Hotuba ya Mbowe, ni dawa ya kutibu misuli ya moyo

Hotuba ya Mbowe, ni dawa ya kutibu misuli ya moyo

NIMERUDIA kuisikiliza Hotuba ya Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mara kadhaa! Hii ni hotuba inaweza kudumu kwa muda mrefu sana kama rejea sahihi ya maamuzi sahihi yaliyowahi kufanywa na Chadema, tangu mfumo huu wa vyama vingi uanze.

Hotuba ya Mbowe, ni dawa ya kutibu misuli ya moyo! Katika siasa maamuzi mazuri yanayochelewa, ni mabaya zaidi kuliko maamuzi mabaya yanayokuja kwa wakati.

Katika siasa muda na nyakati ni muhimu zaidi kuliko tukio lenyewe. Maamuzi ya haraka ni ishara ya kudhibiti mipango miovu iliyotegwa kwa muda mrefu na wajanja wachache! Naipongeza Chadema kwa kuruka kihunzi hicho kilichokuwa kimetegwa.

Ieleweke kuwa katika siasa hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya! Matukio yote hupangwa. Na nyakati nyingine, huandaliwa mazingira fulani ili kuharakisha tukio jingine kutokea! HONGERENI Chadema kwa kuvunja mpangilio wa matukio mengine yaliyokuwa yamepangwa kutokea ndani ya wiki hii inayoanza!

Chadema wamefanya maamuzi ambayo hata sisi ndani ya CCM hatuwezi kuyafanya! Tumekwisha kupoteza uhalali wa kufanya maamuzi kama yaliyofanywa na Chadema siku nyingi sana.

Chama chetu kiliwahi kuwa na uwezo na jeuri hiyo zama za Mwalimu Nyerere. Baada ya Mwalimu Nyerere, kutangulia mbele za haki, Chama chetu kilipoteza kila kitu:

Mosi, tulipoteza Baba wa Taifa. Nimeambiwa kwa sasa tumebakiza "Mashangazi" wa Taifa.

Pili, tulipoteza Mzee mwenye busara na hekima, mwenye uwezo wa kukemea hadharani bila kificho na mwenye uwezo wa ushawishi na maono!

Kwa sasa hatuna mwanasiasa mshawishi ndani ya umma anayetokana na CCM.

Nje ya CCM wapo. Ukitaka mwanasiasa jasiri, mwenye ushawishi na NGUVU ya hoja mtafute Tundu Antipas Lisu.

Ukitaka mwanasiasa mwenye uwezo wa kuvumilia na usikivu uliovuka mipaka ya kawaida na aliyevuka mipaka ya kuwa mwasiasa na sasa ni mwanasiasa taasisi, mtafute MAALIM SEIF Sharrif Hamad.

Ukitaka mwanasiasa mwenye nguvu ya uchambuzi, mtafute Zitto Kabwe.

Ukitaka mwanasiasa mwenye nguvu ya maono, mtulivu wa hoja na mwenye uwezo mkubwa wa kuwasilisha hoja zake kwa umma mtafute Freeman Mbowe!

Mbowe, ni mwanasiasa mwenye nguvu ya maono. Ukimsikiliza utanielewa kile nichozungumza hapa! Hawa ni wanasiasa wachache sana Taifa limewahi kuwa nao! Kuna kipindi ni natamani angelikuwa CCM ili aweze kuziba ombwe linalotukabili kwa sasa!

Huku kwetu CCM, MUNGU wetu ni mkarimu. Ameumba watu wa aina mbalimbali. Wakiishaumbwa, hatuwezi kuwaumba tena! Tunachoweza ni kuishi nao katika hali tusiyoweza kuibadili!

WANA-CCM wenzangu, tuendelee kuisikiliza Hotuba ya Mh. Mbowe, ni dawa ya misuli ya moyo.

Ndimi Mkukima wa Bamia, Bonde la mto Simiyu-Magu,Mwanza.
Mkuu kunywa bia nitakuja kulipa.
 
Maana hotuba za upande mwingine ni zile Nileteeeeni......, Nileteeeeeeeni........ Nileteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeni... Gwa....... hadi muda unakwisha
Nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuuuuuuuuu?MNIOMBEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
 
Baada ya kusikiliza kile kilichoitwa maamuzi ya kikao cha kamati kuu haya ndiyo nimejionea.

1.Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum.!

2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao.!

3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la chadema.!

4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!

Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?

Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?

Mbona Zito Kabwe na Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa hawakupewa nafasi ya kuomba radhi na kurudishiwa uanachama wao?

Hapa kuna sinema inachezwa na ndani ya siku 30 tutaona matokeo yake, kama mtu alikuwa tayari kutengeneza igizo la kuangushwa na konyagi na kisha kusingizia wasiojulikana, hapa kuna mengi yanakuja.
Hayo uliyoyabainisha ni kweli ndiyo yalikuwa msingi wa matokeo yaliyotokea. Lakini yafaa ujue pia kuwa, kwa kufuata msingi wa Katiba na Kanuni za CHADEMA watuhumiwa walikuwa na haki zote za kujieleza na kutetea njia/mbinu walizotumia hadi kupata hizo zinazoitwa nyaraka za chama za kuthibitisha kuchaguliwa kwao. Aidha, wameogopa kutoea kwa kujua Kuwa watabanwa hadi watoe siri iliyotumika hadi wafike walipofika.
Hoja ya wewe kusema eti ni drama haina msingi wala uhai!
 
Back
Top Bottom