Hotuba ya Rais Magufuli Mei 17, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Hotuba ya Rais Magufuli Mei 17, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Ndo mana nasema wakulaumiwa sku zote ni Mzee wa Msoga na Uncle Benja kwa kutuletea Stone.Na kama wanafunz wa Vyuo ndo watandoka kama Maembe sababu weng sna pia wana viugonjwa vya ajabajab na ukichanganya na wale special wanaolelewa kwa hisan ya Ma Salma.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu shule zitafunguliwa maana neno la mzee baba ni sheria.
Kwa hakika huyu bwana anasononesha.

Eti kuwa shule na ligi anafikiria kuzifungua. Shule na ligi ipi? Kwa takwimu zipi?

Yale yale ya uchaguzi mkuu. Ooh uchaguzi mkuu uko pale pale. Wapi? Umemsikia akiuongelea tena?

Haipo shule wala ligi inafunguliwa karibuni. Pana ushahidi zaidi ya kiwango cha maambukizi kuliko kinachopatikana kwa madereva wa malori mipakani?

Fumbo wamfumbie mjinga.
 
Wewe unachotaka nini hasa

Vitu vingine mnajichosha tu, mnamaliza bando

Corona ipo, tutaishi nayo, hata WHO wanajua

Mtu anaugua corona, anapona mwenyewe, anaugua tena, wewe unadhani unaweza kupumbana na ugonjwa wa kijinga kama huo, ni mafua ya kawaida tu

Sasa sijui unabwatuka humu, unataka magufuli afanye nini, mnataka mpige dili kwenye huu ugonjwa wa kusadikika wa wachina et mnapima kumbe ujinga mtupu?

Magu nyoosha haya majinga mpaka yatakapojitambua

Jitu linalilia takwimu ziwe nyingi za wagonjwa, mpaka unajiuliza hili jitu linataka nini?

Sijui lock down ujinga mtupu,

Corona tutaishi nayo, mwenye kufa atakufa na atakatebaki atabaki, nature itaselect.

Mipaka ya ndege imeshafunguliwa, watu wazito wameshashituka na huu upuuzi wa corona, wanakuja Tanzania kutalii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hotuba kila mtu ametoka na mtazamo wake.

Mwenye kuiona ya kweli ametoka na mtazamo wake, mwenye kuiona ya uongo ametoka na mtazamo wake, mwenye kuitilia mashaka ametoka na mashaka yake.

Lakini ukweli utabaki palepale.

"akili ya kuambiwa changanya na ya kwako."
Sure ,na naongeza Mkuu Wa nchi no binadam sio malaika hivyo hawezi Fanya kila kitu sawa yapo ambayo hufanya vizuri na yapo ambayo hufanya pia yasio sawa ,na hapa huwa na mtetea maana wako washauri wake na kazi yao no iyo tu na wanalipwa mshahara.so lazima watimize wajibu wao sio kuogopa kiss kutetea tumbo ,Fanya wajibu wako ukitumbuliwa basi kashone Viatu lakini umetimiza wajibu wako,
Hata hivyo mfano kwa corona kutopiga total lock down nampongeza ila yapo ambayo simpongezi i wish ningepata hata dakika 2 za kuongea nae ningemwabia wazi yapi sikubaliani naye hasa kuhusu corona na siwezi andika hapa.
Mwisho
Mh mteteeni ila wale mnao mtetea kinafiki MUNGU ANAWAONA NA MUNGU AJARIBIWI
 
Mkuu kujaribu kuitafsiri hotuba ile tofauti na mtoa hotuba kama alivyosema ni ukakasi mtupu.

Yaliyopo kwenye bold ndivyo aliyotamka mheshimiwa. Kwa maana ipi tofauti na alivyosema yeye mwenyewe?
Bila ya shaka Mh. alitaka tumuelewe kwa dhahiri ya hotuba yake.

Lakini ulichokiandika wewe ni uliyoyaona kutokana na alichokisema, lakini si kutokana na alichokikusudia/kukimaanisha(yaani dhahiri ya hotuba yake)

Na hii ni baada ya wewe kuchanganya na zako, na si wote ambao watafanya hivyo.

Na hapo ndipo utofauti wa mitazamo unapokuja.
 
Sure ,na naongeza Mkuu Wa nchi no binadam sio malaika hivyo hawezi Fanya kila kitu sawa yapo ambayo hufanya vizuri na yapo ambayo hufanya pia yasio sawa ,na hapa huwa na mtetea maana wako washauri wake na kazi yao no iyo tu na wanalipwa mshahara.so lazima watimize wajibu wao sio kuogopa kiss kutetea tumbo ,Fanya wajibu wako ukitumbuliwa basi kashone Viatu lakini umetimiza wajibu wako,
Hata hivyo mfano kwa corona kutopiga total lock down nampongeza ila yapo ambayo simpongezi i wish ningepata hata dakika 2 za kuongea nae ningemwabia wazi yapi sikubaliani naye hasa kuhusu corona na siwezi andika hapa.
Mwisho
Mh mteteeni ila wale mnao mtetea kinafiki MUNGU ANAWAONA NA MUNGU AJARIBIWI
Sure.
 
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada itifaki yote imezingatiwa.

Hapo jana huko Chatto mheshimiwa akitujia mubashara tokea kanisani, mbona ametuachia mengi fikirishi? Yeye mwenyewe aliurejea ule usemi maarufu wa mzee wa msoga kuwa, "akili ya kuambiwa changanya na ya kwako."

Tokea Chatto mheshimiwa alisema yafuatayo:

1. "Lockdown ni utumwa. Kama ningetangaza lockdown ingewafanya watu hata kutoonana na wake zao au hata watoto wao ndani ya nyumba moja. Lockdown ingewafanya watu wasiende hata kuchimba viazi vyao shambani, kununua vitu sokoni na hata kuvua samaki ziwani."

Akaendelea, "mzee Museveni katuuzia tani 25,000 za sukari. Kungekuwa na lockdown sukari hii isingeweza kuja."

Akili hii ya kuambiwa changanya na ya kwako. Lockdown ya namna gani hii? Huyu mzee kweli hajui kwenye lockdown kunakuwa vipi? Upotoshaji huu ni kwa maslahi gani?

2. "Mwanangu mwenyewe wa kuzaa aliugua Corona. Katumia malimao na kujifukiza tu. Amepona kabisa na hivi sasa yuko kwenye kupiga push up."

Changanya na za kwako. Huyu mgonjwa kaugua lini na kapata ugonjwa akiwa wapi? Vipimo vya wapi viligundua Corona hiyo na pia kuhakiki kutokuwepo kwa corona hiyo baada ya kupona?

3. "Wagonjwa wa Corona wamepungua sana hata nafikiria kufungua mashule na ligi kuanza tena. Fikiria mtu anatoka Dar na lori la mzigo anakutwa na Corona Namanga au Rwanda. Huu ugonjwa tunaweza kuishi nao, tuchape kazi tu."

Changanya na za kwako. Hivi takwimu za ugonjwa zinazoonyesha watu wangapi wamepimwa katika muda gani, waathirika wangapi wamepatikana kwenye muda huo, vifo vingapi, quarantine wapo wangapi, wanaofuatiliwa ni wangapi? Inaweza kuwakilishwa kweli na hii jitihada ya kuwaondoa watu mahospitalini wakaugulie majumbani kwao kama kiwakilishi cha hali ya ugonjwa huu nchini kwa sasa?

Je hawa ambao hawakuzuiwa kwenye isolation wanaendelea kuambukiza wangapi wengine?

Vipi hawa wenye pumu, matatizo ya moyo, kisukari, wazee, wenye seli mundu, nk, wanalindwa vipi dhidi ya hao wenye maambukizi walio huru huku mitaani?

4. "Ndege za kuleta watalii zimejaa na ziko fully booked hadi October. Tena wanapokuja hakuna hata haja ya kuwaweka quarantine. Acha waende moja kwa moja wakaji Coronize huko huko."

Changanya na akili yako. Mataifa mbali mbali yanachukua raia wao kuondoka hapa nchini na maonyo juu kuhusiana na hali yetu ya Corona ilivyo. Ndege hizo zilizojaa watalii kuja kwetu katika kipindi hiki ni za kutoka wapi? Spika wa bunge Ndugai pia kathibitisha hili kuwa katika kipindi hiki hakuna watalii wanaokwenda popote.

5. "Kuna mtu humu ndani kavaa barakoa? Mabarakoa ya nini? Mabarakoa hayahitajiki kwenye kupambana na huu ugonjwa!"

Changanya na za kwako. Umuhimu wa kuvaa barakoa umesisitizwa kila mahali, nchi zote achilia mbali WHO wamekuwa wakisisitiza mabarakoa mtu anapokuwa nje mitaani.

Kwa mujibu wake tupete tu mitaani, kwenye maferi, madaladala, nk kwa raha zetu, hakuna haja ya barakoa. China kulikoanzia ugonjwa huu, ni kosa kubwa la kisheria mtu kuonekana mitaani bila ya kuvaa barakoa.

6. "Kwa nini kupima maiti Corona? Si huyo keshakufa? Vifo vyote vishughulikiwe sawa kama vile vifo vya malaria, TB, ajali, nk. Watu wazike ndugu zao kama kawaida, kama vile wanavyofanya na vifo vya magonjwa mengine na wa Corona wafanye hivyo hivyo!"

Changanya na za kwako. Kufahamu sababu ya kifo si muhimu kwa mzee baba. Kuwa marehemu anaweza kuambukiza hata ambao hawajaathirika bado na hata kama ni jamii nzima, si suala kwa mzee baba.

7. "Pana madaktari na manesi waliwekwa quarantine kwa kuwa walikuwa wamekutana na wagonjwa wenye Corona." Akaendelea, "nikaamrisha watoke quarantine kwani kazi zao ni kukutana na wagonjwa wa Corona. Hivyo kuwa walikuwa wamekutana na wenye Corona, hakuna jipya hapo."

Changanya na za kwako. Wauguzi hawa wana ndugu zao na wanawahudumia wagonjwa wengine pia. Kukaidi hatua za kujikinga kinyume na taratibu za kitaalamu zinazohitajika kuwahami wengine kama hivi, ni kwa maslahi yapi? Je, ni watu wangapi wamepata maambukizi ambayo yangeweza kuepukika kwenye mazingira kama haya?

8. "Uchumi? Linapokuja suala la uchumi hilo ni priority. Si jambo jingine lolote lile." Akaendelea, "tuna stigglers gorge, SGR na miradi mingi mingine mikubwa. Hii inaajiri maelfu ya watanzania. Hii haiwezi kusimama. Never!".

Changanya na za kwako. Mzee baba maisha ya watu si kitu kwake. Haipo huruma na maisha ya watu hayana thamani yoyote. Imejengeka kichwani mwake kuwa hana la kufanya kuhami maisha ya raia wake dhidi ya anayotaka kutuaminisha ni mapenzi au maamuzi ya Mungu. Kweli hakuna haja ya kupambana vya kutosha ila tuyasabirie maisha kama hivyo kwa vigezo kuwa Mungu ndiye aliye panga?

Hii ni kinyume na kinachotokea katika mataifa mengine yanayotambua umuhimu wa kuhami maisha kwanza ili ikibidi kuokoa au kufufua uchumi baadaye.

9. "Waache waji lockdown maana ugonjwa ukisha pita watakuwa soko letu la vyakula."

Changanya na za kwako. Kwanini mzee baba haoni kuwa wenzetu wanaweza kuwa hai kwa kujihami kwao kipindi ambacho sisi tunaweza kuwa wafu wakati ugonjwa huo ukiwa ume kwisha? Kwa nini mzee baba yeye anadhani ugonjwa huu unawahusu wengine tu na kwenye janga hili sisi hatumo wala halituhusu?

10. Nk nk.

Hotuba ile ina mengi ya namna hii.

Wako wapi maswaiba wa mzee baba? Hawa kina Mbatia (wazee wa SMS) na wazee wetu marais wastaafu, wazee wenye umri wao (bila kujali vyama vyao), viongozi wa dini, nk, kumshauri?

Yapo mengi yanayoonyesha kutuunganisha sote kabisa katika umoja wetu wa kizalendo kabisa kama watanzania. Mfano wa haya ni kama:

1. Taarifa za kuzuiwa malori ya kigeni Kilimanjaro.
2. Kusimama imara kukataa unyanywasaji kwa madereva wetu wa malori mipakani.
3. Uamuzi wa kufunga anga kipindi anga la Tanzania lilipofungwa ili kuzuia maambukizi tokea nje ya nchi, japo ilikuwa ni kwa kuchelewa mno.
4. Nk, nk.

Hata ushughulikiwaji wa suala la ugonjwa huu, lingeweza likafanyika katika namna muafaka zaidi ambayo ingeweza kutuunganisha sote dhidi ya ugonjwa huu, na kweli tukaushinda.

Rais Magufuli, pamoja na Corona unayo nafasi ya kuiunganisha nchi - JamiiForums

Nawasilisha.
Upuuzi tu.
 
Wiki ijayo mwendo mdundo, nyie endeleeni kuota na kulazimisha kuwa hali ni mbaya.
 
Kuchanganya na zako bado hakuondoi uhalisia uliopo, Corona bado ipo sana Ila maisha lazima yaendelee na haijalishi kipi kitatokea.


Sent using Jamii Forums mobile app

Haijalishi kipi kitatokea kama hutachukua hatua stahiki hakuhalalishi matokeo yoyote mabaya yanayoweza kutokea katika hali kama hiyo.
 
Hahaha, hakuna hoja ya kujibu hapo.

IMG_20200519_112008_269.jpg
 
Kwa siku za karibuni nimemkubali sana Rais wangu JPM. He is very optimistic.

Tunawahitaji watu wa kaliba hii.

JESUS IS LORD!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu uko nje ya mada. "Akili za kuambiwa changanya na za kwako".

Hata hivyo kukumbusha tu:

Taifa halina dini. Vipi wasiowaumini wa hiyo dini yako nao unawashirikisha je kwenye hilo hitimisho lako?
 
Wiki ijayo mwendo mdundo, nyie endeleeni kuota na kulazimisha kuwa hali ni mbaya.

Sina hakika ni kwa mada ipi unaandika. Mkuu mwendo mdundo wa kuelekea wapi? Kisutu au Kinondoni?
 
Bila ya shaka Mh. alitaka tumuelewe kwa dhahiri ya hotuba yake.

Lakini ulichokiandika wewe ni uliyoyaona kutokana na alichokisema, lakini si kutokana na alichokikusudia/kukimaanisha(yaani dhahiri ya hotuba yake)

Na hii ni baada ya wewe kuchanganya na zako, na si wote ambao watafanya hivyo.

Na hapo ndipo utofauti wa mitazamo unapokuja.

Mkuu niliandika " ........ ametuachia mengi fikirishi".

Akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Yote niliyoandika (yote) aliyatamka. Hakuna aliyekanusha wala kufafanua vinginevyo.

Ninaamini kama kungekuwa na tafsiri zingine zingewekwa humu.

Ninadhani "JF is where we dare air our views openly."

Inahitaji kuvaa miwani ya mbao kutokukiona kigugimizi hicho.
 
Hili ndio linaonesha tuna rais wa namba gani:

4. "Ndege za kuleta watalii zimejaa na ziko fully booked hadi October. Tena wanapokuja hakuna hata haja ya kuwaweka quarantine. Acha waende moja kwa moja wakaji Coronize huko huko." -HE John Pombe Magufuli.
Sijui hata alimaanisha nn , inawezekana na wabongo tunaendelea kujcoronize .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unachotaka nini hasa

Vitu vingine mnajichosha tu, mnamaliza bando

Corona ipo, tutaishi nayo, hata WHO wanajua

Mtu anaugua corona, anapona mwenyewe, anaugua tena, wewe unadhani unaweza kupumbana na ugonjwa wa kijinga kama huo, ni mafua ya kawaida tu

Sasa sijui unabwatuka humu, unataka magufuli afanye nini, mnataka mpige dili kwenye huu ugonjwa wa kusadikika wa wachina et mnapima kumbe ujinga mtupu?

Magu nyoosha haya majinga mpaka yatakapojitambua

Jitu linalilia takwimu ziwe nyingi za wagonjwa, mpaka unajiuliza hili jitu linataka nini?

Sijui lock down ujinga mtupu,

Corona tutaishi nayo, mwenye kufa atakufa na atakatebaki atabaki, nature itaselect.

Mipaka ya ndege imeshafunguliwa, watu wazito wameshashituka na huu upuuzi wa corona, wanakuja Tanzania kutalii

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu mimi nitake au nitake Magufuli afanye nini? Mada mbona iko wazi. Nini kamili alisema na nini alitushauri kufanya - yaani kuchanganya na za kwetu. Nothing more, nothing less!

Mbona povu jingi namna hiyo?

Hukupenda alichokisema au ushauri aliotoa au wengine kuutumia ushauri wake kikamilifu?

Grow up buddy!

Mtu kuugua Corona akapona halikupi taabu. Je anaambukiza wangapi ambao labda hawatapona ina maana yoyote kwako?

Umeona wapi kilio cha takwimu kwenye bandiko langu ku merit msisitizo mkubwa kiasi hicho ulichotoa wewe kuhusu hilo?

Inaonyesha unajua umuhimu wa takwimu sahihi vilivyo kwenye kupambana na ugonjwa huu. Kwa nini mnachagua kuwa kwenye state of denial wakati kumbe vya muhimu mnavijua?

WHO inasema tujifunze kuishi na ugonjwa huu. Unataka kumwaminisha nani kuwa ni kwa njia fyongo kama hizi tunazoziona hapa? Anayowaambia WHO mnayazingatia kikamilifu? Au yale tu yanayowapa marriages uchwara za convenience?

Unayebwatuka ni wewe ambaye bila ya shaka ndiyo jitu. Nilichoandika chote kiko wazi kwa source na hata kwa essence.

Matusi mengine uliyotumia yanakuhusu wewe zaidi. Nikiyatumia hayo kwangu itakuwa kujidhalilisha kwa kujifananisha na wewe.

Hoja hujibiwa kwa hoja. Matusi ni dalili chanya kabisa za kukosa hoja.
 
Back
Top Bottom