Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.
Nami kama kawaida kwa kushirikiana na wadau wenzangu akinina Skype, MaishaPesa, Simiyu Yetu, Deo Corleone, kbm, Mkuu ya Kaya na wengine tutaendelea kuwaletea yatakayojiri. Hadi wakati huo, Stay Connceted.
-================================================================
UPDATES
Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
*Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
*kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
*semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
*Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
*Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
*Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
*Siku ya Ijumaa saa 10 jioni, Rais atakuja kulizindua Bunge
==================================================================
UPDATES
Jaji Joseph Sinde warioba ameanza kuhutubia bunge mnamo saa tatu na nusu. Katika hotuba yake amepitia sehemu zote za Rasimu ya Katiba. Masuala muhimu aliyoeleza ni kama ifuatavyo
Baada ya hayo na mengine, akiwa amewasilisha hotuba yake kwa dakika 85, Jaji Warioba alipumzika kwa dakika tatu. Na baada ya hapo anazungumzia muundo wa Muungano. Kwamba muundo uliopendekezwa ni wa Serikali tatu. Warioba anasema kuwa wamefanya utafiti juu ya muungano wetu na utafiti huo umeibua malalamiko kadhaa kwa pande zote za muungano. Ni kutokana na malalamiko hayo ndipo walipofikia uamuzi wa kupendekeza muundo wa serikali tatu.
- Mihimili ya dola itaendelea kuwa serikali, mahakama na Bunge
- kuhusu Serikali, Rasimu inapendekeza kuwa matokeo ya Rais yanaweza kupingwa mahakamani na mgombea urais na si mwingine.
- madaraka ya Rais yamepunguzwa hasa kwenye suala la uteuzi
- Mawaziri hawatatokana na wabunge
- Rais hatakuwa sehemu ya Bunge
- Kuhusu Bunge, ukomo wa wabunge ni awamu tatu ya miaka 5
- Spika na naibu Spika hatatokana na Wabunge
- Warioba pia kazungumza juu ya Uraia na amesema kuwa uraia ni wa aina mbili nao ni wa kuzaliwa na wa kujiandikisha. Pia imeelezwa kuwa hakuna uraia wa nchi mbili
======== Updates ==========
Baadhi ya Malalamiko ya Zanzibar;
4.Kutokuwa na Uwazi wa Mapato na Matumizi wa Fedha za Jamhuri ya Muungano,
5. Kutokuwa na Akaunti ya Pamoja.
6. Uwepo wa Mkanganyiko wa Mapato jinsi ya kuchangia gharama uendeshaji wa Serikali zote mbili.
7. Kuwepo kwa Tume mbili zinazoshindana katika Nchi moja.
8. Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mchakato wa kupata misaada kutoka kwa Nchi za nje.
9. Malalamiko kuwa Viongozi Wakuu wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma na sio Zanzibar
10. Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadi ya mambo yamefanywa kuwa ya Muungano kupitia kutungwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo huwa katika utatanishi.
Kwa Upande wa Tanzania Bara baadhi ya malalamiko ilikuwa kama ifuatavyo;
1. Zanzibar imekuwa nchi huru, inabendera yake, inawimbo wa Taifa,Serikali yake na imebadili Katiba yake kutambuliwa kama Nchi.
2. Zanzibar imebadili masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inasema Sheria za Muungano zinazotungwa na Bunge hilo,zitumike sehemu zote, badala yake Katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa ili Sheria
itumike Zanzibar Sharti ipelekwe kwenye Baraza la Muungano.
3. Zanzibar imetunga Sheria kuhusu Fedha, ambalo ni suala lililopo kwenye Katiba ya Muungano.
4. Zanzibar imetunga Katiba ambayo imechukua Madaraka ya Rais yaliyopo kwenye Jamhuri ya Muungano,inaeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano anamadaraka ya kugawa Nchi katika maeneo ya Kiutawala, mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 yametambua kuwa Zanzibar ni Nchi na yamempatia Rais wa Zanzibar mamlaka ya Kuigawa Nchi katika meneo ya Muungano.
5. Katiba ya Zanzibar inaeleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi mbili lakini Katiba ya Jamhuri inaeleza kuwa Tanzania ni Nchi moja.
6. Masharti ya Katiba yaliyowekwa kwenye Katiba ya Zanzibar kuhusu Mchango wa Zanzibar katika mambo ya Muungano yamepingana na masharti ya Muungano.
7. Muundo wa Muungano uliopo umepoteza kutambulisho Kihistoria Tanganyika kuhusu watu wa Tanganyika kupitia maslahi yao.
8. Wananchi wa Tanzania Bara, kutokuwa na haki ya kumiliki Ardhi,wakati wenzano wa upande wa Zanzibar wanahaki ya kumiliki Ardhi Tanzania Bara.
9. Wabunge wa Zanzibar huchangia mijadala ya Muungano na ambayo kwa uhakika wake ni mambo ya Tanganyika na kwamba Wabunge wa Tanganyika hawana nafasi ya kuchangia katika Baraza la Wawakilishi.
10. Kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari ya mwaka 1985 Watanzania ambao ni Watanzania wa Bara kutakiwa kutimiza masharti Maalum ili kupata haki ya kiraia wakati Mzanzibari hutakiwi kupata haki hiyo bila masharti
yeyote,haki hiyo ni pamoja na kugombea Uongozi.
Tume iliamua kufanya uchambuzi wa kina kuhusu malalamiko haya na endapo malalamiko ya Zanzibar yakipatiwa ufumbuzi na ya bara yatakuwa yamepatiwa Ufumbuzi.
JAJI WARIOBA AKIWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE
Inaoenaka CCM tukiwa peke yetu na tukiwa sehemu siri tunataka serekali 3 tukiwa mbele ya vyombo vya habari na watu tunataka srekali 2.
hapa ni wazi ndani ya CCM kuna tatizo.
KWANINI NIMESEMA HIVI
Kama tulivyomsikia Jaji warioba. Sehemu muhimu ndani ya serekali wamependekeza serekali 3.
Kwa mfano afisi ya waziri mkuu, afisi ya makamo wa rais. hizi kama sitakosea zimependekeza muundo wa serekali 3. Hizi ni Ofisi nyeti ambazo kazi yake ni kutatua kero za Muungano.kama zimependekeza muundo wa serekali 3 ni wazi kwamba kuna tatizo.
Hapa CCM tumeshika hatamu. Hapa kuna makatibu wakuu licha ya kutokwa watendaji wa Chama lkn wengi wao ni wakereketwa wa Chama. wakurugenzi na hata mawaziri wote hawa ni Chama chetu.
Kama haya ndio mapendekezo ya ofisi hizi mbele ya jaji Warioba ni wazi CCM pia inataka serekali 3 nyuma ya pazia lkn mbele ya vyombo vya habari inataka serekali 2.
Ofisi ya Bunge na ofisi ya baraza la wawakilishi. Hili kwa kiasi kiikubwa ndio wawakilishi wa wananchi. Kwa mujibu wa warioba hawa pia wamepndekeza serekali 3. hapa CCM imejaa.hapa ndipo alipo spika wa CCM , hapa ndipo penye wenyeviti wa CCM wa kamati za Bunge.Mapendekekezo haya yanaushawishi mkubwa kutoka ccm.
HII NI SEHEMEU YA MAPENEDEKEZO YA TAASISI ZA SEREKALI
103 .Baadhi ya taasisi za kiserikali, ama moja kwa moja au kwa tafsiri ya
mapendekezo yao, pia zilipendekeza au kukubali muundo wa Serikali Tatu. Kwa
mfano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilipendekeza kuwepo kwa mamlaka huru ya
Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano na iwekwe wazi maeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka. Baraza la Ofisi ya Makamu wa Rais lilipendekeza, kuhusu Muundo wa Serikali kwamba, nanukuu
kuwe na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wakuu wa Serikali za Washirika wa Muungano wapewe vyeo vingine 32 vinavyoendana na hadhi na mamlaka zao. Pia katika kutaja hizo serikali tatu inabidi zitenganishwe ili Serikali ya Muungano ionekane ndio ya juu
104. Baraza la Ofisi ya Waziri Mkuu lilipendekeza, kuhusu uongozi wa taifa kwamba kuwe, na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Serikali ya Tanganyika na Waziri Mkuu wa Serikali ya Zanzibar. Mapendekezo hayo ni kwa sababu hakuna umuhimu wa kuwa na marais watatu (3) katika nchi moja na wala neno Rais halimuongezei hadhi kiongozi yeyote. Pia kutoa nafasi kwa Mawaziri Wakuu kuwa watendaji zaidi na hivyo kusimamia Serikali za Washirika. Aidha, Bunge la Jamhuri ya Muungano katika maoni yake
lilipendekeza kuwepo kwa Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo o inajumuisha, katika Wajumbe, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano (Mwenyekiti), Spika wa
Bunge la Tanzania Bara na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mkuuu, hayo ni mawazo yako. Mimi nitakuwa wa kwanza kumpinga jaji warioba kwani mdumo alioupendekeza hauna tija katika kudumisha muungano. Muungano wa kweli ni wa serikali mojana atakaekataa serikali tatu sasa huyo atakuwa mweendawazimu baada ya hoja zote hizo narudia tena atakauwea mwendawazimu.
Revocatus Kashaga, naona unaongelea issue ambayo iko nje ya uwezo wako wa kufikiri. Opinion polls ni Sayansi na huendeshwa kitaalam kwa kufuata misingi ambayo kama utapenda kuielewa, labda thread ifunguliwe. Shida yako kubwa nadhani ni kutoelewa principle inayoongoza utafiti wa maoni ya walio wengi katika jamii. Hakuna namna unaweza kuwauliza Watanzania milioni 45 mawazo yao kama unavyotamani ingefanyika, badala yake unatumia kitu kinaitwa sampling. Ndio maana kwa nchi kama Marekani yenye watu zaidi ya milioni 350, maoni ya watu 35,000 (0.1%)kwa mfano, inatosha kabisa kuonesha wazi muelekeo wa wengi. Bahati mbaya sina muda, labda siku nyingine nitakuelewesha zaidi...naomba nikuache na hili hapa;Kwa mujibu wa ripoti ya mwenyekiti wa tume ya kuandaa rasimu ya katiba inaonyesha kuwa takribani 61% kutoka Tanzania bara waliunga mkono hoja ya serikali tatu na 60% kutoka Zanzibar walipendekeza Muungano wa mkataba; ni wazi kuwa ripoti hiyo haionyeshi kiuhalisia wa jumla ya watanzania waliohojiwa na kutamka kwa vinywa vyao kuwa wanataka muundo wa serikali tatu.
Ripoti hiyo inasema kwa Tanzania Bara wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni yao kuhusu Muungano na karibu 27,000 walizungumzia Muundo (Hawakusema kama wanataka serikali tatu).
Kwa Zanzibar karibu wananchi wote waliotoa maoni walijikita kwnye suala Muungano. Kati ya wananchi karibu 38000 waliotoa maoni, wananchi 19,000walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano (hawakusema kama wanataka serikali tatu).
Sasa swali linalojitokeza ni je, hizi asilimia zinazoonyesha kuwa idadi kubwa ya watanzania wanataka muundo wa serikali tatu inatoka wapi? Ukweli wa mambo unaonyesha kuwa, kimsingi ni kweli kamati teule iliwahoji watanzania takribani 333,516; kati hao watanzania 16,470 walipendekeza muundo wa serikali tatu, kwa Tanzania Bara, wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni yao kuhusu Muungano, 27,000 walizungumzia Muundo.
Kwa Zanzibar wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano na wengi wakipendekeza muungano wa mkataba. Takribani wananchi 287537 hawakuzungumzia suala la muungano au muundo wa serikali tatu.
Sasa je, asilimia 61% inatonduka wapi amabyo inaunga mkono hoja ya muundo wa serikali tatu? Ni watanzania wapi wengi ambao wameonyesha nia ya kuwa na muundo wa serikali tatu?
The mathematics of probability proves the size of the population is irrelevant unless the size of the sample exceeds a few percent of the total population you are examining. This means that a sample of 500 people is equally useful in examining the opinions of a state of 15,000,000 as it would a city of 100,000. For this reason, The Survey System ignores the population size when it is "large" or unknown. Population size is only likely to be a factor when you work with a relatively small and known group of people (e.g., the members of an association).
Kwani kama 1+1=2 na si tatu, iweje tulilie muungano wa serikali tatu. Me ningemuelewa warioba angekuja na suluhu la serikali mojaKinachoonekana ni walaghai kushindana na mkweli. Jaji Warioba hawezi kusema 1+1=3. Ameshuhudia mambo mengi sana ya unafiki na mwisho akakaona aepuke dhambi ya kudanganya watanzania na awambie ukweli kuwa wakati wa Nyerere kulikuwa na Nchi 1 na serikali 2 ambayo ilikuwa rahisi sana kwenda kwenye serikali 1 na Nchi 1. Lkn baada ya mwl. Nyerere; waliofuatia Alhaji Mwinyi, Ben Mkapa na Jakaya Mrisho kikwete wameendekeza serikali 2 na nchi 2.
Pia Jaji Warioba amesema anayeona kuwa Rais wa Muungano hatakuwa anasimamia masuala ya elimu, afya n.k ni yule tu anayedhani kuwa muugano ni Tanganyika akauliza kwani kwa sasa Rais wa Muungano anasimamia hayo huko Zanzibar?. Hili ni somo kubwa katika karne hii watu kama WASIRA na GENGE lake hawawezi kuilewa mpaka warudi shule na hakuna shule ya kuwapokea kwa kuwaogopa! VIVA WARIOBA (Wakondya Tata), Kama sio unafiki ulistahili kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya kuundwa kwa Zanzibar na Tanganyika rasmi. Mungu akubariki sana!
Kitaeleweka tu,siasa zimeufumba uharisia.
Mkuu, mjadala huu ni mpana sana. Ni vema tukatumia forum hii kumwaga yaliyo moyoniMwenyekiti taarifa:
Jaji Mstaafu Joseph Warioba ameamua kuwapendelea Wazanzibari katika hotuba yake ya kihistoria katika kuandika katiba mpya. Popote ambapo Jamhuri ya Muungano au Chama cha Mapinduzi kilipofanya uamuzi kuihurumia Zenji amepita kana kwamba ni haki. Niko tayari tujadili.
mbona wanataka kutimiza unabii wa Kakobe mapema hiviItoshe kusema CCM ni chakubimbi!!!