Hotuba ya Tundu Lissu Februari 5, 2023 ina viwango vya kimataifa, ina Takwimu na Facts - haina Propaganda!

Hotuba ya Tundu Lissu Februari 5, 2023 ina viwango vya kimataifa, ina Takwimu na Facts - haina Propaganda!

Hahahaha pro_pesa Kalamaganda Kabugi amjibu TAL?! Wapi na wapi kama sio atatoa mimacho yake kama chura kabanwa na mlango tu na viswahili Uchwara "mia kenda....."!

Sent from my Nokia G21 using JamiiForums mobile app
Hivi Ccm kumebaki na kichwa hata kimoja cha kujibu hoja?
 
Kwahiyo Lisu amekuja Tanzania ametoa hutuba yenye viwango Kisha amerudi kwao si ndiyo

Chadema imeshakufa kifo Cha kawaida
 
Ukifuata mtiririko .. WA pathos , ethos and logos .. hapa bongo kwa Kuwa wengi ni bongolala hata ukihutubia ujinga, uongo, utumbo , matakataka .. mataputapu Ila ufuate mtiririko utawaokota wengi Sana .
 
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa hotuba za Tundu Lisu, Dr Slaa, Zitto Kabwe, Freeman Mbowe na Komredi Kinana kwa zaidi ya miaka 10 sasa

Kiukweli Uhutubiaji wa Tundu Lisu leo umekuwa wa viwango vya juu sana

Amekuja.na facts na Takwimu pia katuachia rejea

Kwa mfano issue ya Kura amesema Mwenye mashaka na alichosema aende NEC akahakiki

Issue ya kujificha Ubalozi wa German unaweza kwenda Central Police kuhakiki

Issue ya mapori ya Ikungi kuuzwa unaweza kwenda kwa DED kuhakiki

Issue ya Hayati Mkapa kuchota Dollar million 100 unaweza kusoma Kitabu cha Maisha yake ujiridhishe

Leo Tundu Lisu hakuwa mtu wa propaganda na Uzushi kama alivyozoeleka

Akiendelea hivi itabidi CCM imchukue Prof Kabudi awe anajibu hoja za TAL

Leo Lisu amehutubia kama Benjamin Netanyahu wa Israel!

Kongole kwake
Mpuuzi huyo siasa ya upinzani ameamua kwake ni kufanya biashara kutumikia mabeberu. Hapo ndio ameona inalipa vizuri. Anasemaga uongo akijiamini kijinga kwamba hakuna wenye akili kumzidi.
Saa hizi amefika njia panda ameona bora awe mkimbizi.
 
Back
Top Bottom