IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Shapu,
Huyu ndugu Ogah msamehe..namuamini waga ni mtu makini sana. Sijui hii hoja leo ameingalia kwa kutokea kipande ipi. Otherwise hoja zake ni makini.
Nadhani muungwana Ogah hajawahi fika Kigoma na hii mikoa iliyo pembezoni mwa nchi yetu ajue hali halisi.
Ogah umeshaambiwa... tangu uhuru almost nusu Karne..Kigoma haijawahi kuwa na barabara ya lami!!!!!..sasa sijui kama hiyo serikali unayoisema ilikuwa likizo ama vipi.
Wakubwa salaam,
Ninawaletea hotuba yangu jimboni Kigoma. Asante
HOTUBA YA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA UCHAGUZI JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI.
KALINZI, AGOSTI15, 2009.
Ndugu wajumbe, ninayo heshima kubwa kuwashukuru kwa jitihada mlizofanya kuhakikisha leo karibu viongozi wote wa vijiji vya jimbo la Kigoma Kaskazini tunakutana hapa kata ya Kalinzi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA. Natambua kuwa mnafanya kazi katika mazingira magumu, lakini mnafanya mambo makubwa sana..........
Asanteni kwa kunisikiliza.
Kabwe Z. Zitto, Mb
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Kalinzi, 15/8/2008.
Je huoni ulichofanya ni usaliti kwa wananchi wa maeneo mengine na kujifikiria wewe peke yako ubunge wako na wananchi wako pekee? Utaalamu wa kufumua bajeti umejifunzia wapi? Waamini ulichofanya ni sahihi?.
Masanja:
Hile posti yako ya mwanzo katika thread imenikumbusha mbali sana. Nadhani wengi wetu hawajafika intilia za Tanzania na kujionea politics za huko.
Dilunga umekuja "kuchafua hali ya hewa hapa nahisi,anyway kutoa maoni yako ni haki yako ya msingi na ipo ndani ya katiba!
Zitto kaza mwendo mkuu;tukijipanga vyema NEC-CCM itakutana sana 2011 kupanga tena kumdhibiti Spika,na wala si kukutana kupanga waone jinsi gani wataleta maendeleo kwa watz maana upinzani utakuwa unadhibiti bunge!
Tunahitaji akina Zitto wengi bungeni!
Dilunga,
Naungana nawe 100%.
Mheshimiwa Zitto ametoa shukrani nzito sana kwa mafisadi kiasi cha kuwafanya wawe ni wa muhimu zaidi katika miradi hiyo kama vile walikuwa anatekeleza miradi hiyo kwa hiari yao. Ninadhani angewaambia wananchi wake straight kuwa alifanikiwa kuifanya serikali isikilize kilio chao na kutekeleza miradi hiyo anayotaja.
Mambo mengine aliyaweka vizuri sana isipokuwa hilo hapo ambalo Dilunga kaengua
hivi kama kweli walifanya hayo mambo aliotaja zitto hawastahili asante japo kuwa wana maovu mengine? sidhani kuna ubaya wowote wa kuwapa asante yao hio inaonesha uungwana kwani hawa watu kama walifanya hayo kwa upande huo wana stahili kupewa hio asante na upande ule wamaovu wanastahili kukemewa.Je, ilikuwa lazima kuwashukuru hao, hasa Chenge na Mrema? Jamani alama za nyakati zinasemaje?
Sasa hao wabunge wa mikoa ya kati ndo na wao wangehangaika wakapata barabara za kuwaunganisha na mikoa ya pembezoni kusudi wapiga kura wao wafanye biashara. Sijua RA mbunge wa Ndugu Sikonge anasikia huu ushauri wa bure?
Ahsante Kichuguu kwa kuliona hilo, aksante.
Zaidi ya Mkapa na Vithlani, hakuna kichwa kinachotafutwa Tanzania kikajibu shutuma za ubadhilifu kama kichwa cha Andrew Chenge.
Zitto Kabwe, mbunge kiongozi wa upinzani, ameenda kuwaambia wananchi kwamba kwa kushirikiana na Ephraem Mrema aliyeilipisha TANROADS Sh bilioni 3.3 kwa kampuni illegal ya Norconsult na Zhakia Meghji aliyesaini makaratasi ya Billal wa EPA, Andrew Chenge amewajengea mabarabara!
Kana kwamba kina Zhakia Meghji na Chenge walifanya hisani kutoa hela, hela zinazopita kwa idhini ya Bunge.
Unalalamika Buzwagi, Buzwagi, Buzwagi halafu wakina Chenge waliosaini mikabata unaenda kuwauza kwa watu? Unasimama mbele za wananchi wenye disapointment na frustration unataja ``Chenge`` kwa ufahari kabisa?
Labda ni Waganda walikasirika mwaka '79 wakatutafutia dawa, au Wakenya walinyunyiza kimiminika na helikopta ili tupwelee tuwaachie ardhi, lakini kuna mkono wa mtu, hatuwezi kuwa wazima. Anamsifu Chenge hadharani?