Hotuba yangu jimboni Kigoma


MASA,
Hapa jibu mwenyewe.
Nikijibu mimi naweza kuandika zaidi ya maneno millioni 10 nikimuonyesha umuhimu wa historia na kumbukumbu.
 

Mzee usisahau History gives glimpse into the future! upo hapo ...
http://www.runnersgazette.com/results/whal02.htm
 

Plan ya hii barabara ikikamilika itakuwa ni bomba sana; ila bado ujenzi wake ni mwendo wa kujikongoja; maana mpaka sasa sehemu kubwa ipo ktk kiwango cha kusawazisha (kuweka level) kwa kumwaga vifusi/udongo, kujenga madaraja/makalavati n.k.
Vile vile process hii imesogea hatua si kubwa sana kama watu wanavyodhani,maana mpaka sasa wala haina dalili ya kufika wilaya ya kasulu ambayo ndio ina mpaka na burundi.

Mheshimiwa mbunge anastahili pongezi zake kwa jitihada zake pamoja na wapiga kura wake but tusiwasahau Wakandarasi (China Hinen km cjakosea) wa hii barabara, wale wachina wamejitahidi sana ktk supervision ya hii project na wapo makini sana.

Vilevile kama mh. mbunge ataweza wakutane na wabunge wenzake kina nzasugwanko na wengineo cjui kina nani hao, wahakikishe ile barabara ya kasulu-kibondo-kahama itengenezwe, maana ndio kiungo muhimu cha kuingilia mkoa wa kigoma kutokea mikoa mingine ya Tanzania.

Tuvute subira nadhani baada ya muda si mrefu wakazi wa kigoma na mikoa jirani wataisahau adha ya TRL, watasafiri na NBS, Adventure, Saratoga at el kwa raha mustarehe bila ya kuonekana wamepakaa poda nyekundu (vumbi jekundu) wakifika safari zao.
Usafiri wa KGM/DSM, KGM/TBR na KGM/MWZ unataka moyo; vinginevyo uwe na nguo za spea ili mwisho wa safari yako ubadili vinginevyo ni kituko!!!


Ni kweli mkuu; watu hawatembei kabisa kuyajua maeneo ya nchi yetu.
 
MASA,
Hapa jibu mwenyewe.
Nikijibu mimi naweza kuandika zaidi ya maneno millioni 10 nikimuonyesha umuhimu wa historia na kumbukumbu.

Mkuu Makyao,

Huo ujumbe wa Masa ilikuwa JOKE. Kama haoikuwa JOKE basi mimi sioni hata haja ya kuweka kwenye VITABU. Ingelibidi iwepo Maktaba ya Taifa na Museum ya Taifa na hizi habari zote ziwe kwenye DVD, Blueray na HDs. Hizi zitadumu milele na milele zaidi ya mavitabu ambayo hata space yanachukua kubwa sana.

Sijui maktaba na Museum ya Taifa tunayo kweli na wanatunza habari kama hizi. Ila itabidi tuweke hadi za akina Kigunge wakipinga waraka wa Wakatoliki ili kuwaonyesha wajukuu zetu jinsi enzi hii watu kwa kupenda UFISADI, wanaweza kusema PUMBA hadi zinaleta RAHA. Hii ni kama lile jengo BAYA la UK ambalo wanafunzi wa Archetecture huwa wanapelekewa kwenda kuangalia jengo la OVYO na kuwaonya wasije wakawa wanafanya makosa ya namna hiyo.
 

Mkuu hapo ndipo panapogomba ngoma kama Chenge ije ikupe madili kwamba kuna vijifisadi vinataka kukufisadi .teh teh teh teh
Hako ka mstari haujakaona nini?.

Nikwambie neno Fisadi RA kafanya mambo makubwa jimboni kwake kupita karibu wabunge wote.wenda naye anamfuko wakusaidia yatima wengi ,tumpe makofi RA kwa hilo kwakwa kwa kwa kwa!!!

Kule kwetu mwaibara hatupokei misaada ya masharati ndio maana wengi wanatuona kama wakorofi
 
Dilunga acha kutupa wasi wasi na uwezo wako....ina mana haujui kama kuna wakati shukrani inahitajika kwa watu waliofanya meme?... Dilunga kutuambia kuwa Zitto amewaambia wakazi wa Kigoma Kaskazini kuwa mafisadi wote ni wasafi?... Ina mana umesahau kuwa hata mabaniani walio wabaya lakini viatu vyao vinaweza kuwa dawa....

Katika hili Zitto ameonyesha ushujaa mkubwa sana wa kisiasa kwa kuthamini michango ya watu bila ya kujali tofauti zao za kimaadili..

Dilunga unatakiwa ku-call spade a spade siku zote..

Ulitaka awashukuru kina nani sasa kwa msaada wao?... Hivi Kigoma kuna majimbo mangapi ambayo hayana lami miaka nenda miaka rudi...

Ulipashwa umpongeze kwa nguvu zako zote na sio kushushia mzigo wa lawama.. Katika hilo zitto wewe ni shujaa na utaendelea kuwa shujaa... Chapa kazi watanzania wenzako tunakuunga mkono kwa ukarimu wako..

Dilunga unapashwa kufahamu kuwa mtu yeyote anapongezwa kwa mazuri yake na analaumiwa kwa mabaya yake...

Keep it up Zitto
 
Je, ilikuwa lazima kuwashukuru hao, hasa Chenge na Mrema? Jamani alama za nyakati zinasemaje?

Yes! it wa absolutely necessary, especially as a "Statesman" ni vizuri kukiri kuwa ulipata msaada hata kama siyo wakati mwafaka. Kwa sababu moja muhimu kuwa wakati wanafanya hivyo walikuwa wanatimiza wajibu wa kazi zao kitaifa, siyo kichama!
Ni sawasawa na akikubali kuwa anapohitaji msaada wa ulinzi wa Polisi anapewa na anashukuru sana.

Hapa ndipo mambo mengi huharibika sana wakati wabunge wanapoteuliwa kuwa mawaziri.
 
dilunga acha kutupa wasi wasi na uwezo wako

dilunga unatakiwa ku-call
sped a sped siku zote..

ulipashwa umpongeze...

dilunga
unapashwa kufahamu

Nimesikia kaka.

Uwezo wangu unatia wasi wasi dada.
 

Mwaibara ni wapi tena?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…