Nakubaliana na mtoa mada, tupeni huku tuichambue
Bunge hili linaendeshwa kwa matakwa ya bwege mmoja hivi anatokea huko burigi.Bunge linaendeshwa kwa kanuni na taratibu, waziri mkuu ametoa mapendekezo ya bajeti yake,Kub alitakiwa akosoe kama ina mapungufu au la. Alitaliwa akosoe hata mapungufu ya 2019-2020.Sio kuleta habari za tulipigwa wakati sisi ni wabunge,mara Kub hana nyumba na ananyanyaswa,mara Mh Tundu Lissu bado anadai mshahara,mara CAG aliteleza n.k. Subject matter ilikuwa bajeti ya waziri mkuu,Kub alitakiwa akosoe kama ina mapungufu.
Hizo ndizo gharama za kumkabidhi uongozi mpumbavu.Wabunge na akili zenu timamu mnakula pesa za walipa kodi alafu mnaenda bungeni kutoa hotuba iliyojaa uzushi.
Mnazunguka na kamati za bunge mnakula posho za bure,badala mjibu hotuba ya bajeti ya waziri mkuu, Kub analeta habari zingine kabisa.
Kwamba mlikula virungu au Kub hana nyumba na mshahara wa Tundu Lissu unahusika vipi?
Muwe mnajibu subject matter acheni kupoteza muda.
Wajue tu ujumbe utafika kwa jamii, wapende, wasipende.Utafiti mpya unaonyesha kwamba zaidi ya 85% ya familia za kitanzania kuna Angalau Smartphone 1 na kuna access ya Internet
Uko sahihi na nakuhakikishia kwamba CHADEMA imejiandaa kwa hilo na tuliyajua hayo mapema na utaanza kuona hotuba zetu mitandaoni bila shaka yoyoteNaunga mkono pendekezo.
Kuna bunge kubwa zaidi huku nje zaidi ya hilo lililopo Dodoma, ambalo kwa kila namna linaonekana ni Bunge la Chama kimoja.
Ukweli ni kwamba hawa wabunge wa upinzani walitakiwa wawe walishaunda mfumo mbadala wa kufikisha mawazo yao kwa wananchi kwa njia nyingine zaidi ya hilo Bunge bandia.
Huyu ni mdau humu humu kaamua kubadili ID baada ya kupoteza mvuto kwa wanaJF!Umeanza kwa moto sana bwashee. Tulia soma ramani kwanza.
Kulikuwa na kina Jingalao, Wiliam Malecela na wengineo walikuwa na moto kuliko wewe saa hizi wamepoa sana. Nafsi zao zinawasuta
Nenda taratibu mkuu, kuna maisha zaidi ya siasa na unafiki.