Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Rais Samia amesema kuanza sasa ataanza kuteua wachapakazi bila kujali itikadi ya kisiasa katika Serikali yake.

Amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kupokea mabadiliko yatakayoleta Umoja wa Kitaifa.

Huko mbele katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, Mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka Chama kipi yule katoka Chama gani lengo letu ni kujenga umoja wa Watanzania

Halafu uteuzi sio kipimo cha utendaji
 
Napingaje sasa?

Sisi ccm tunaridhia wapinzani wapewe vyeo waache kulia lia
Hahahaha... Umeshageuka mara hii???
Wapinzani hawacheleweshi tena maendeleo?

Nilisema ni suala la muda tu mutamkana Jiwe na siasa zake. Hata miezi 2 haijaisha Umeshamgeuka Mwendazake.
 
Sioni jipya hapa.

JPM aliwateua akina Kitila Mkumbo, David Kafulila,Wilbroad Slaa, Julius Mtatiro na Anna Mghwila wakiwa upinzani ! Issue ni kuwa ukishateuliwa inabidi ukubali kutekeleza ilani ya CCM, na hapo ndipo ulipo ugumu kwa vyama vya upinzani; ni ugumu huo unaowalizimisha wateule kuhama vyama baada ya kuteuliwa.
Kuna muda vyama sio jambo la msingi sana endapo kutakua na uhuru na mawazo huru ya hao walioteuliwa kuruhusiwa kutumia bongo zao sawasawa kwa maslahi ya nchi.Vyama vya upinzani vinakuja kwasababu ya watu kutaka mawazo mbadala na uwezi kua na mawazo mbadala yakasikika au kutekelezeka ukiwa mtu binafsi bila kupia chama.Hao walioteuliwa uko nyuma inawezekana kuna mapungufu yaliyowabana wakashindwa kudeliver kile ambacho kilitazamiwa kwahiyo inawezeksna namba moja atakuja na mwarubaini wa wote wanaopata hizo nafasi kuziwajibikia nasio kuishia kufanya sherehe badala ya kazi.
 
Lisu muongo sana afai kuwa mwanasheria,alisema kuna TISS kafa kwa Corona kumbe ni uwongo mtupu.
Umesahau waziri mkuu alidanganya taifa kuwa marehemu dikiteta magufuli tu bukheri na afya njema, kumbe tayari alikuwa keshang'ata shuka?
 
Hahahaha... Umeshageuka mara hii???
Wapinzani hawacheleweshi tena maendeleo?

Nilisema ni suala la muda tu mutamkana Jiwe na siasa zake. Hata miezi 2 haijaisha Umeshamgeuka Mwendazake.
Jiwe tumemkanaje?

Slaa, Mgwira, Kitila, Mtatiro, Kafulila wote hao waliteuliwa na jiwe enzi zake..
 
Rais Samia amesema kuanza sasa ataanza kuteua wachapakazi bila kujali itikadi ya kisiasa katika Serikali yake.

Amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kupokea mabadiliko yatakayoleta Umoja wa Kitaifa.

Huko mbele katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, Mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka Chama kipi yule katoka Chama gani lengo letu ni kujenga umoja wa Watanzania

1620411362444.png

Gharama za kuprint haya mabango si za lazima, yanatumika kwa dakika tu na kupoteza milions of coins
 
Nilicheka sana aliposema jana au juzi, “Mnanitukana sana mitandaoni” halafu hakutoa vitisho vya kuwakamata watu. Akitulia huyu anaweza akafanya mambo makubwa sana kwa nchi yetu na akawa ni kioo cha uongozi si kwa Tanzania na Afrika tu bali dunia nzima.
Tuzo ya utawala bora ya MO IBRAHIM atakuja kubeba asubuhi tu!
 
Back
Top Bottom