Hotuba yangu jimboni Kigoma

Hotuba yangu jimboni Kigoma

Kwa wale mnaomlalamikia Zitto kwa ku-acknowledge akina Chenge, Meghji etc, nadhani mnasahau kuwa utendaji wa serikali yetu ukoje na hasa hii lobbying ya waziwazi ya wabunge. Hili si suala la mbunge mmoja ni wote tu ni self-serving na nakuhakikishieni hakuna mbunge ambaye sio successful lobbyist anaweza kutetea kiti chake cha ubunge..Hizi ndio facts zilizopo ground-level..ukikaa kushinda nyuma ya computa yako huwezi kuyajua haya.

Maendeleo ktk nchi yetu yanaenda kwa njia ya ku-lobby. Mbunge akiwa na urafiki na waziri wananchi mmeula, mbunge akichonga gega sana kwenye mjengo wananchi ya jimbo lake wanaula, mbunge akiteuliwa uwaziri ndio hivyo tena miradi inaletwa kwa staili ya vimemo.etc etc etc..

Ni sahihi kabisa usemavyo, kilicho mfanya zitto awashukuru chenge na zakhia ni mambo hayo huenda aliwa approach in friendly manner. Au pengine waliogopa kwa sababu wanamjua atalipua mambo mengi, ktk hili kumbuka Dk. Mwakyembe alisema ..."atayasema hata aliyo amua kuto yasema...." ktk sakata la richmond. Kwa hiyo kama wabunge kuna mambo wanajuana so si ajabu akiwashukuru, japo ni wezi.
 
Hongera sana Zitto kwa hotuba nzuri.
Kuwashukuru wote waliofanikisha wewe kukamilisha miradi ya maendeleo ni haki hata kama wamehusishwa na ufisadi. Sio oni mantiki ya mtu kuhoji hizo shukrani kwani wewe hutoi shukrani kwa ufisadi wao, ila kwao kutimiza wajibu zao walipokuwa na dhamana. Hakuna ubishi kuwa viongozi wengi wa serikali kwa makusudi wamekuwa wanapunguza/au kukata huduma katika majimbo mengi yaliyochini ya upinzani. Wasiofahamu warejee kipindi cha fisafi Mkapa katika majimbo yaliyokuwa chini ya upinzani.
 
Dilunga, Kichuguu na wengine,

Lazima kwanza mfahamu kuwa mambo ya UJENZI (civil Engineering) yanakwenda sana na wanasiasa. Ujenzi kwa kuwa huwa unakula hela nyingi sana, huwa unafanya wanasiasa wote wawe wanalala na kushinda huko. Ni ujenzi huohuo uliwafanya akina Bin Laden kuwa JINA kubwa hadi kufahamiana na kuwa marafiki na George Bush Family. Ndiyo maana utaona kuwa kila nchi, wajenzi na wanasiasa ni watu walio karibu sana. Na unaweza shangaa kuwa jamaa alikuwa masikini, ghafla ni tajiri wa kutupwa na ukaja utawala mwingine, ukashangaa umekuwa masikini. Inatosha ukajenga barabara au jengo fulani na serikali IKAGOMA kukulipa. Au ukaagiza mashine za kujengea barabara ya lami kwa mamilion ya dola, zikifika pale Dar, unaambiwa mradi umefutwa. Hizo mashine unaweza kuziweka mapambo............

Tabora yalishaletwa MAPIPA ya lami ili kuuwekea uwanja wa Tabora Lami. Ukabadilika uongozi na Mwandosya akawa Waziri wa UJENZI. Huyu jamaa nafikiri ntaendelea kumchukia kwa hilo. Badala ya aagize mapipa mengine ya LAMI na hayo ya Tabora yabaki na wajenge LAMI, yeye akaja na kuyaondoa. Yakabebwa kimyakimya na kupelekwa Mbeya kwenye uwanja wa ndege. Sijui yalishajengewa au bado? Sintshangaa kusikia hadi leo bado yamekaa ndani ya mapipa maana si kukomoana? Heri tukose wote?

Swala la Zitto kuwashukuru Mafisadi kwa kweli ni swala GUMU. Ila ukisoma niliyoandika juu basi utaelewa kwa nini inabidi UWASHUKURU hawa viongozi MAFISADI. Bila wao ukweli ni kama aliosema Ngosha Masanja kuwa "ISINGEJENGWA". Wangelimgomea tu na wakajenga kwa lami mbovu..... Pia tumekuwa na kimsemo hapa kilicholetwa na member mwenzetu mmoja ila nimemsahau kuwa : HATA SAA MBOVU KUNA WAKATI HUSEMA UKWELI.

Dilunga, tofauti ya YUSUFELI na CHENGE ni kuwa: Chenge ni binadamu na damu ya Yesu inaweza kumuokoa kama akitubu (kama Mkristo). Ila Ibilisi yeye hana cha kuomba msamaha maana laana lake halitibiki. Hiyo ndiyo tofauti kuwa Ibilisi hafanyi zuri lolote lile wakati Chenge kama binadamu, anakuwa ni saa bovu ambalo mara mbili kwa siku husema saa ya kweli. Inawezekana Zitto aliBAHATIKA kuwa kwenye muda haswaa ambao saa linasema ukweli - JIMBO LAKE LIKAPATA LAMI.
 
Mkuu Zitto,
hotuba imefika.ukirudi jamvini kupitia response ya wapiga kura waliochaichambua hii hotuba naomba uyawweke wazi yafuatayo:

-ni kweli unagombea uenyekiti wa chama?
-ni kweli unataka gombea jimbo moojawapo hapa dar es salaam?
 
Na sio ajabu unaweza kukuta akina Zitto wana-lobby kujengewa barabara ambayo haitoki nje ya mkoa yao! Nilikuwa Kigoma mwaka jana na nimejionea hali halisi ya kule. Sasa technically ni upotevu wa fedha za umma kujenga barabara ambayo haitoki. Kwa maoni yangu, mathalan kwenye ishu ya barabara, serikali ilitakiwa ihakikishe kwanza mikoa yote inafikika kwa njia ya barabara ya lami . Baada ya hapo nguvu ndio zielekezwe kuangalia makao makuu ya wilaya na miji.nk.nk.nk.

Mkuu,
Hilo swala lipo sana Mbeya. Kwa Mwandosya barabara na umeme huwa zinaishia kwenye mpaka wa JIMBO lake la uchaguzi. Haizidi hata cm 1.

Labda hii inabidi iwe fundisho kwa WANANCHI WAPIGA KURA kuwa mambo ya kuchagua wabunge wa kupitisha bajeti yamepitwa na wakati. Mtu kama Komba kakata viuno wee basi MNAMPA ubunge. Sasa huko aje atetee nini? Kutetea kukata viuno? Kwake yeye kuwa na Nyumba pale alipo sasa ni the dream becomes true. Sasa ukianza kumwambia maji taka yasiwepo, barabara nzuri, maji masafi, umeme, ........ kwake ya nini??

Kama Kigoma walimchagua Zitto na kutoka kwake Upinzani ame-lobb hadi barabara itajengwa, hayo ndiyo mambo sasa. Sisi hapa Sikonge tulimchagua kunguru Saidi Nkumba wa CCM, tumepata nini? Hawa ndiyo wanaitwa wasindikizaji na wagawa KURA tu. Yeye kila siku ni KUULIZA ili asikike radioni au kuuza sura kwenye TV. Jibu lolote akipewa hata la kitoto basi huwa anaridhika. Kwanza ninawasiwasi hata kama huwa anasubiri jibu zaidi ya kufurahi kuwa kafanikiwa kuuliza swali.

YES, tuchague wabunge Wazuri wa kutufanyia Lobbying BUNGENI na kutupigania haki zetu kimajimbo na kitaifa. Hebu fikiri wangelitokea akina Zitto kama 30 hivi wakaanza kugombania hilo milions za ujenzi wa lami. Hapo ndiyo ungeliona kile kinafanyika nchi kama za Korea. Zingelitandikwa humo ndani ya bunge na waziri wa Miundombini angelikuwa milele ana hali mbaya. Nisingelishangaa wengine wangekuwa wanakataa. Lakini ndiyo unakuta kwa TANZANIA hata wanalilia wapewe ..........
 
Nakubaliana na Mkaguzi katika swala la ukomavu, lakini nadhani Zitto angezishukuru wizara husika pamoja na Tanroads bila kuwataja majina viongozi hao manake majina yao yanatuchefua kweli kweli.
 
Mbunge mwingine ,tuseme yule mwenyekiti wa ccm mkoa shinyanga ajaribu kumshukuru Edward Lowasa kwa kuvunja ule mkataba wa kutumia maji ya ziwa victoria na kufanikisha kuyafikisha maji hayo shinyanga sehemu kama.

Utaona moto wake humu ataitwa kila aina ya jina.
 
Katika shuguhuli za Bunge lobbying ndio kazi haswa ya Mbunge. Mabunge yote duniani hufanya hivyo. Mnakumbuka miswada ya Obama kuhusu miundombinu jimboni kwake kutoka federal funds.......? All politics is local.

Nimewashukuru kina Chenge sio kwa sababu ninawapenda, bali kwa sababu walisaidia sana barabara hizi kujengwa Jimboni kwangu. Wabunge wa CCM wa mkoa wa Kigoma walienda delegation kwa Waziri kumshawishi kuwa barabara zinazopita jimboni kwangu zicheleweshwe mpaka baada ya uchaguzi. Chenge akaniita ni kunieleza na kuniambia amekataa. Pia kulikuwa ni 'deal'. Mtakumbuka mwaka 2007 Hazina ilitenga fedha kiasi kidogo sana kwa Wizara ya Miundombinu. Bajeti ile ilikuwa inalipa madeni tu ya wakandarasi na kusingekuwa na miradi mingine. Wakati huo mimi nilikuwa Mjumbe wa Kamati ya fedha na Uchumi ya Bunge na waziri kivuli wa Uchumi. Kamati ya Miundombinu ikamtuma Mbunge wa Sumbawanga mjini Mzee Kimiti kuja kamati ya fedha kutuomba tuzuie Bajeti yote mpaka Fedha za Barabara ziongezwe. Wabunge wakaniteua mimi kuandaa paper ya fedha zitapunguzwa wapi. Mimi niliongoza timu ndogo ya Wabunge kufumua Bajeti ile na tukaja na wazo la kupunguza bajeti ya 'matumizi mengineyo' kwa asilimia 15 na fedha zote kwenda katika barabara. Katika mazungumzo haya ndipo nilipofanikiwa kupata fedha za Barabara ya Mwandiga Manyovu (kutoka 800m mpaka 7bn mwaka ule, na imekuwa hivyo kwa miaka iliyofuatia). Ilikuwa ni mazungumzo binafsi ya Waziri wa Fedha (Zakhia Meghji) na Waziri wa miundombinu (Andrew Chenge) kwa msaada mkubwa wa Dkt. Bukuku yaliyopelekea kupatikana kwa mradi. Chenge alikataa ushawishi wa Wabunge wenzake wa CCM kuchelewesha lakini pia ndugu Mrema wa TANROADS alikataa ushawishi wa wabunge hao hao kuchelewa kutangaza tenda.

Nimewashukuru watu hawa kwa sababu mbili

1. Uungwana wa kushukuru (mnyonge mnyongeni, Haki yake mpeni)
2. Kutuma ujumbe kwa CCM na wabunge wake na Waziri Mkuu Pinda kuwa mradi ule haukushuka tu. Kuna kazi ilifanyika na wao hawajui. Ninaamini wamekwenda kumwuliza Chenge!

Mwisho, naomba nieleweke kuwa siasa zangu sio za Kinafiki. Ninasema ninachofikiri na ninachomaanisha. I am not choosing words to fit the political wave. Tumezoea wanasiasa wa aina hiyo. Mimi sipo hivyo! What you see in Zitto is what you get - Mkandara once said!
 
Bravo Zitto kweli wewe Kidume umewapiga bao wabunge wasinziaji Bungeni wao kugonga meza tu wkt majimbo yao yanataabika tu.
 
Bw.Zitto,

Kukubaliana na mtindo huo wa kuitana pembeni ili kuleta miradi ya maendeleo nadhani sio aina ya lobbying iliyoleta maendeleo Marekani na popote kule. Mojawapo ya effects za ku-lobby hiyohiyo mpaka leo watu wa Kigoma hawana usafiri wa uhakika!

Maendeleo endelevu na ya kweli yanawekewa mikakati kitu ambacho hakipo hapa Tanzania. Miradi ya maendeleo inaletwa kwa njia ya ajali (randomly) bila ya kuzingatia vipaumbele au miakakati na vigezo sahihi vya kisayansi . Kwa aina hii ya uendeshaji nchi na kuruhusu miradi kupelekwa njia zisizo za kisayansi ndio inasababisha miradi kuishia njiani baada ya 'mnene' anayeshinikiza kuondolewa mahali husika na matokeo yake fedha za wavuja jasho kupotea bure.

Nasema haya sio kwamba barabara isijengwe bali barabara zijengwe kukamilisha network na sio kufuata matakwa ya kisiasa.

Lobbying ya aina hii mnayoipigia debe ni ubabaishaji na inadhirisha mifumo yetu ya kujiendesha ni dhaifulhali.
 
You are very very wrong.

The roads being built in my constituency are strategic roads. Mwandiga Manyovu links Kigoma municipality and Bujumbura city and Kigoma Kidahwe links Kigoma and Tabora.

Nani kakwambia miradi hii siyo ya kisayansi? Wouldnt you just googleearth and view the roads?
 
nini majukumu ya Tanroad, waziri wa miundo mbinu na waziri wa fedha?
 
big up zitto, endelea kuwaburuza. sisi tunaofaidika ndio tunaokuelewa, wasiojua hawawezi kukuelewa milele. Big up. BY THE WAY MWANAKIJIJI nakuomba 2010 uingie mjengoni na wewe. ili mkasaidiane na zito kuwaburuza hawa wazee
 
Nimeipenda hiyo point ya Uungwana wa kushukuru (mnyonge mnyongeni, Haki yake mpeni)

Hata kanisani, misikitini na kwenye shughuli nyingi za kijamii mafisadi wanapotoa michango mikubwa wanapigiwa makofi, Viongozi wetu wa dini wanawapogeza sana japo ni mafisadi...
 
Bravo Zitto kweli wewe Kidume umewapiga bao wabunge wasinziaji Bungeni wao kugonga meza tu wkt majimbo yao yanataabika tu.

Niungane na Fide na wengineo kukupongeza Zitto kwa kazi nzuri. Of course wewe ni mwanadamu una challenges zako lakini nasema toka moyoni kuna mengi ya kujifunza kutoka kwako. Nimeguswa sana na hotuba nzima lakini zaidi sana issue ya kusomesha watoto wasiojiweza imenitoa machozi to be honest. Hii support kwa hao watoto 198 hakuna anayejuwa itafika umbali gani. Queen Jordan ambaye ni activist mkubwa wa elimu kwa watoto anasema "Education is the best equalizer to human kind" Ni ngumu sana Zitto kujuwa ni kazi ya ukubwa gani umefanya katika hili-Mungu akubariki sana sana. Siasa ina mambo mengi lakini yasikukatishe tamaa wewe songa mbele. Nakumbuka Pinda alipofanya ziara huko alisema ni CCM ndio waliojenga barabara sasa sijuwi ni katika hiyo bilioni moja tunayowalipa kwa kodi zetu kama ruzuku kila mwezi? Songa mbele Zitto uko very determined nasi wapenda nchi tunakuombea dua kwa Mungu ufanikiwe.
 
Katika shuguhuli za Bunge lobbying ndio kazi haswa ya Mbunge. Mabunge yote duniani hufanya hivyo. Mnakumbuka miswada ya Obama kuhusu miundombinu jimboni kwake kutoka federal funds.......? All politics is local.

Nimewashukuru kina Chenge sio kwa sababu ninawapenda, bali kwa sababu walisaidia sana barabara hizi kujengwa Jimboni kwangu. Wabunge wa CCM wa mkoa wa Kigoma walienda delegation kwa Waziri kumshawishi kuwa barabara zinazopita jimboni kwangu zicheleweshwe mpaka baada ya uchaguzi. Chenge akaniita ni kunieleza na kuniambia amekataa. Pia kulikuwa ni 'deal'. Mtakumbuka mwaka 2007 Hazina ilitenga fedha kiasi kidogo sana kwa Wizara ya Miundombinu. Bajeti ile ilikuwa inalipa madeni tu ya wakandarasi na kusingekuwa na miradi mingine. Wakati huo mimi nilikuwa Mjumbe wa Kamati ya fedha na Uchumi ya Bunge na waziri kivuli wa Uchumi. Kamati ya Miundombinu ikamtuma Mbunge wa Sumbawanga mjini Mzee Kimiti kuja kamati ya fedha kutuomba tuzuie Bajeti yote mpaka Fedha za Barabara ziongezwe. Wabunge wakaniteua mimi kuandaa paper ya fedha zitapunguzwa wapi. Mimi niliongoza timu ndogo ya Wabunge kufumua Bajeti ile na tukaja na wazo la kupunguza bajeti ya 'matumizi mengineyo' kwa asilimia 15 na fedha zote kwenda katika barabara. Katika mazungumzo haya ndipo nilipofanikiwa kupata fedha za Barabara ya Mwandiga Manyovu (kutoka 800m mpaka 7bn mwaka ule, na imekuwa hivyo kwa miaka iliyofuatia). Ilikuwa ni mazungumzo binafsi ya Waziri wa Fedha (Zakhia Meghji) na Waziri wa miundombinu (Andrew Chenge) kwa msaada mkubwa wa Dkt. Bukuku yaliyopelekea kupatikana kwa mradi. Chenge alikataa ushawishi wa Wabunge wenzake wa CCM kuchelewesha lakini pia ndugu Mrema wa TANROADS alikataa ushawishi wa wabunge hao hao kuchelewa kutangaza tenda.

Nimewashukuru watu hawa kwa sababu mbili

1. Uungwana wa kushukuru (mnyonge mnyongeni, Haki yake mpeni)
2. Kutuma ujumbe kwa CCM na wabunge wake na Waziri Mkuu Pinda kuwa mradi ule haukushuka tu. Kuna kazi ilifanyika na wao hawajui. Ninaamini wamekwenda kumwuliza Chenge!

Mwisho, naomba nieleweke kuwa siasa zangu sio za Kinafiki. Ninasema ninachofikiri na ninachomaanisha. I am not choosing words to fit the political wave. Tumezoea wanasiasa wa aina hiyo. Mimi sipo hivyo! What you see in Zitto is what you get - Mkandara once said!

Huku ndo kumkoma nyani mchana kweupeeeee...!!!!!

Asante sana mhehimiwa mbunge wa Kigoma Kaskazini. Wenye macho hawaambiwi tazama. Juhudi zako zinaonekana. Tuendeleze mapambano.
 
Hii ndiyo nimeandika page ya nyuma. Mkichagua Libunge lijinga, hivi vitu hata halijui mnategea nini? Kuna mjinga mmoja alishasema eti wenzetu USA wameendelea sana, wana ma-computer. Sasa mtu anayetoa pumba kama hizo ukampa ubunge, masikini yarabi.
Tuchague wabunge wenye mueleo wa mbali wa mambo na wana power ya kwenda kwenye mawizara na kudai haki za wananchi. Ukipata mbunge anayesema "mie najua KUKATA VIUNO sana na pia huimba kwa sauti ya juu sana", akifika bungeni kweli ATAKANA VIUNO. Haya mambo yanayokwenda kwenye vikao vya pembeni yeye wala hafahamu. Anasema tu " ehhh, mwenzetu ana bahati". Na ndiyo majinga yanayokuja kuuza nchi kwa dola milioni 20. Kwa kuwa wao ni wa bei rahisi, basi huuza au kujiuza kwa bei chee kabisa.
Chagua Mbunge IMARA na mwenye muono wa KIMATAIFA, chagua Rais IMARA na mwenye muono wa KISAYARI, hapo kweli mtaenda mbele. Vinginevyo, kalaga baho.
 
nini majukumu ya Tanroad, waziri wa miundo mbinu na waziri wa fedha?

Mkuu MkamaP,

Majukumu majukumu. Kwenye mambo ya UJENZI, majukumu hata hayapo. Soma ujumbe wangu page ya NYUMA.
Kama angelitokea RAIS kutoka UKEREWE, na anapenda sana kwao (kama Mkandara vile) basi ile PORT ingelijengwa, kivuko cha uhakika kwenda Bunda kingeliwekwa, na meli ziwa Nyasa zingelikuwa kibao.

Unaona Mtwara kulivyo sasa? Kwenda Mozambique itakuwa tambarare. Unafikiri vimekuja kutokana na MAJUKUMU ya hao jamaa juu?
HILO LILIKUWA LOBBYING LA NGUVU LA CHE NKAPA.
 
You are very very wrong.

The roads being built in my constituency are strategic roads. Mwandiga Manyovu links Kigoma municipality and Bujumbura city and Kigoma Kidahwe links Kigoma and Tabora.

Nani kakwambia miradi hii siyo ya kisayansi? Wouldnt you just googleearth and view the roads?

Bw. Zitto,

Nadhani hujaipata main point au umeiavoid 'kisiasa'. Hoja yangu kuu ilikuwa upatikanaji wa miradi ya maendeleo kwa njia ninazoziona sio za kukubalika, jinsi inavyoweza ku-override mikakati au masterplan za wataalamu wetu na kuishia kukwamisha maendeleo ya pamoja kama taifa. Sijui kama umenipata.

Sikuwa nazungumzia specifically kuwa barabara 'yako' haipo kwenye vipaumbele au kama ulivyoiita kitaalamu 'strategic'. Pia nijuavyo ni kuwa barabara ya Kigoma - Tabora bado haitoki sasa sijui ni strategy gani hiyo unayoizungumzia.

Nitarejea kukomenti ile michakato yenu ya kule mjengoni. Nina machache ya kusema kwenye post yako ya pili sehemu iliyobaki.
 
Back
Top Bottom