaenda hotel na viatu, afu wakifika wavivua wanaanza kutembelea ndala, akienda breakfast anavaa ndala. Akitoka kuzunguka kidogo anavaa ndala.

Mnamaliza ndala za watu ndio maana wanazifanya hivyo.

Jambo la pili; Ni hao mabinti wa kitanga mnao ingia nao guest/hotel. Ni wezi balaa, maana unakuta wewe umelipia hotel afu yeye ametoka kwao bila hata mia. Naishia hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…