Hotuba ya Rais Magufuli Mei 17, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Hotuba ya Rais Magufuli Mei 17, akili za kuambiwa changanya na za kwako

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada itifaki yote imezingatiwa.

Hapo jana huko Chatto mheshimiwa akitujia mubashara tokea kanisani, mbona ametuachia mengi fikirishi? Yeye mwenyewe aliurejea ule usemi maarufu wa mzee wa msoga kuwa, "akili ya kuambiwa changanya na ya kwako."

Tokea Chatto mheshimiwa alisema yafuatayo:

1. "Lockdown ni utumwa. Kama ningetangaza lockdown ingewafanya watu hata kutoonana na wake zao au hata watoto wao ndani ya nyumba moja. Lockdown ingewafanya watu wasiende hata kuchimba viazi vyao shambani, kununua vitu sokoni na hata kuvua samaki ziwani."

Akaendelea, "mzee Museveni katuuzia tani 25,000 za sukari. Kungekuwa na lockdown sukari hii isingeweza kuja."

Akili hii ya kuambiwa changanya na ya kwako. Lockdown ya namna gani hii? Huyu mzee kweli hajui kwenye lockdown kunakuwa vipi? Upotoshaji huu ni kwa maslahi gani?

2. "Mwanangu mwenyewe wa kuzaa aliugua Corona. Katumia malimao na kujifukiza tu. Amepona kabisa na hivi sasa yuko kwenye kupiga push up."

Changanya na za kwako. Huyu mgonjwa kaugua lini na kapata ugonjwa akiwa wapi? Vipimo vya wapi viligundua Corona hiyo na pia kuhakiki kutokuwepo kwa corona hiyo baada ya kupona?

3. "Wagonjwa wa Corona wamepungua sana hata nafikiria kufungua mashule na ligi kuanza tena. Fikiria mtu anatoka Dar na lori la mzigo anakutwa na Corona Namanga au Rwanda. Huu ugonjwa tunaweza kuishi nao, tuchape kazi tu."

Changanya na za kwako. Hivi takwimu za ugonjwa zinazoonyesha watu wangapi wamepimwa katika muda gani, waathirika wangapi wamepatikana kwenye muda huo, vifo vingapi, quarantine wapo wangapi, wanaofuatiliwa ni wangapi? Inaweza kuwakilishwa kweli na hii jitihada ya kuwaondoa watu mahospitalini wakaugulie majumbani kwao kama kiwakilishi cha hali ya ugonjwa huu nchini kwa sasa?

Je hawa ambao hawakuzuiwa kwenye isolation wanaendelea kuambukiza wangapi wengine?

Vipi hawa wenye pumu, matatizo ya moyo, kisukari, wazee, wenye seli mundu, nk, wanalindwa vipi dhidi ya hao wenye maambukizi walio huru huku mitaani?

4. "Ndege za kuleta watalii zimejaa na ziko fully booked hadi October. Tena wanapokuja hakuna hata haja ya kuwaweka quarantine. Acha waende moja kwa moja wakaji Coronize huko huko."

Changanya na akili yako. Mataifa mbali mbali yanachukua raia wao kuondoka hapa nchini na maonyo juu kuhusiana na hali yetu ya Corona ilivyo. Ndege hizo zilizojaa watalii kuja kwetu katika kipindi hiki ni za kutoka wapi? Spika wa bunge Ndugai pia kathibitisha hili kuwa katika kipindi hiki hakuna watalii wanaokwenda popote.

5. "Kuna mtu humu ndani kavaa barakoa? Mabarakoa ya nini? Mabarakoa hayahitajiki kwenye kupambana na huu ugonjwa!"

Changanya na za kwako. Umuhimu wa kuvaa barakoa umesisitizwa kila mahali, nchi zote achilia mbali WHO wamekuwa wakisisitiza mabarakoa mtu anapokuwa nje mitaani.

Kwa mujibu wake tupete tu mitaani, kwenye maferi, madaladala, nk kwa raha zetu, hakuna haja ya barakoa. China kulikoanzia ugonjwa huu, ni kosa kubwa la kisheria mtu kuonekana mitaani bila ya kuvaa barakoa.

6. "Kwa nini kupima maiti Corona? Si huyo keshakufa? Vifo vyote vishughulikiwe sawa kama vile vifo vya malaria, TB, ajali, nk. Watu wazike ndugu zao kama kawaida, kama vile wanavyofanya na vifo vya magonjwa mengine na wa Corona wafanye hivyo hivyo!"

Changanya na za kwako. Kufahamu sababu ya kifo si muhimu kwa mzee baba. Kuwa marehemu anaweza kuambukiza hata ambao hawajaathirika bado na hata kama ni jamii nzima, si suala kwa mzee baba.

7. "Pana madaktari na manesi waliwekwa quarantine kwa kuwa walikuwa wamekutana na wagonjwa wenye Corona." Akaendelea, "nikaamrisha watoke quarantine kwani kazi zao ni kukutana na wagonjwa wa Corona. Hivyo kuwa walikuwa wamekutana na wenye Corona, hakuna jipya hapo."

Changanya na za kwako. Wauguzi hawa wana ndugu zao na wanawahudumia wagonjwa wengine pia. Kukaidi hatua za kujikinga kinyume na taratibu za kitaalamu zinazohitajika kuwahami wengine kama hivi, ni kwa maslahi yapi? Je, ni watu wangapi wamepata maambukizi ambayo yangeweza kuepukika kwenye mazingira kama haya?

8. "Uchumi? Linapokuja suala la uchumi hilo ni priority. Si jambo jingine lolote lile." Akaendelea, "tuna stigglers gorge, SGR na miradi mingi mingine mikubwa. Hii inaajiri maelfu ya watanzania. Hii haiwezi kusimama. Never!".

Changanya na za kwako. Mzee baba maisha ya watu si kitu kwake. Haipo huruma na maisha ya watu hayana thamani yoyote. Imejengeka kichwani mwake kuwa hana la kufanya kuhami maisha ya raia wake dhidi ya anayotaka kutuaminisha ni mapenzi au maamuzi ya Mungu. Kweli hakuna haja ya kupambana vya kutosha ila tuyasabirie maisha kama hivyo kwa vigezo kuwa Mungu ndiye aliye panga?

Hii ni kinyume na kinachotokea katika mataifa mengine yanayotambua umuhimu wa kuhami maisha kwanza ili ikibidi kuokoa au kufufua uchumi baadaye.

9. "Waache waji lockdown maana ugonjwa ukisha pita watakuwa soko letu la vyakula."

Changanya na za kwako. Kwanini mzee baba haoni kuwa wenzetu wanaweza kuwa hai kwa kujihami kwao kipindi ambacho sisi tunaweza kuwa wafu wakati ugonjwa huo ukiwa ume kwisha? Kwa nini mzee baba yeye anadhani ugonjwa huu unawahusu wengine tu na kwenye janga hili sisi hatumo wala halituhusu?

10. Nk nk.

Hotuba ile ina mengi ya namna hii.

Wako wapi maswaiba wa mzee baba? Hawa kina Mbatia (wazee wa SMS) na wazee wetu marais wastaafu, wazee wenye umri wao (bila kujali vyama vyao), viongozi wa dini, nk, kumshauri?

Yapo mengi yanayoonyesha kutuunganisha sote kabisa katika umoja wetu wa kizalendo kabisa kama watanzania. Mfano wa haya ni kama:

1. Taarifa za kuzuiwa malori ya kigeni Kilimanjaro.
2. Kusimama imara kukataa unyanywasaji kwa madereva wetu wa malori mipakani.
3. Uamuzi wa kufunga anga kipindi anga la Tanzania lilipofungwa ili kuzuia maambukizi tokea nje ya nchi, japo ilikuwa ni kwa kuchelewa mno.
4. Nk, nk.

Hata ushughulikiwaji wa suala la ugonjwa huu, lingeweza likafanyika katika namna muafaka zaidi ambayo ingeweza kutuunganisha sote dhidi ya ugonjwa huu, na kweli tukaushinda.

Rais Magufuli, pamoja na Corona unayo nafasi ya kuiunganisha nchi - JamiiForums

Nawasilisha.
 
Hivi wee Magufuli, Wagonjwa wa corona wamepungua au wamepunguzwa? Maambukizi ya Corona yamepungua au mnakwepa kupima? Vifo vimepungua au mnaficha?

Ni dhambi kutaja jina la Mungu kushuhudia uongo tena ukiwa kanisani.
Toeni taarifa za kweli umma ujilinde.
 
Mkuu sidhani Kama huyu mtu anahitaji kushauriwa.Huyu anahitaji kungolewa na corona ili akasimamie hiyo miradi yake akiwa kaburini huko

Kwa hakika huyu bwana anasononesha.

Eti kuwa shule na ligi anafikiria kuzifungua. Shule na ligi ipi? Kwa takwimu zipi?

Yale yale ya uchaguzi mkuu. Ooh uchaguzi mkuu uko pale pale. Wapi? Umemsikia akiuongelea tena?

Haipo shule wala ligi inafunguliwa karibuni. Pana ushahidi zaidi ya kiwango cha maambukizi kuliko kinachopatikana kwa madereva wa malori mipakani?

Fumbo wamfumbie mjinga.
 
Hili ndio linaonesha tuna rais wa namba gani:

4. "Ndege za kuleta watalii zimejaa na ziko fully booked hadi October. Tena wanapokuja hakuna hata haja ya kuwaweka quarantine. Acha waende moja kwa moja wakaji Coronize huko huko." -HE John Pombe Magufuli.
 
Hili ndio linaonesha tuna rais wa namba gani:

4. "Ndege za kuleta watalii zimejaa na ziko fully booked hadi October. Tena wanapokuja hakuna hata haja ya kuwaweka quarantine. Acha waende moja kwa moja wakaji Coronize huko huko." -HE John Pombe Magufuli.

Tulipokuwa shule za msingi kwenye hisabati kulikuwa na alama inaitwa "kubwa kuliko" yaani " > ".

Kazi kweli kweli.
 
"Coronize" possible meaning please.

Sent using Jamii Forums mobile app

This is a new English word by mzee baba possibly intended to mean - "spread or catch the Corona virus as you wish or at your own will".

In Swahili it would possibly be "sambaza au jipatie virusi vya Corona kwa raha zako".

We have a long way to go.
 
Mtoa mada wewe kiazi kweli!!

Hebu nenda kamwambie mr chsir wabunge watakavyomkimbia,

Mmeshindwa kujiongeza na kuchanganya AKILI zenu huko chadema mtaweza kuchanganya AKILI za kumuelewa Jpm kweli?????

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jiweke kwenye nafasi ya watu waliopoteza wapendwa wao, wanaendelea kupoteza wapendwa wao na watakaoendelea kupoteza wapendwa wao.

Jiweke kwenye nafasi ya wazee au watu wenye matatizo yoyote yale ya afya kama ya moyo, pumu, seli mundu, figo, cancer, ukimwi, kisukari, malaria, nk. Kimsingi kwa misimamo ya mzee baba tayari ameshasaini hati zao za vifo. Hii bila ya yeye kuwa Sub-hana w-ata Allah. Bali kinunda nunda kuwatanguliza wao akhera.

Kwa hakika mkururo wa watu wote hao hauwezi kuwa na maneno mazuri sana kwa mzee baba. Ambaye yeye kwa takribani miezi miwili sasa ameji barricade kwenye ngome yake Chatto.
 
Mtoa mada wewe kiazi kweli!!

Hebu nenda kamwambie mr chsir wabunge watakavyomkimbia,

Mmeshindwa kujiongeza na kuchanganya AKILI zenu huko chadema mtaweza kuchanganya AKILI za kumuelewa Jpm kweli?????

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hii mada imekuwapo hapa tokea jana. Yaonyesha imekugusa vilivyo na bila shaka hukulala usiku.

Mada haina jipya hata moja. Mada ina maneno yote kama yalivyotamkwa na mzee baba. Yote yamenukuliwa katika maana aliyohitaji mzee baba mwenyewe.

Yamekuwia machungu. Umeshindwa kuona uanzie wapi kuyakanusha maana yote ni ya kweli na ndivyo alivyosema na kushauri mzee baba mwenyewe kuwa "tukiambiwa tuchanganye na za kwetu."

Mkuu avatar yako huitendei haki. Picha ya kiazi ingekufaa zaidi. Huyo bwana kwenye picha hiyo (rip) kwa hakika hawezi kufanana na wewe katu!

Mnachojidanganya ni kuwa, kila anayesema ukweli, kwa kuendekeza njaa zenu mnamwona ni CHADEMA. Mbona hata ACT, NCCR, NLD, CUF, CCM, nk, na hata tusiokuwa na vyama tupo?

Hukuwahi kusikia kuwa "wavumao baharini ni papa, lakini na wengine wamo?"

Mkuu kwa hakika kiazi ni wewe, haiwezekani ukawa kitu kingine!
 
Hii hotuba kila mtu ametoka na mtazamo wake.

Mwenye kuiona ya kweli ametoka na mtazamo wake, mwenye kuiona ya uongo ametoka na mtazamo wake, mwenye kuitilia mashaka ametoka na mashaka yake.

Lakini ukweli utabaki palepale.

"akili ya kuambiwa changanya na ya kwako."
 
Hii hotuba kila mtu ametoka na mtazamo wake.

Mwenye kuiona ya kweli ametoka na mtazamo wake, mwenye kuiona ya uongo ametoka na mtazamo wake, mwenye kuitilia mashaka ametoka na mashaka yake.

Lakini ukweli utabaki palepale.

"akili ya kuambiwa changanya na ya kwako."

Mkuu kujaribu kuitafsiri hotuba ile tofauti na mtoa hotuba kama alivyosema ni ukakasi mtupu.

Yaliyopo kwenye bold ndivyo aliyotamka mheshimiwa. Kwa maana ipi tofauti na alivyosema yeye mwenyewe?
 
Back
Top Bottom