Monduli sio Longido tafadhali!
Kati ya hotuba nzuri zilizojaa busara, ujasiri, ukweli na weledi wa kisiasa basi ni hii ya leo kule Monduli ambapo Mheshimiwa Freeman Mbowe amezungumza juu ya ukweli wa maisha ya kisiasa ya hayati Lowassa.
Hotuba hii iliyojaa ujasiri na umahiri mkubwa imegusa watu wengi na kujikuta wakipiga makofi mengi kwa Mh Mbowe. Mbowe amemtaja Lowassa kama mgombea urais wa CHADEMA aliyeipaisha demokrasia ya nchi na kuwaweka wapinzani katika ramani mpya ya siasa, kuwezesha wabunge zaidi ya 120 wa upinzani na madiwani zaidi ya 2,000 kutoka upinzani ikiwa ni karibu nusu ya madiwani wote nchini.
Mbele ya rais Samia na viongozi wakubwa kote nchini, Mbowe amehoji kwanini ukweli huu unafichwa? Huu ni unafiki wa kisiasa na Mbowe ameonekana kusikitishwa na kukasirishwa na unafiq huu mkubwa. Mbowe amemtaja Lowassa kama mhanga wa mifumo hovyo ya kidemokrasia nchini.
Hongera sana Freeman Mbowe kwa ujasiri huu!