Nilipokua nafuatilia bunge juzi mwenyekiti wa bunge alimpa nafasi waziri wa nchi sera uratibu na bunge ndg Lukuvi nafasi ya alichokiita kujibu alichosema prof Limbumpa baada ya hicho alichokiita majibu kwa Lipumba, mh Lukuvi alimsifia sana Mrema kwa mchango wake uliomfurahisha bila shaka na kuwafurahisha wakubwa wa ccm mpaka akafikia kumuahidi kwamba atahakikisha Mrema anapata mafao yak...e ,maswali ya kujiuliza
1. je ni haki ya Mrema kupata hicho Lukuvi anachookiita mafao au ni rushwa baada ya kuwafurahisha kwa mchango wake bungeni
2.kama ni haki yake inahitaji kujipendekeza kwao ndio upate haki yako?
3. hii inatufundisha nini kwamba mpaka tujipendekeze kwa ccm ndio tunaweza kupata haki yetu?
4. kwanini Watanzania tunaruhusu mambo ya kijinga haya yatokee katika nchi yetu kwanini tunaruhusu waziri atumie ofisi ya umma na rasilimali za umma kwa manufaa ya chama chao na serikali iliyoko madarakani
5.ni wangapi wataanza kujipendekeza kwa ccm na serikali yake ili wapate wanachokitaka je tutajenga demokrasia kwa njia hizi?
inakera sana[/QUOTE
Huo ni uthibitisho mwingine, usio na mashaka yoyote kuwa suala la mafungamano ya rushwa na CCM ni sawasawa na mafungamano ya mgonjwa aliyezidiwa na uji.
Kama ambavyo mgonjwa aliyezidiwa, anavyoutegemea uji umsogezee maisha yake, ndivyo hivyo hivyo kwa CCM, ambapo kinga yao peke yake inayowafanya waendelee kuwa madarakani kwa sasa, ni kutoa rushwa!!
Jaribu ku-imagine, Augustine Lyatonga Mrema, alikuwa Naibu Waziri mkuu, wakati wa utawala wa awamu ya pili, wa Rais Ali Hassan Mwinyi. Sasa kama kweli nafasi hiyo ya Naibu waziri mkuu, ilikuwepo kwa mujibu wa katiba yetu,mafao hayo Mrema, angeshalipwa siku nyingi.Ilikuwaje Mrema asilipwe mafao hayo, ambapo sasa ni zaidi ya miaka 20 imepita?!!
Alichosema Lukuvi, ambacho ndicho kinachoweza kufanyika, ni kwa Lukuvi kupeleka ombi 'maalum' hazina, ambako Waziri wake mdogo, ni kada mkubwa sana wa CCM, Mwigulu Nchemba, na kuziomba pesa hizo za walipa kodi 'zichotwe' ili 'azawadiwe' Augustino Lyatonga Mrema, kwa kazi nzuri ya 'kutukuka' aliyoifanya ya kuwasaliti Ukawa wenzake, na kubaki na kundi la Intarahamwe, ndani ya bunge la katiba!!
Ndiyo maana kipindi hiki, viwanda vya kuchapisha T/Shirt, Khanga na Vitenge,vinajiaandaa kwa msimu wao wa mavuno ya kupindukia, kwa kupata Tender nono nono toka CCM, ili Fulana, Khanga na Vitenge hivyo visambazwe na kugawiwa bure kwa mamilioni ya watanzania, kwa lengo moja tu, la kuibakisha CCM madarakani!
Ndiyo maana nimesema siku CCM watakapoacha kutoa rushwa kwa wananchi, ndiyo itakuwa mwisho wa wao kutawala,hiyo ni sawasawa, kama vile mgonjwa, ambaye ameandikiwa na daktari 'diet' ya uji, ambapo mgonjwa huyo, ataamua kukaidi na kuususa uji huo, ndiyo siku itakayokuwa mwisho wa kuishi duniani, ambapo atakata roho!!!