Hotuba yangu jimboni Kigoma


Mie huwa nashukuru wazazi wangu kwa kunizaa......

MkamaP, hizo shukurani maana yake ni kuwa wale wasio nazo basi na wao wafahamu kuwa mambo yako hivi na nyie mkichachamaa, basi mtajengewa. Kama Mwakyembe alijengewa na daraja na wanajeshi akajisifu kuwa ni yeye kajenga na hata hakusema Asante kwa Mwamunyange mkuu wa JWTZ. Mhhh, sasa hivi nasikia JWTZ wanasema kuwa hilo daraja mwakani kabla ya uchaguzi litahitajika sehemu nyingine muhimu saana zaidi ya Kyela. Sasa wewe prove kuwa ni KYELA linahitajika zaidi.
Katika nchi yenye matatizo mengi, ni wanasiasa wanaamua kipi kiwe wapi. Wakikupa si vibaya ukasema asante. Kama wameweza kuchota pesa BoT pale walipohitaji, wanaweza kufanya lolote lile walipendalo. Hapa Zitto alitumia UBAVU wake wa Mkono kwa mkono. Chenge kapata hela nyingi na yeye akatiwe 10% kwa ajili ya wananchi wake.
 

Kasheshe,

Ukiangalia kisheria SI KWELI kuwa Wabunge/Mawaziri/TANROADS wanaojenga. Hii ni kama Dodoma ni mji mkuu ila mambo yote kasoro Bunge yako Dar. Sasa wapi ni MAKAO MAKUU?

Viongozi wanakuwa na hela mkononi. Wao ndiyo wanaamua zijengwe wapi. Sehemu za kujenga zipo kibao. Kama ningelikuwa mie ndiyo waziri wa ujenzi, ningeliweka LAMI kiwanja cha ndege Tabora, kujenga barabara ya LAMI kutoka Nzega hadi Tabora na kuja Sikonge na ipitilize hadi Mbeya. Nikaweka barabara zote za Tabora Lami, maji, umeme, nk na kwengine huko kwa akina Zitto nikakusau na acha wafe na njaa au giza. Sasa mtu atakepigania kwa udi na uvumba hadi zile pesa ziende kwake, huyo ndiyo KAJENGA. Pesa kwenye majimbo haziji tu. Zahanati haziji tu. Umeme, maji na takataka nyingine haziji tu. Ni lazima UPIGANE ili zije. Mtu akipigana hadi zikaja, ukitaka unaweza kusema KAZIPIGANIA ila kisiasa twasema "KAJENGA".
 
Mnyonge Mnyongeni, Haki yake Mpeni!.
Hongera sana Mh.Zitto kwa changamoto zako Bungeni na uliyoyafanya jimboni mwako.
Pia nakuunga mkono ulichofanya kushukuru ni muhimu, huo ni uthibitisho kuwa wewe ni mtu unaekumbuka fadhila.
Shukrani ni jambo jema, haijalishi anayeshukuriwa amefanya mabaya mangapi, hata kama ana mabaya mia moja na jema moja, anastahili shukrani kwa hilo jema moja na shutuma kwa mabaya mia.
Angalizo, wote aliowashukuru, hakuna hata mmoja mwenye tuhuma zozote, labda ni shutuma tuu, kama ni suala la shutuma, hata hao wapiganaji wa ufisadi nao wanazo shutuma lukuki na wengine ni mafisadi walifisidi wakapata pesa, sasa wanapinga ufisadi.
Tusihukumu tusije tukahukumiwa.
Hongera tena Zitto, ila kwa hili la Uenyekiti, mimi Mh....
 
..hii hotuba ina mambo mengi sana positive ya kuangalia.

..kuna suala la soko la kahawa ambalo Zitto anadai amefanikisha.

..kuna msaada kwa vijana wasiokuwa na uwezo ambao anawasaidia kupata masomo.

..vijiji vimepimwa na kupewa hati ya ardhi.

..binafsi naelewa msimamo wa Zitto ktk masuala ya kitaifa, na nilikuwa namsubiri kwa hamu atueleze jinsi anavyoshughulikia masuala ya wananchi wa Kigoma-Kaskazini.

..sote tunapaswa kukumbuka kwamba bila wananchi wa Kigoma-Kaskazini kumchagua Zitto kuwa mbunge huenda wengi wetu tusingemjua ktk harakati za kupigana na mafisadi.
 
kitendo tu cha kukaa na kujadili hotuba ya Zitto tu; kunaonyesha jinsi gani alivyo mbali sana ya wengi wetu humu.Kama kuna kosa kwa mawazo ya mtu fulani basi si kosa kwa Zito na kwa watu wengine.

Inabidi na nyie muandae zenu tuzisome, after all huyu ni Kijana tu!

acheni LOW MIND!

Kama mna hasira hivyo hata nyumba zenu za kupamga za mafisadi hameni!
 

Bado napinga suala la Zitto kutoa shukrani. Hivi mnataka tuwashukuru hata wakoloni kwa kuwa waliweza kujenga vishule, vijizahanati, reli na vijibarabara wakati wanatutawala? Hivi kweli ni halali kumshukuru mtu ambaye amelihujumu taifa au hata kama anashutumiwa tu - lisemwalo lipo la sivyo kwa nini ashutumiwe Chenge na wengine katika kundi la Watanzania lukuki?
 
Hongera Zitto .Mie naishia hapa kwa ufupi tu .Hongera sana na kazana urudi mjengoni Kaka .Unapigana vita kubwa ambayo wengi hapa ni maneno tu hata mtaani kujitokeza kuelezea umuhimuwa Waraka wana ogopa ila nguvu yao kuandika hapa .Nakubaliana na MkamaP kukubali kuto kubaliana na yote ni maoni jamani .
 

Lakini Bluray, unajua ubovu ya hiyo nadharia kwamba ni utamaduni wetu, kwamba ni aina yetu ya mawasiliano, ni kuwa kuelewa maana halisi ya kinachosemwa kinakuwa ni kubahatisha. Zamani nilifikiri mimi ndio sielewi walengwa - wananchi - wanaelewa, kumbe si peke yangu. Ingekuwa ni culture tungekuwa tunaelewana.

Sasa cheki, wewe hapo umesema ulivyoelewa alichotaka kusema. Lakini angalia huyu mchangiaji mwingine makini sana alivyoelewa yeye, au anavyomwombea Zitto msahama:


MkamaP, hizo shukurani maana yake ni kuwa wale wasio nazo basi na wao wafahamu kuwa mambo yako hivi na nyie mkichachamaa, basi mtajengewa.

Ushaona tafsiri ya huyu Mkuu hapo? Anasema Zitto alikuwa anaongea na watu wa majimbo mengine, sio audience iliyoko mbele yake! Upo?

Kwa hiyo, kila mtu anatafsiri kivyake, wengi tuna struggle kujaribu ku make sense of it, what was he trying to do lavishing praise on Andrew Chenge, tena akiwa katikati ya ngome ya upinzani, Kalinzi, ndani mwisho wa reli huko kwenye grassroots za CHADEMA ambako wanajaribu kujenga chama, vijijini. Unaenda kumhimidi Chenge!

Halafu angalia Zitto anavyowasiliana. Anasema CCM hawana mpango wa kujenga mabarabara ya lami, lakini anasema Chenge na Meghji na Mrema na Bukuku "walielewa tatizo letu... walitenga fedha...wamehakikisha tunajenga mabarabara ya lami"!


Kha!

Kumbe Chenge na Meghji ni chama gani, CUF?

Zitto aliwahi kuleta hapa draft ya speech anayokwenda kuitoa Bungeni, alikuwa kamwagia sifa Pinda, akaulizwa Pinda kafanya nini huyo, baada ya muda akaelewa somo, akaki edit out kile kipande, hakikufika Bungeni. Leo anaenda kumwinua Andrew Chenge mbele ya watu wa CHADEMA. Yeye anadhani ni political decency and maturity, wakati Chenge hakuna anaetaka kumsikia. Kama anampenda Chenge akanywe nae chai huko, pembeni huko, na akiona tunapita afunike kombe, na akimalizana nae asije kumsujudia sujudia Chenge mbele yetu.
 
..binafsi nadhani wa-Tanzania tuko too negative.

..kila kitu tunaona hakiwezekani, everybody is not good enough na lazima tumtoe kasoro na kumkatisha tamaa.
 

Mkandara
Wenda mie ndio sielewi kwa hiyo usichoke kunielewesha si unajuwa elimu hakukwishi.

sasa mkuu nataka uniwekee haya mambo mawili bayana la kwanza ni wakati gani na mazingira yepi kitu unachopewa kinaitwa msaada.?

La pili ni wakati gani na mazingira gani mtu hustahili pongezi kwa zao alilotenda?
 
Mkandara, Bob, Swahiba,
Hakuna siku ambayo umeni-bore kama hii!
Sorry, we are friends, but what zitto said is really cheap diplomacy seeking reverage (levelage check spellings) among the people in power, his cronies in his party (we might know what they think), mafisadi etc. It never cookes, this guy spoke the best about corruption, he made us into it, we are discussing it. We already onto it!

One thing, does he know politics, opportunities and loopholes? What do you want to buy by praising the corrupts? This enterprets we still have loopholes in opposition who cannot seize the opportunities, but can act as stoog(ies) for SisiM. I don't trust this boy satements, and I am par with Dilunga!!

We have long way to go achieving democracy!!
 
..binafsi nadhani wa-Tanzania tuko too negative.

..kila kitu tunaona hakiwezekani, everybody is not good enough na lazima tumtoe kasoro na kumkatisha tamaa.

Si hivyo, hii inaitwa analysis.Saa kwa sababu hatujazoea critical analysis hiki ni kitu kigeni kwetu.

Tunahitaji hi zaidi, zero tolerance.
 

Kuna mcameroon hapa aliniuliza plan yangu ipo je ? nikamwambia niko mbioni kurudi nyumbani ,akazidi kuniambia are u mad? nikamwambia kwanini akasema me better to suicide than going back .Nikamuuliza kulikoni??
Kasema cameroon kusainiwa karatasi lako inabidi utowe bribe and top of that itakubidi kushukuru kwa jamaa kuipokea bribe yako.
 

Dilunga,
kuna kitu kinaitwa REFERENCE. Unaweza kufanya kitu kwa kutumia mfano wa mtu mwingine ambaye alifanya kitu kama hicho au kinachofanana tu. Sasa ukishatumia REFERENCE ya mtu fulani, ina maana huyo mtu alipokuwa akifanya au akiandika au akivumbua basi alivumbua kwa ajili ya watu wengine?
Zitto kaonyesha jinsi alivyo-LOBBY. Nilitegemea kila mtu mwenye akili yake atakuwa ameliona hilo kuwa "mwenzetu Zitto kafanya hivi, basi na sisi akili kichwani". Wewe unakuja unasema kwa sababu mie nimeliona hilo na kuandika basi nimebadili maana kwa kuonyesha kuwa alikuwa anaongea na wabunge wengine.

Kuna wakati huwa kweli unaamsha hoja kwenye NEGATIVEs zako. Ila hili naona leo limekukalia kushoto. Au tafute makala nyingine au kajipange upya maana naona umeDANDIA KWA MBELE na limekutupa pwaaaaa!!!!

Dillunga, sasa naamini kuwa wewe ni mtu yule asemwaye:
1. Nilisikia wakiambiwa usinywe Pombe na kuendesha gari, ila kwa kuwa sikuwepo kwenye mkutano nikajua hilo mie halinisihusu.
2. Nilisikia akiwaambia kuwa kuna gonjwa na tujilinde, mie kwa kuwa sikuwepo kwenye mkutano, nilijua mimi hilo halinihusu.
3. Nilisikia wakiambiwa kuna Tsunami inakuja, ila kwa kuwa sikuwepo kwenye mkutano, nilijua mimi hilo halinihusu.

4. Nilisikia Zitto akiwaambia jinsi alivyo-Lobby. Kwa kuwa Dilunga(mbunge) mie sikuwepo kwenye mkutano , nilijua mimi hilo halinihusu.
 
Mh Zitto

Unaonaje hotuba zako ukazikusanya na kuweka kwenye kitabu kimoja ili iwe kumbu kumbu hata kwa vizazi vijavyo?
 

MkamaP,

Kwenye SIASA mambo yako hivyo mkuu. Ukisikia mtu anasema mie sintampigia magoti fulani kwa kuwa yeye ni BIG MAN basi ujuwe magoti yake hadi yameota SIJIDA kwa kuyapiga. Heri ya Zitto kakiri waziwazi waliomsadia. Ila ya Cameroon ni kali maana hata kutoa Hongo inabidi uandike OMBI? Likikubaliwa ndiyo unatoa na hapo unapotoa unapiga magoti kuomba Mungu jamaa asibadili mawazo. Akipokea asante nyingi sanaa.

MkamaP, field ya Civil Engineering ukubali au ukatae, ni field moja ambayo MAFISADI wanaipenda sana. Kule kuna PESA na utafiti wake ni mgumu sana hasa kama wala 10%. Inapofika sehemu kwamba zipo pesa kidogo na mahitaji mengi, wakikupa wewe na kuendelea kumsahau Mkandara na Sikonge, basi inabidi uwape ASANTE. Kumbuka wengine tulipiga pia magoti na kuomba tutowe Hongo ila tukakataliwa vilevile. Matokeo yake Ukerewe na Sikonge ni Ndugu mmoja. Vipi kule kwenu, ile lami aliacha Nyerere bado ipo au ndiyo kuna mashimo kama vile mwajiandaa kujenga mahandaki?
 
Mh Zitto

Unaonaje hotuba zako ukazikusanya na kuweka kwenye kitabu kimoja ili iwe kumbu kumbu hata kwa vizazi vijavyo?

Duuu,

Yaani una maana kuwa hata vizazi vijavyo watakuwa kama sisi? Kumbe hii historia ni kweli:
Mao Zedong, JKN na Borris Yeltsin wameenda kwa Mungu ili kuuliza kule kwao hali itakuwaje in future:

1. Mao Zedong akaambiwa kuwa China inakwenda safi sana baada ya miaka 100, inakuwa super power duniani kwa kila kitu.

2. Borris Yeltsin akaambiwa Russia mambo yatakuwa bomba baada ya miaka kama 150 hivi.

3. Alipokuja Nyerere na swali hilohilo, Mungu akamwangalia na bila kusema neno akaanza kulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…