Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu


Kitaeleweka tu,siasa zimeufumba uharisia.
 

Yaani we acha tu, na hapo ndo kura ya SIRI inapotakiwa!
 
Nimeangalia Tv na kumsikiliza Jaji Warioba vizuri sana. Tume yake imefanya kazi nzuri sana na mwiba kwa wanasiasa si wa ccm tu hata wa upinzani. Wanasiasa hawaipendi hii rasimu ya kuelekea katiba kamili,kisa ni wengi waliwekeza huko ili baadaye wapate marejesho manono.nimeziangalia sura za wenye vyama vya siasa ingawaje vinaitwa vyama vya wananchi,walikuwa wamekunja nyuso zao mithili ya mtu anayemeza sumu. wanasiasa hawa wamemwaga mamillioni kwenye vyama na kujaribu kutumia nguvu kubwa ya kupata madaraka, katiba inayotakiwa na wananchi ndio Warioba kaitilia mkazo kuliko yanayotakiwa na wanasiasa. na sina hakika kama bunge hili litakwisha salama,maana hii rasimu inafanyiwa kila aina ya vioja,vitimbi na hujuma ili isifanikiwe.
 
Viongozi wa Ccm wako malaya. Kama hujui biashara yake, atajifanya ni mwema sana. Ila ukimpa kisogo utamkuta street.
 
na atakaekataa serikali tatu sasa huyo atakuwa mweendawazimu baada ya hoja zote hizo narudia tena atakauwea mwendawazimu.
Mkuuu, hayo ni mawazo yako. Mimi nitakuwa wa kwanza kumpinga jaji warioba kwani mdumo alioupendekeza hauna tija katika kudumisha muungano. Muungano wa kweli ni wa serikali moja
 
Kinachoonekana ni walaghai kushindana na mkweli. Jaji Warioba hawezi kusema 1+1=3. Ameshuhudia mambo mengi sana ya unafiki na mwisho akakaona aepuke dhambi ya kudanganya watanzania na awambie ukweli kuwa wakati wa Nyerere kulikuwa na Nchi 1 na serikali 2 ambayo ilikuwa rahisi sana kwenda kwenye serikali 1 na Nchi 1. Lkn baada ya mwl. Nyerere; waliofuatia Alhaji Mwinyi, Ben Mkapa na Jakaya Mrisho kikwete wameendekeza serikali 2 na nchi 2.
Pia Jaji Warioba amesema anayeona kuwa Rais wa Muungano hatakuwa anasimamia masuala ya elimu, afya n.k ni yule tu anayedhani kuwa muugano ni Tanganyika akauliza kwani kwa sasa Rais wa Muungano anasimamia hayo huko Zanzibar?. Hili ni somo kubwa katika karne hii watu kama WASIRA na GENGE lake hawawezi kuilewa mpaka warudi shule na hakuna shule ya kuwapokea kwa kuwaogopa! VIVA WARIOBA (Wakondya Tata), Kama sio unafiki ulistahili kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya kuundwa kwa Zanzibar na Tanganyika rasmi. Mungu akubariki sana!
 
Revocatus Kashaga, naona unaongelea issue ambayo iko nje ya uwezo wako wa kufikiri. Opinion polls ni Sayansi na huendeshwa kitaalam kwa kufuata misingi ambayo kama utapenda kuielewa, labda thread ifunguliwe. Shida yako kubwa nadhani ni kutoelewa principle inayoongoza utafiti wa maoni ya walio wengi katika jamii. Hakuna namna unaweza kuwauliza Watanzania milioni 45 mawazo yao kama unavyotamani ingefanyika, badala yake unatumia kitu kinaitwa sampling. Ndio maana kwa nchi kama Marekani yenye watu zaidi ya milioni 350, maoni ya watu 35,000 (0.1%)kwa mfano, inatosha kabisa kuonesha wazi muelekeo wa wengi. Bahati mbaya sina muda, labda siku nyingine nitakuelewesha zaidi...naomba nikuache na hili hapa;
 
Kuandika kitu kwa herufi kubwa hata kama kina umuhimu kiasi gani inamaanisha unachokifanya ni shouting tu wala huoneshi umuhimu wake
Mkuu, kawleza hoja ya msingi sana. Si vema kumbeza
 
Kwani kama 1+1=2 na si tatu, iweje tulilie muungano wa serikali tatu. Me ningemuelewa warioba angekuja na suluhu la serikali moja
 
walioba kamaliza kazi yake kazi lipo kwa bunge mkumbuke tume imeshapoteza mabilioni ya pesa na pia bunge linakula mabilkoni yetu arafu msitupatie katiba hatutawaelewa kabisa
 
Mkuu, mjadala huu ni mpana sana. Ni vema tukatumia forum hii kumwaga yaliyo moyoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…