Watanzania ...hatuwezi kujieleza, halafu tuna a very complex communication system.
Kuelewa hiyo kauli ya Zitto inabidi uelewe culture yetu, hii culture inayomfanya mtu anayekufa na cancer kitandani akiulizwa unajisikiaje ajibu "najisikia vizuri".Kuna mambo fulani ambayo ni crucial sana -kama kum acknowledge mtu kama Chenge, regardless ya alichofanya- kwa sababu za ku play Mr. Nice Guy.This has more to do with our culture than Zitto personally.
Mimi nilifikiri watu tulivyoisema hotuba ya Zitto iliyomshukuru profusely Waziri Mkuu Pinda bila ya kuwa na sababu ya msingi, Zitto alielewa hii concept.
Lakini Bluray, unajua ubovu ya hiyo nadharia kwamba ni utamaduni wetu, kwamba ni aina yetu ya mawasiliano, ni kuwa kuelewa maana halisi ya kinachosemwa kinakuwa ni kubahatisha. Zamani nilifikiri mimi ndio sielewi walengwa - wananchi - wanaelewa, kumbe si peke yangu. Ingekuwa ni culture tungekuwa tunaelewana.
Sasa cheki, wewe hapo umesema ulivyoelewa alichotaka kusema. Lakini angalia huyu mchangiaji mwingine makini sana alivyoelewa yeye, au anavyomwombea Zitto msahama:
MkamaP, hizo shukurani maana yake ni kuwa wale wasio nazo basi na wao wafahamu kuwa mambo yako hivi na nyie mkichachamaa, basi mtajengewa.
Ushaona tafsiri ya huyu Mkuu hapo? Anasema Zitto alikuwa anaongea na watu wa majimbo mengine, sio audience iliyoko mbele yake! Upo?
Kwa hiyo, kila mtu anatafsiri kivyake, wengi tuna struggle kujaribu ku make sense of it, what was he trying to do lavishing praise on Andrew Chenge, tena akiwa katikati ya ngome ya upinzani, Kalinzi, ndani mwisho wa reli huko kwenye grassroots za CHADEMA ambako wanajaribu kujenga chama, vijijini. Unaenda kumhimidi Chenge!
Halafu angalia Zitto anavyowasiliana. Anasema CCM hawana mpango wa kujenga mabarabara ya lami, lakini anasema Chenge na Meghji na Mrema na Bukuku "walielewa tatizo letu... walitenga fedha...wamehakikisha tunajenga mabarabara ya lami"!
Mimi nawaambia viongozi wenzangu, mnapaswa kuwauliza ni wapi ndani ya Ilani ya CCM wameahidi kujenga barabara ya Mwandiga - Manyovu kwa kiwango cha lami?. Hakuna!
__________________________________
Napenda nimshukuru kwa dhati kabisa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu ndugu Andrew Chenge na Katibu Mkuu ndugu Enos Bukuku kwa msaada mkubwa walionipa kuhakikisha tunajenga barabara hii kwa Lami. Napenda kumshukuru aliyekuwa Waziri wa Fedha ndugu Zakia Meghji kwa kuelewa tatizo letu na kutenga fedha
Kha!
Kumbe Chenge na Meghji ni chama gani, CUF?
Zitto aliwahi kuleta hapa draft ya speech anayokwenda kuitoa Bungeni, alikuwa kamwagia sifa Pinda, akaulizwa Pinda kafanya nini huyo, baada ya muda akaelewa somo, akaki edit out kile kipande, hakikufika Bungeni. Leo anaenda kumwinua Andrew Chenge mbele ya watu wa CHADEMA. Yeye anadhani ni political decency and maturity, wakati Chenge hakuna anaetaka kumsikia. Kama anampenda Chenge akanywe nae chai huko, pembeni huko, na akiona tunapita afunike kombe, na akimalizana nae asije kumsujudia sujudia Chenge mbele yetu.