Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Rais Samia amesema kuanza sasa ataanza kuteua wachapakazi bila kujali itikadi ya kisiasa katika Serikali yake.

Amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kupokea mabadiliko yatakayoleta Umoja wa Kitaifa.

Huko mbele katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, Mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka Chama kipi yule katoka Chama gani lengo letu ni kujenga umoja wa Watanzania

Bila katiba mpya hakuna issue hapo
 
Sioni jipya hapa.

JPM aliwateua akina Kitila Mkumbo, David Kafulila,Wilbroad Slaa, Julius Mtatiro na Anna Mghwila wakiwa upinzani ! Issue ni kuwa ukishateuliwa inabidi ukubali kutekeleza ilani ya CCM, na hapo ndipo ulipo ugumu kwa vyama vya upinzani; ni ugumu huo unaowalizimisha wateule kuhama vyama baada ya kuteuliwa.
 
Nilicheka sana aliposema jana au juzi, “Mnanitukana sana mitandaoni” halafu hakutoa vitisho vya kuwakamata watu. Akitulia huyu anaweza akafanya mambo makubwa sana kwa nchi yetu na akawa ni kioo cha uongozi si kwa Tanzania na Afrika tu bali dunia nzima.
Huu ushauri Mama nilimpa hapahapa Jukwaani naona huwa anapitia JF yaani.
 
Bado matakwa yetu Watanzania ya kutaka Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi yako pale pale. Hii danganya toto haisitishi matakwa hayo. Zitto ameula Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. [emoji12][emoji12]
Mkuu mbona zitto umempigia kura mapema sana?au ni poti wako?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
🤣🤣🤣🤣🤣hapana asee huyo jamaa ni msaliti mkubwa ila nimeona tangu mama aingie amekuwa akijikomba komba kwa nama yetu.
Mkuu mbona zitto umempigia kura mapema sana?au ni poti wako?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom