Hotuba yangu jimboni Kigoma

Hotuba yangu jimboni Kigoma

Nashindwa kabisa ku post topic mpya?how?

Chagua jukwaa unalotaka kuanzishia post mpya. Kisha ukiangalia juu kabisa (kuelekea upande wa kushoto wa page yako), kuna sehemu ya kuanzisha new thread.

Bonyeza hiyo kisha utapata page ya kuandikia new thread yako.
 
Ninajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kuwa ninatimiza majukumu kwa vizuri ili yeyote atakayeteuliwa na CHADEMA kuwa Mgombea aweze kuwa na rekodi ya kujivunia na apate ridhaa ya kuwa Mbunge wetu.
Asanteni kwa kunisikiliza.

Kabwe Z. Zitto, Mb
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Kalinzi, 15/8/2008.
Mkuu umeeleweka.

Nilikuwa na mkuu mmoja wa sisi M hapa wakati nasoma hii thread ansema wewe ni tishio kwao.
😀
Mimi nakukubali mkuu. wewe uko juu. Hawa ndugu zako wasipokuelewa watakufa maskini vinywa wazi.

Wakupe tu ubunge tena bila kupingwa! Vyama mapinduzi sijui havitawatoa.
 
Sometimes tunahitaji kuweka mukhtasari wa habari au hotuba yenyewe ,na ingekuwa vizuri kama hotuba nzima ingekuwemo kwenye pdf file attached ,wengine tukisoma msusuru wa habari basi tukifika katikati yale ya mwanzo huwa hayapo tena ,inatokana na kasi ya kusoma,ila hongera Mheshimiwa Zitto kwa kuwaweka sawa wananchama na zaidi wambie ikiwa utanafasika kuwahutubia tena kuwa ,Chama ni wananchi na si viongozi,kwani viongozi wanaweza kuhama hama au kurejea CCM au kukisaliti Chama kama tulivyoona kwa baadhi ya viongozi wa kutegemewa katika kambi ya upinzani ,hivyo wao wananchi ndio wadau wakuu wa vyama vya upinzani.

Mwenyezi Mungu akipenda muumalize mkutano wenu kwa salama usalimini na mpate baraka za mwezi Huu mtukufu wa Ramadhani kwani nia zenu ni kuwakomboa na kuwatetea wanyonge popote pale walipo hapa Tz na Pemba.
 
siasa ni mchezo mchafu, lakini Zitto anapoelekea sio, naona yupo bize sana kuwasafisha hao jamaa wenye network ya DOWANS, kwa "kuwasifia" hao jamaa sisi unatuachia maswali mengi mno maana sasa hivi hali ya kisiasa ipo kwenye transition ya kugawanyika mafungu mawili Mafisadi na wasio.

Kwa hiyo hata wa upinzani nao pia wapo kwenye huo mchakato wa upepo wa kisiasa, unaweza ukawa unawasafisha wenzio huku wanakuachia matope na maji yameisha,
kwa hao jamaa (Chenge at el) kutoa na kusimamia huo mradi ilikuwa ni wajibu wao na wala hawakustaili kushukuriwa wala kusifiwa hao walikuwa wametimiza wajibu wao.

Lakini kama kulikuwa hakuna fungu la huo mradi na wewe ukaforce mpaka ukapata hilo fungu kwa mlango usio sahihi nadhanin sasa huko bize kulipa fadhila, na kwa mwelekeo munaoenda itakucost sana kulipa hizo fadhira, reputatuion yako itakuja kuondoka kabisa, maana ulitupa wasiwasi sana kwenye issue ya DOWANS, kwa ule msimamo wako wa kifisadi, nadhani pia ilikuwa ni kulipa fadhira sasa sijuhi ni hizi za hii barabara au ni nyingine.

Time will tell, muda wa shinikizo ukifika nadhani utakuwa wazi zaidi ya sasa ambapo unaingia na kutoka
 
Wakubwa salaam,

Ninawaletea hotuba yangu jimboni Kigoma. Asante

HOTUBA YA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA UCHAGUZI JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI.

KALINZI, AGOSTI15, 2009.

Ndugu wajumbe, ninayo heshima kubwa kuwashukuru kwa jitihada mlizofanya kuhakikisha leo karibu viongozi wote wa vijiji vya jimbo la Kigoma Kaskazini tunakutana hapa kata ya Kalinzi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA. Natambua kuwa mnafanya kazi katika mazingira magumu, lakini mnafanya mambo makubwa sana..........

Lakini zaidi nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutusaidia uhai hadi leo hii kupata fursa ya kufanya mkutano huu muhimu sana kwa mustakabali wa chama na hatima ya demokrasia, kuanzia ngazi za msingi, vijiji vyetu, kata, jimbo, na kimsingi Taifa kwa ujumla.
Sote tunajua kuwa huu ni mkutano mkuu wa pili kikatiba tangu mnichague kuwa mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini mwaka 2005.

Kuna wengi tulikuwa nao katika mkutano mkuu uliopita, lakini leo hatunao kwa sababu mbalimbali. Wapo waliotangulia mbele ya haki, Mwenyezi Mungu awalaze mahala pema! Wengine hatunao kwasababu hawakupata fursa kutokana na michakato ya chaguzi kwenye vijiji na kata zao;Na hiyo ndiyo demokrasia yenyewe tuliyoamua kufuata kama chama. Wapo ambao wamekwenda katika vyama vingine na wengine tunao hapa kama wajumbe wapya kutoka vyama vingine vya siasa. Sote sasa ni familia moja ya CHADEMA yenye lengo la kutoa uongozi mbadala na kuchochoea maendeleo katika Jimbo letu.

Ndugu wajumbe;
Wengi tumekuwa tukikutana, kuwasiliana na kujadili katika nyakati tofauti ninapokuwa kwenye ziara za jimbo letu, na hata nje ya jimbo letu katika harakati mbalimbli za kuchochea maendeleo. Ninawashukuru kwa kazi yote tuliyoifanya, na kwakuwa leo tumekutana tena, ni fursa basi kuangalia kwa pamoja kama tumefanikiwa kufanya nini kuelekea malengo tuliyo jiwekea.

Ndugu wajumbe;
Ni kazi ya Mkutano Mkuu wa chama kutafakari kuhusu kazi ambazo kama chama tumezifanya kuelekea malengo tuliyojiwekea. Chama chochote cha siasa kina kazi kuu za aina mbili; kuna kazi za chama ndani ya chama, na kuna kazi za chama kwenye jamii. Kazi za chama ndani ya chama ni majukumu yote ambayo tunayafanya kuhakikisha chama kinajiendesha, kinafanya vikao, kinatekeleza na kusimamia maamuzi ya vikao kwa lengo la kuhakikisha kinajenga mtandao imara wa chama kuanzia ngazi za msingi. Kwahiyo, tunapokutana leo kupima kazi tunazofanya kuelekea malengo yetu, tunapaswa kujiuliza tumefanya nini kuelekea ujenzi imara wa chama, tumefanya nini kuhakikisha uongozi wa pamoja ndani ya chama, tumefanya nini kuhakikisha tunawaunganisha zaidi wanachama kuanzia ngazi ya msingi, vijiji, kata mpaka jimbo.

Kazi ya pili ya chama ni ujenzi wa chama kwenye jamii. Hii ni jumla ya majukumu yote ambayo viongozi tunayafanya kutetea na kuhakikisha maendeleo kwa jamii yetu..Hii ni kazi muhimu sana kwa chama. Ni muhimu kwasababu ni kazi hii inayomfanya mtu wa kawaida kuona sababu ya kujiunga na chama. Kwahiyo tunapokutana leo katika Mkutano Mkuu, tunapaswa kujiuliza,sasa ni takribani mwaka mmoja kuelekea uchaguzi, Tumefanya nini kutetea na kuhakikisha maendeleo kwa jamii tunamoishi?

Ndugu wajumbe;
Mnafahamu kwamba tangu kurejeshwa mfumo wa vyama vingi, ni kipindi hiki ambacho jimbo letu limefanikiwa kuongozwa na upinzani, tena kupitia chama chetu CHADEMA. Kwa hiyo Kigoma Kaskazini, CHADEMA ndio chama chenye Mbunge, ingawa sio chama tawala kwani hatuna madiwani wengi wala wenyeviti wa vijiji. Ndio maana ni lazima viongozi wawe na ujuzi wa kujua namna ya kuendesha siasa ukiwa chama chenye uwakilishi Bungeni. Nasema ni lazima kwasababu maswali mengi yanayohusu maendeleo ya jimbo hili ni sisi viongozi wa CHADEMA wenye jukumu la kutoa majibu yake. Nasema ni sisi, na sio mimi kwasababu siwezi kukutana na kila mwananchi ndani ya jimbo hili kumweleza tunafanya nini? Na Tumekwishafanya nini?. Ni jukumu la viongozi wote kujua wenyeviti wa vijiji kupitia CHADEMA wamefanya nini kuelekea malengo yetu? Madiwani kwa tiketi ya CHADEMA wamefanya nini kuelekea malengo yetu? Na Mbunge wa Jimbo lenu nimefanya nini kuelekea malengo tuliyojiwekea.

Ndugu wajumbe;
Mnakumbuka niliwaambia wakati wa kampeni mwaka 2005, kuwa haiwezekani sehemu zingine za nchi serikali inabandua lami na kuweka lami ilhali majimbo mengine mtoto anaweza kuzaliwa, kusoma shule ya msingi kijijini, sekondari kwenye kata, chuo cha ualimu kwenye wilaya, na kufanya kazi ndani ya wilaya hata kustaafu kabla ya kuona lami. Nikasema hili haliwezekani, na nikawaahidi kupigania ujenzi wa barabara ya Mwandiga Manyovu kwa kuwa nilijua kuna kila sababu ya barabara hii kujengwa kiwango cha lami, na hakuna sababu hata moja kuzuia hili.

Niliposhika Ubunge wa Jimbo hili, nilikuta bajeti ya Barabara ya Mwandiga – Manyovu ni shilingi 800 milioni tu katika Bajeti ya mwaka 2005/2006. Nilikuta mpango wa serikali ya CCM ni kuweka lami inayoitwa ‘Otta Seal’ ambayo ni teknolojia ya Afrika Kusini. Nilikataa lami hii kwani haidumu na mvua tatu tu za Kigoma zingeweza kuondoa lami hiyo! Ndani ya Kamati za Bunge ya miundombinu na Fedha na Uchumi na ndani ya Bunge la Bajeti la 2006/2007 nilikataa kata kata mradi walioutaka na kubadili fedha hizo kwenda kufanya upembuzi yakinifu. Matokeo ya hatua hizo za Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini ndio yanayoonekana leo katika mradi wa mabilioni ya ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Manyovu. Bajeti zilizofuata niliweza kufuatilia na kuongeza fedha kutoka 800 milioni nilizozikuta mpaka Bilioni 7 mwaka 2009/2010.

Napenda nimshukuru kwa dhati kabisa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu ndugu Andrew Chenge na Katibu Mkuu ndugu Enos Bukuku kwa msaada mkubwa walionipa kuhakikisha tunajenga barabara hii kwa Lami. Napenda kumshukuru aliyekuwa Waziri wa Fedha ndugu Zakia Meghji kwa kuelewa tatizo letu na kutenga fedha. Nawashukuru sana TANROADS chini ya Mkurugenzi Mkuu ndugu Mrema kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa katika Mradi huu.

Nimepigania kuhakikisha hilo, mchakato wa ujenzi wa barabara umeanza, viongozi wa CCM wanaanza kuweweseka na kudai kuwa wanatekeleza ilani ya CCM. Mimi nawaambia viongozi wenzangu, mnapaswa kuwauliza ni wapi ndani ya Ilani ya CCM wameahidi kujenga barabara ya Mwandiga - Manyovu kwa kiwango cha lami?. Hakuna! Mimi najua nimefanya nini kuhakikisha hili linafanyika! Ndio sababu mlinichagua. Viongozi wa CHADEMA mnao wajibu wa kuwaliza viongozi hao wanaojipitisha huku kwa aibu na kudai eti ni Ilani ya CCM inayojenga barabara ya Mwandiga - Manyovu.

Hii ni barabara ya kwanza ya kiwango cha lami kujengwa ndani ya jimbo hili na Mkoa huu tangu Tanzania ipate uhuru. Mnapaswa kuwauliza walikuwa wapi miaka yote hiyo wakumbuke leo? Mnapaswa kuwaliza, Mkoa wa kigoma tuna majimbo saba, huku sita yakiongozwa na CCM. Waulizeni kwanini hawakwenda kujenga majimbo yaliyo chini ya CCM?. Kwanini Kigoma Kaskazini, kwanini leo? Mimi najua ni kwanini Kigoma kaskazini, najua kwanini leo, ndio sababu mlinichagua!..Na ndio maana nawaambia, ninyi viongozi mna kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kazi hii!

Ndugu wajumbe;
Leo viongozi wote wa vijiji mko hapa. Wakati wa kampeni mwaka 2005, ni vijiji 5 tu kati ya 32 vilikuwa vimepimwa. Nikaahidi kuhakikisha vijiji vyote ndani ya jimbo langu vinapimwa ndani ya miaka 5 ya uongozi wangu. Leo ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, Naomba niwaulize viongozi wa vijiji, Ni kijiji gani katika jimbo hili hakijapimwa? Haya ndio mambo mnapaswa kuwaambia wana CCM wanaojipitisha huku kudanganya wananchi kuwa mbunge wenu hafanyi kazi za jimbo. Waulizeni kwanini vijiji hivi havikupimwa miaka yote hii isipokuwa leo? Lazima muwaulize kwanini hawajafanya hivi Kasulu wala Kibondo?. Ina maana serikali ya CCM inawapenda wananchi waliochagua CHADEMA mkoani Kigoma kuliko majimbo walio chagua CCM? Msipowauliza na kuwaambia wananchi maswali haya mtakuwa hamkitendei haki chama chenu.

Ndugu wajumbe;
Niliwaambia mwaka mwaka 2005 wakati wa kampeni, nitatumia asilimia 30 ya mshahara wangu kuwasomesha watoto wa wanaotoka familia duni, zisizojiweza kabisa kiuchumi kama mchango wangu kwenu, kwani mimi nimezaliwa na kuishi katika familia duni, ninatambua mchango wa elimu katika kuinasua familia kutoka mduara wa ufukara uliokithiri. Nimekwenda shule kwa kutembea kwa mguu! Nilianza mara moja kutekeleza ahadi hiyo. Nimefanya hivyo, na mpaka sasa ninatoa zaidi ya asilimia 30 ya mshahara wangu. Na leo vijana 198 kutoka vijiji vyote vya jimbo langu wapo sekondari kwa mchango huo. Haya siyafanyi kwa bahati mbaya wala bahati nasibu! Ni mpango na nidhamira. Mkitaka kuona tofauti, waulizeni hata jirani zenu walio chini ya CCM, kwao wabunge wao wanasomesha watoto wangapi wa kimasikini? Kwao wamefanya nini?

Ni muhimu mkawauliza hao wanaojipitisha jimbo hili kwa hoja za eti mbunge wenu hamko nae kila siku. Nilipogombea ubunge nilitoa ahadi, na nilijua nitapimwa kwa ahadi nilizotoa. Waulizeni kipi bora kati ya mbunge kuwa na wananchi kila siku jimboni au mbunge kusomesha watoto? Waambieni watoe hoja kuhusu ahadi nilizotoa. Mbunge niliyechukua nafasi yake mwaka 2005 alikuwa mbunge kwa miaka 15 na alikuwa anakaa sana jimboni. Ninyi mnajua hiyo miaka 15 tumepata maendeleo gani.

Ndugu wajumbe;
Kabla sijaingia madarakani, Tarafa ya Mwandiga haikuwa na kituo cha afya. Leo kituo cha afya kimeanza kujengwa tarafa ya Mwandiga. Tayari tumeshapata mchango wa Shirika la NHIF katika mradi huu.
Niliahidi kuhakikisha tunajenga mabweni kwa wanafunzi wa kike, katika jimbo letu. Leo kwa ushawishi na mchango wangu wa moja kwa moja nimefanikisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Bugamba kwa kushirikiana na Shirika la TANAPA. Mimi binafsi nimetoa fedha za ujenzi huu. Nasikia kuna baadhi ya watu CCM wanasema wao ndio wamejenga bweni hili. Aibu tupu hii kwani wao wanajua ni juhudi za nani. Tayari nimefanya mazungumzo na TANAPA ili mwaka huu wa fedha tujenge bweni katika Sekondari ya Bitale. Haya ndio maswala ambayo Mbunge anapaswa kupimwa nayo na ninyi kama viongozi wa CHADEMA vijijini lazima muhakikishe wananchi wanajadili na kukipima CHADEMA kwa ahadi zake. Na sio majungu yasiyopimika.

Ndugu wajumbe;
Kuna mengi tumeyafanya kwa kipindi kifupi na katika mazingira magumu. Nilipoingia madarakani tu, nilihakikisha wakulima wa kahawa wanapata soko la uhakika la kahawa ili kuongeza tija ya kilimo kwa maisha ya mkulima. Nikawaunganisha wakulima wa kahawa wa jimbo letu na soko la uhakika Marekani, na sasa kuna mradi wa milioni 300 kwa ajili ya kuboresha na kutafuta soko la kahawa. Wanachama wa chama cha ushirika cha KANYOVU chini ya uongozi dhabiti wa Mzee Yahaya Mahwisa wanajua juhudi hizi na mafanikio yake. Ni kazi hizi zinazonifanya niamini kwamba ninyi viongozi wa CHADEMA mna kila sababu ya kwenda kifua mbele kwasababu mengi tunayoyafanya leo, hayakufanyika wakati jimbo hili likiwa chini ya CCM, na hayafanyiki majimbo mengi ya jirani zenu chini ya CCM. Ni lazima muoneshe tofauti ya Maendeleo ya jimbo hili wakati wa CCM na wakati wa CHADEMA ili wananchi wapime.

Ndugu wajumbe;
Niliwaambia wakati wakati wa kampeni, kwamba ninataka kwa kipindi chote cha uongozi wangu wa jimbo hili, sura ya jimbo ibadilike ili nitakapomaliza muda wangu yabaki mambo ambayo mtayakumbuka na kurejea kipindi cha uongozi wa jimbo hili chini ya CHADEMA. Leo Mwandiga Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza mpango wa kujenga kituo kikubwa kabisa cha mabasi. Upembuzi umeanza kufanyika na michoro kuuchorwa kwa ajili ya mradi huu mkubwa sana wa mabilioni fedha na ambao utabadili kabisa sura ya Mkoa wa Kigoma.

Leo tunaongea hapa, lakini ninawaambia ndani ya siku mbili , kata za Mwamgongo na Kagunga zitakuwa zimepata mawasiliano ya simu. Niliahidi kuhakikisha kuwa kunakuwa na mawasiliano ya simu katika Jimbo zima. Kampuni ya Zain imejenga minara Mwamgongo, Zashe na Kagunga. Jana nimezungumza kwa mara ya mwisho na ndugu zangu wa Zain na tumekubaliana kuwa siku nitakayokuwa kuwa Kagunga nitazungumza nao kwa kutumia simu yangu ya Zain.................... kutokea Kagunga! Haya ndio mnapaswa kunipa nayo, haya ndiyo mnapaswa kuipima kwayo CHADEMA.

Kata ya kagunga walikuwa na changamoto ya Soko. Niliahidi katika Kampeni kuwa nitahakikisha kuwa tunapata soko Kagunga. Nilifuatilia suala hili ndani ya Bunge. Nilifuatilia suala hili katika vikao vya Madiwani. Soko limeanza kujengwa Kagunga na Kagunga haitakuwa ile ile tena. Maana kuna mradi mkubwa zaidi.

Ndugu Wajumbe,
Leo ninapozungumza nanyi kuna mradi mkubwa sana wa kujenga Gati Kagunga na hivyo kuifanya kuwa Bandari. Kwa juhudi zangu binafsi kama Mbunge nimehakikisha kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wanaingiza Kagunga katika miradi ya magati Ziwa Tanganyika. Mradi wa Gati la Kagunga utagharimu zaidi ya shilingi 600 milioni. Gati hili litachochea maendeleo Kagunga kwa kiasi kikubwa sana na kuufanya mpaka wa Kagunga kuchangamka kama ilivyo Namanga na Tunduru. Hii ndio kazi ya Mbunge wenu. Hii ndio kazi mnayopaswa kujivunia.......!

Ndugu Wajumbe,
Mimi niseme wazi, na nikiri kwamba nina majukumu mengi ya Kitaifa na Kimataifa. Nimekuwa mjumbe wa Kamati ya Uanzishwaji wa Afrika mashariki, Kamati ya kuchunguza mikataba ya madini nchini, nimekuwa kwenye timu ya kumshauri Rais wa Ujerumani kuhusu masuala ya uchumi wa bara la Afrika, Na sasa mimi ni Mwenyekiti wa mwenza wa Mtandao wa wabunge wanaoshughulikia migogoro ya kisiasa duniani, Mwenyekiti mwenza wangu ni mbunge katika bunge la Ujerumani. Yote haya yanakijengea heshima kubwa chama chetu, mkoa wetu, na hasa jimbo letu. Leo ukiwa mkoa wowote Tanzania ukisema natoka Kigoma, unaulizwa kwa Zitto Kabwe?

Sasa kuna wana CCM wasio na hoja wanasema, eti mbunge wenu ni wa kitaifa, hawajali jimbo lake. Mimi nawaambia, ni kweli ninafanya majukumu mengi kama mbunge wa nchi hii. Wengine wanaweza kudhani nikiwa sipo Kigoma labda nipo Dar es Salaam. Lakini mimi nawaambia nimeumbwa kutumikia wananchi. Nikiwa sipo jimboni kwangu, nipo majimbo mengine tunaendesha harakati, tunatetea maslahi ya Taifa. Na ni kwasababu ya harakati hizo, Mbunge wenu nimejijengea heshima kubwa na uwezo wa kuibana serikali itekeleze baadhi ya mambo mnayoyaona jimboni hapa, ambayo hayafanyiki kwenye majimbo jirani yenu.

Mimi ninawaapia, siwezi kuacha kupambana na viongozi wabovu ndani ya serikali ya CCM kama ilivyo Buzwagi, kwa propaganda za CCM eti kwasababu Buzwagi haipo Kigoma kaskazini. Hilo siwezi, na nipo tayari kuhukumiwa kwa hilo. Ninasema haya kwasababu ninaamini hata barabara hii ya lami ya Mwandiga - Manyovu , ambayo ni ya kwanza kujengwa Kigoma tangu uhuru , haijengwi kwa pesa za Halmashauri ya wilaya ya Kigoma. Ni serikali kuu, ambayo kama tutaiacha iendelee kupoteza mapato kwa ufisadi, miradi mingi mikubwa kama hii itakwama. Huwezi kuacha kumkamata fisadi eti kwasababu hajaiba Kigoma Kaskazini. Fedha za kodi zinazolipwa Buzwagi ndio zitakazojenga Barabara yetu Kigoma, fedha za malipo ya wafanyakazi katika migodi ya madini ndio zinazofanya NSSF wajenge miradi Kigoma ukiwemo mradi wa Kituo cha Mabasi cha Kimataifa Mwandiga. Mamlaka ya Bandari Tanzania inajenga Gati la Kagunga kwa fedha za tozo kwa waagizaji Bidhaa kutoka nje na kupitia Bandari ya Dar es Salaam yakiwemo makampuni ya Madini ambao Mbunge wenu amejipambanua kupambana nao ili nchi ifaidike na rasilimali ya madini.

Ndugu Wajumbe,
Hao wanaosema kuwa mimi ni Mbunge wa Taifa na hivyo nimeliacha jimbo ni wapuuzi wachache ambao hawajui nchi inaendeshwa namna gani. Kuwa Mbunge wa Taifa ni sifa kwenu ninyi maana Bunge lina wajumbe 320 na ni wachache sana ambao tunaonekana kuwa wa Taifa. Miradi yote hii ya maendeleo inayoendelea hivi sasa inakuja kwa sababu mimi ni Mbunge wa Taifa. Nimepata heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma kwa sababu yenu. Msingenichagua kuwa Mbunge nisingepata heshima hizi ninazopata leo. Ninawashukuru sana. Asanteni. Hivyo, nipimeni na wabunge wengine ambao sio wa Taifa katika maendeleo!

Ndugu wajumbe,
Ninawatakia kila la kheri katika Mkutano Mkuu huu wa uchaguzi. Ninawaomba mchague viongozi ambao watapelekea chama chetu kushinda Vijiji vingi katika uchaguzi unaotukabili. Ninawaomba mchague viongozi ambao watatupelekea kushinda madiwani wengi zaidi. Mchague viongozi ambao watatupelekea kushinda Ubunge mwaka 2010. Ninajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kuwa ninatimiza majukumu kwa vizuri ili yeyote atakayeteuliwa na CHADEMA kuwa Mgombea aweze kuwa na rekodi ya kujivunia na apate ridhaa ya kuwa Mbunge wetu.
Asanteni kwa kunisikiliza.

Kabwe Z. Zitto, Mb
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Kalinzi, 15/8/2008.

Hongera Zitto na Wana Kigoma Kaskazimi chini ya CHADEMA
 
Mheshimiwa Zitto,
Hii hotuba ni ya lini? maanake naona tarehe hapo chini kidogo imenishtua... au ndio makosa ya uchapishaji.
 
Ahsante kwa yote mpambani wetu, hakika Jamii tunajivunia kuwa na kichwa kama wewe pale mjengoni. Mungu akuzidishie uhai ili tuendeleze mapambano ya kumkomboa mtanzania
 
Mheshimiwa Zitto,
Hii hotuba ni ya lini? maanake naona tarehe hapo chini kidogo imenishtua... au ndio makosa ya uchapishaji.

nafikiri ni tarehe ya kuandaliwa na sio ya kuwasilishwa...!!! Hotuba ndefu namna hio inahitaji muda kuiandaa...otherwise utakuwa mbabaishaji tu mbele za wananchi...!!!
 
Zitto unajitahidi sana. Nimeangalia CV kumbe ulisoma Galanos, hata mimi nilisoma Galanos Form 5 (1994-1995) kabla ya kuhamia Tambaza 1995. Mimi zitto naona kitu kimoja ambacho ningekuomba ufanye zaidi ni kuangalia mbali na haya ni mambo ambayo naomba ufanye

1) Pigania elimu ya watoto, cable imeshakuja ya internet lakini bila elimu kazi haziwezi kuja Tanzania mfano. Rafiki yangu alinieleza alipata tender ya kuweka software PPF sijui inaitwaje siku hizi lakini alikuwa hana wataalamu wa kutosha.
2)Usisahau Vijana wa nje sio kwenye mijadala tu. Tunaomba ututangaze tunavyosaidia nchi kwa kutuma pesa. Vilevile tupigie debe la uwekezaji na hata kazi kwa vijana waliosoma na wanataka kurudi. Sio lazima kila kitu kiwe siasa.Mfano vijana tunasumbuliwa bandarini hata kama tumeleta vifaa na mashine za maendeleo tungetakiwa tupongezwe hata kidogo basi.
3) Maendeleo mengi ya Watanzania ni bila msaada wa serikali. Watu wemejenga lakini hakuna barabara, mikoani hata kigoma kwa mfano hakuna barabara za uhakika. Watanzania wakiwekewa barabara wataendelea wenyewe. Mfano vijana kuja nje serikali haijasaidia chochote no mwamko wa Watanzania wenyewe hivyo barabara ikiwekwa watanzania wataweka mwamko wa maendeleo.
4)Productivity Tanzania inatatizo moja la kufanya kazi bila statistics. Kama tanzania ikiweka statistics za maendeleo kama shule, kilimo, afya itakuwa rahisi kwa serikali kufanya maamuzi. Mfano kama kilimo cha umwagiliaji kinafanikiwa Arusha ni kwanini kisifanikiwe sehemu nyingine kama kuna data ya vitu wanavyofanya Arusha ni kwa nini zilipelekwe mikoa mingine. Kwanini msichukue data za shule zinazofanya vizuri mfano watoto wa shule record zao, walimu, mazingira ya kusoma n.k na kuzipeleka sehemu ambazo shule zinafanya vibaya na kuzibadilisha. Nilishafanya project ya shule za Texas ili kujua ni kwanini shule zinafeli kwa kutumia Benchmark methodology data kama hizo tulipewa grant ya $3million. google APQC (America Productivity and Quality Cnt).
Sitachukuwa muda wako mwingi lakini usisahau vijana wa nje na jibu email.
 
nafikiri ni tarehe ya kuandaliwa na sio ya kuwasilishwa...!!! Hotuba ndefu namna hio inahitaji muda kuiandaa...otherwise utakuwa mbabaishaji tu mbele za wananchi...!!!
Sidhani kwa sababu kuna mengi yaliyotokea baada ya tarehe hiyo yamo ktk hotuba hii..Bila shaka ilitakiwa isomeke mwaka 2009 badala ya 2008, Mh. Zitto sii mchovu kiasi cha kutayarisha Hotuba mwaka mzima.
 
Mkuu,
Hilo swala lipo sana Mbeya. Kwa Mwandosya barabara na umeme huwa zinaishia kwenye mpaka wa JIMBO lake la uchaguzi. Haizidi hata cm 1.

Labda hii inabidi iwe fundisho kwa WANANCHI WAPIGA KURA kuwa mambo ya kuchagua wabunge wa kupitisha bajeti yamepitwa na wakati. Mtu kama Komba kakata viuno wee basi MNAMPA ubunge. Sasa huko aje atetee nini? Kutetea kukata viuno? Kwake yeye kuwa na Nyumba pale alipo sasa ni the dream becomes true. Sasa ukianza kumwambia maji taka yasiwepo, barabara nzuri, maji masafi, umeme, ........ kwake ya nini??

Kama Kigoma walimchagua Zitto na kutoka kwake Upinzani ame-lobb hadi barabara itajengwa, hayo ndiyo mambo sasa. Sisi hapa Sikonge tulimchagua kunguru Saidi Nkumba wa CCM, tumepata nini? Hawa ndiyo wanaitwa wasindikizaji na wagawa KURA tu. Yeye kila siku ni KUULIZA ili asikike radioni au kuuza sura kwenye TV. Jibu lolote akipewa hata la kitoto basi huwa anaridhika. Kwanza ninawasiwasi hata kama huwa anasubiri jibu zaidi ya kufurahi kuwa kafanikiwa kuuliza swali.

YES, tuchague wabunge Wazuri wa kutufanyia Lobbying BUNGENI na kutupigania haki zetu kimajimbo na kitaifa. Hebu fikiri wangelitokea akina Zitto kama 30 hivi wakaanza kugombania hilo milions za ujenzi wa lami. Hapo ndiyo ungeliona kile kinafanyika nchi kama za Korea. Zingelitandikwa humo ndani ya bunge na waziri wa Miundombini angelikuwa milele ana hali mbaya. Nisingelishangaa wengine wangekuwa wanakataa. Lakini ndiyo unakuta kwa TANZANIA hata wanalilia wapewe ..........

Bwana Sikonge naona unajichanganya,

Hapo juu kabisa umeonesha ubaya wa lobbying, kwa kuonesha miundombinu ikiwekwa kwa kufuata mipaka ya kisiasa. Na bahati nzuri au mbaya mwaka 2006 nilipita kule Mbeya, sikufanya utafiti wa kina lakini ktk mazungumzo ya kawaida na wenyeji wangu waligusia hili la umeme kuwekwa kisiasa na matokeo yake TANESCO kuingia hasara baada ya kutandaza mtandao lakini wateja hakuna!

Nadhani ktk larger picture huwezi ukakubalina na lobbying halafu then ulalamike jimboni kwako Sikonge hakuna maendeleo. Kumbuka hali hiyo imejitokeza kutokana na watu wenye influence ku-lobby na ku-pertubate funds zilizotakiwa zigawanywe kwa kutumia formula inayokubalika na kusababisha maeneo kama Sikonge et al kukosa funds.

Sijui kama umenipata.
 
Ahhhhh. Nimechoka kabisa.

Kwa maandiko yaliyoko huku ndani, hawa watu wanaoitwa mafisadi wameshasikilizwa na kukutwa na hatia na tayari wamehukumiwa. HII SI SAWA hasa ukizingatia kuwa hapa ni mahali pa watu wanaofikiri kwa kina.

Kuna mambo mengi na pengine karibu yote katika hotuba ya Mheshimiwa yanatakiwa kuthibitishwa hasa na wale wanaotoka kule kigoma. Hapa ndipo nilipotegemea hoja nyingi zaidi kutika kwa wana jf. kuliko kuwashukuru waliochangia kwenye safari ya yeye kufanikisha malengo yake.

Sidhani kama kuna ubaya wowote katika kushukuru kwake, tatizo liko mahali hapa, wana jf wengine wanataka mafisadi wote wasipewe tena nafasi ya kutajwa popote lakini naamini mafisadi hawa hawajsikilizwa? labda kwa sababu za kimfumo au kwa makosa ya watanzania wenyewe.

Ushauri
Kuna haja ya kuiambia sarikali ya CCM na Hasa JK, kama mafisadi watuhumiwa hawatafikishwa mahakamani na wao KURA HAWATAPATA. Dilunga ukija na hoja hii nitakuunga mkono.
 
Bwana Sikonge naona unajichanganya,

Nadhani ktk larger picture huwezi ukakubalina na lobbying halafu then ulalamike jimboni kwako Sikonge hakuna maendeleo. Kumbuka hali hiyo imejitokeza kutokana na watu wenye influence ku-lobby na ku-pertubate funds zilizotakiwa zigawanywe kwa kutumia formula inayokubalika na kusababisha maeneo kama Sikonge et al kukosa funds.

Sijui kama umenipata.

Mkuu Abdulhalim,

Naona hukunielewa nilitaka kusema nini. Ukweli siku zote wanasema uko katikati. Ndiyo maana nikakuonyesha sura zote mbili. Lobbying inaweza kufanyika kwa manufaa au ikaleta hasara. Wakati wa Nyerere sijui kuna mtu ali-lobby basi na sisi tukapata kiwanda cha nyuzi pale Tabora mjini. Kile kiwanda kilikuwa kikitegemea mali ghafi kutoka Shinyanga na Mwanza. Kilikuwa kwa kutegemea malighafi zitoke mbali namna hiyo. Hapohapo karibu na kiwanda kulikuwa na kambi ya JKT ndogo ikiitwa Miyemba ambayo ilikuwa chini ya Msange JKT. Palikuwa na mashine kubwa la kupasua mawe. Ila mlima ulikuwa mbaaali na hamna roli la kuleta mawe na matokeo yake eti kuruta kama 20 ndiyo wanaenda kutafuta mawe na kuyaleta pale. Alipokuja Makame akaamuru ule mtambo upelekwe Mwanza sehemu ilipo milima/mawe mengi na demand kubwa.
Kama mie nakuwa Rais, nina Lobby na kupata kiwanda cha kuzalisha umeme na wakati huo makaa ya mawe au Gas inatoka Kyela/Songa si itakuwa wendawazimu? Huku ndiyo ku-lobby kwa kuleta umeme na wakati huo watumiaji hamna.
Kwa Sikonge kama nikijenga mtambo wa kutengeneza funiture kama za Ikea na watu wanaenda kuziunga wenyewe majumbani, itakuwa jambo la muhimu sana hasa ukichukulia tuna mbao nyingi pale na tunaexport nje ya mkoa/nje ya nchi MAGOGO. Ningelijenga kiwanda cha kusindika Asali. Ningelijenga kiwanda cha kuzalisha mafuta nk . Hivi ndiyo vitu kwa sasa Sikonge wanaweza kusema wanahitaji kwa nguvu. Kiwanda cha Sigara kama kingelikuwepo hapo basi ile Tumbaku yote ya Sikonge/Tabora ingelikuwa inatengenezwa hapo Sigara na hapo tunauza product na si mali ghafi. Watu wangu wanapata kazi na si kwenda kuwapa wengine kazi.

Mwisho kama nilivysema. Lobby ipo, upende usipende. Ila inategemea una lobby nini. Nenda Iraq na Afghanistan uone wauza silaha na vifaa vya usalama duniani wakiwa kazini. Wanahaha kuwezesha bidhaa zao zinunuliwe. Hii ndiyo sheria ya uchumi. Kama wanunuzi ni wachache na bidhaa ni nyingi, wenye bidhaa AKILI KICHWANI. Hapo ndipo nasema, Zitto katufungua macho kuwa ukichagua MBUNGE "kiwete" basi kazi mnayo.
 
I couldnt say it more!

Jamani hivi kweli dunia ya leo kuna politics bila lobbying? ulizia Marekani..Senator akiwa Chairman wa Committee..ndo jimbo lake limeula. Wazee mpaka wanatoana machozi kwa kugombania uenyekiti wa kamati...Kifupi ni kwamba politics na lobbying ni vitu ninaendana. Sema tu kama alivyoeleza muungwana Sikonge. LAZIMA U-lobby kwa kufuata priority. Na ndo tatizo letu sisi Tanzania. Unakuta Mtu ana lobby kujenga international Airport Arusha..wakati in less than 40 KMs kuna nyingine Moshi. Anashindwa kuwa creative. Una lobby kulingana na strength uliyo nayo. Hapo ndo wananchi wako watafaidika.

Leo Sikonge akiwa mbunge..ni kwamba kilimo cha Tumbaku Sikonge ndo kitakuwa kimeinuka. Unaweza lobby kujengewa kiwanda cha Sigara.

Harafu hapa mnasahau kitu kimoja. Zitto kaeleza kabisa. Wabunge wa CCM wa Mkoa wa Kigoma waliandamana kwenda kwa waziri kuzuia hiyo barabara isijengwe..kwa sababu iko kwenye jimbo la upinzani!!! Sasa jamani hiyo ni akili au ni tope??? sasa mbunge kama huyo kweli anaweza kupata hata akili ya ku-lobby kwa waziri apewe barabara? Na waziri atamuona ni buricheka.

Wanaomlaumu Zitto, nadhani wanaongea politics za kufikirika. In otherwords...wanachokiongea katika uhalisia wa siasa hakipo. Though in theory ndo tunafundishwa darasani...After all ndo maana tuna wabunge. Otherwise tungekaa bila wabunge-after all serikali ina jukumu la kuendeleza Tanzania bila wala upendeleo.

Siku hizi hata serikali za kiafrica zina-commission lobbying firms (paying them millions) huko Washington, Berlin, London nk..kuwasaidia kupata misaada kuliko nchi nyingine..au na hili hamlijui jamani?
 
Mkuu Abdulhalim,

Naona hukunielewa nilitaka kusema nini. Ukweli siku zote wanasema uko katikati. Ndiyo maana nikakuonyesha sura zote mbili. Lobbying inaweza kufanyika kwa manufaa au ikaleta hasara. Wakati wa Nyerere sijui kuna mtu ali-lobby basi na sisi tukapata kiwanda cha nyuzi pale Tabora mjini. Kile kiwanda kilikuwa kikitegemea mali ghafi kutoka Shinyanga na Mwanza. Kilikuwa kwa kutegemea malighafi zitoke mbali namna hiyo. Hapohapo karibu na kiwanda kulikuwa na kambi ya JKT ndogo ikiitwa Miyemba ambayo ilikuwa chini ya Msange JKT. Palikuwa na mashine kubwa la kupasua mawe. Ila mlima ulikuwa mbaaali na hamna roli la kuleta mawe na matokeo yake eti kuruta kama 20 ndiyo wanaenda kutafuta mawe na kuyaleta pale. Alipokuja Makame akaamuru ule mtambo upelekwe Mwanza sehemu ilipo milima/mawe mengi na demand kubwa.
Kama mie nakuwa Rais, nina Lobby na kupata kiwanda cha kuzalisha umeme na wakati huo makaa ya mawe au Gas inatoka Kyela/Songa si itakuwa wendawazimu? Huku ndiyo ku-lobby kwa kuleta umeme na wakati huo watumiaji hamna.
Kwa Sikonge kama nikijenga mtambo wa kutengeneza funiture kama za Ikea na watu wanaenda kuziunga wenyewe majumbani, itakuwa jambo la muhimu sana hasa ukichukulia tuna mbao nyingi pale na tunaexport nje ya mkoa/nje ya nchi MAGOGO. Ningelijenga kiwanda cha kusindika Asali. Ningelijenga kiwanda cha kuzalisha mafuta nk . Hivi ndiyo vitu kwa sasa Sikonge wanaweza kusema wanahitaji kwa nguvu. Kiwanda cha Sigara kama kingelikuwepo hapo basi ile Tumbaku yote ya Sikonge/Tabora ingelikuwa inatengenezwa hapo Sigara na hapo tunauza product na si mali ghafi. Watu wangu wanapata kazi na si kwenda kuwapa wengine kazi.

Mwisho kama nilivysema. Lobby ipo, upende usipende. Ila inategemea una lobby nini. Nenda Iraq na Afghanistan uone wauza silaha na vifaa vya usalama duniani wakiwa kazini. Wanahaha kuwezesha bidhaa zao zinunuliwe. Hii ndiyo sheria ya uchumi. Kama wanunuzi ni wachache na bidhaa ni nyingi, wenye bidhaa AKILI KICHWANI. Hapo ndipo nasema, Zitto katufungua macho kuwa ukichagua MBUNGE "kiwete" basi kazi mnayo.

Waambie, nikisema mimi itakuwa "it's just that godless Bluray"
 
Ukizungumza tena na wapiga kura wako epuka kuwafagilia mafisadi kwa namna yoyote ile. Ungeishukuru serikali kwa ujumla na sio kutaja majina kama Chenge ambayo yanatia kichefuchefu!
 
Big up Zitto, tunataka viongozi wenye hoja kama wewe, nimeisoma hotoba yako kwa umakini wa hali ya juu, umeanisha ahadi ulizotoa na jinsi ambavyo zimetekelezeka, safi sana.2015 nadhani utafaa kuchukua uraisi wa hii nchi kama ukizidi kuwa makini kama ulivyo sasa maana tumechoka na propaganda za CCM
 
Sikonge said:
Mkuu Abdulhalim,

Naona hukunielewa nilitaka kusema nini. Ukweli siku zote wanasema uko katikati. Ndiyo maana nikakuonyesha sura zote mbili. Lobbying inaweza kufanyika kwa manufaa au ikaleta hasara. Wakati wa Nyerere sijui kuna mtu ali-lobby basi na sisi tukapata kiwanda cha nyuzi pale Tabora mjini. Kile kiwanda kilikuwa kikitegemea mali ghafi kutoka Shinyanga na Mwanza. Kilikuwa kwa kutegemea malighafi zitoke mbali namna hiyo. Hapohapo karibu na kiwanda kulikuwa na kambi ya JKT ndogo ikiitwa Miyemba ambayo ilikuwa chini ya Msange JKT. Palikuwa na mashine kubwa la kupasua mawe. Ila mlima ulikuwa mbaaali na hamna roli la kuleta mawe na matokeo yake eti kuruta kama 20 ndiyo wanaenda kutafuta mawe na kuyaleta pale. Alipokuja Makame akaamuru ule mtambo upelekwe Mwanza sehemu ilipo milima/mawe mengi na demand kubwa.
Kama mie nakuwa Rais, nina Lobby na kupata kiwanda cha kuzalisha umeme na wakati huo makaa ya mawe au Gas inatoka Kyela/Songa si itakuwa wendawazimu? Huku ndiyo ku-lobby kwa kuleta umeme na wakati huo watumiaji hamna.
Kwa Sikonge kama nikijenga mtambo wa kutengeneza funiture kama za Ikea na watu wanaenda kuziunga wenyewe majumbani, itakuwa jambo la muhimu sana hasa ukichukulia tuna mbao nyingi pale na tunaexport nje ya mkoa/nje ya nchi MAGOGO. Ningelijenga kiwanda cha kusindika Asali. Ningelijenga kiwanda cha kuzalisha mafuta nk . Hivi ndiyo vitu kwa sasa Sikonge wanaweza kusema wanahitaji kwa nguvu. Kiwanda cha Sigara kama kingelikuwepo hapo basi ile Tumbaku yote ya Sikonge/Tabora ingelikuwa inatengenezwa hapo Sigara na hapo tunauza product na si mali ghafi. Watu wangu wanapata kazi na si kwenda kuwapa wengine kazi.

Mwisho kama nilivysema. Lobby ipo, upende usipende. Ila inategemea una lobby nini. Nenda Iraq na Afghanistan uone wauza silaha na vifaa vya usalama duniani wakiwa kazini. Wanahaha kuwezesha bidhaa zao zinunuliwe. Hii ndiyo sheria ya uchumi. Kama wanunuzi ni wachache na bidhaa ni nyingi, wenye bidhaa AKILI KICHWANI. Hapo ndipo nasema, Zitto katufungua macho kuwa ukichagua MBUNGE "kiwete" basi kazi mnayo.

Sikonge, Masanja, Bluray, Kitila, Phillemon M,Abdulhalim,

..kuna somo ambalo watu hawakulizangatia ktk hotuba ya Zitto.

..somo lenyewe ni kwamba Mbunge anapaswa ku-fight kwenye kamati za kisekta za bunge kabla bajeti ya wizara haijasomwa bungeni.

..bajeti ikishafika bungeni ni kwamba mchezo umekwisha, na ni lazima upite. kama mbunge alikuwa na masuala yake na yamesahauliwa itabidi asubiri bajeti ya mwaka unaofuatia.

..somo hilo ndilo linalonikumbusha wabunge wanaopiga makelele kila bunge la bajeti. malalamiko yao ni hayo hayo kila bunge la bajeti. hivi kwa mwaka mzima wanakuwa wameshindwa kuzungumza na ku-lobby wizarani na kwenye kamati matatizo yao yakashughulikiwa?

..halafu wabunge wa aina hiyo ndiyo wenye rekodi ya kuchaguliwa kwa vipindi vingi.
 
Nilichoambulia katika hotuba ya Mh Zitto:

(a) Anahofia upinzani kwenye jimbo lake hasa kutoka ccm na hivyo akaenda kwenye diffensive mode

(b) Akiwa anajaribu utetezi wake hotuba yake ikawa 100% reduced to Zitto vs CMM na sio Chadema vs CCM

(c) Hajakomaa kisiasa, mkomavu kisiasa kamwe hawasifii mafisadi kwa lolote. Fedha walizoiba mafisadi ni zaidi ya mazuri waliyofanya

Hitimisho: Hotuba hii ni chini ya kiwango na inanufaisha CCM kuliko Chadema. Inaonyesha woga wa Zitto dhidi ya CCM, imeshindwa kuonyesha malengo na mikakati ya Chadema kujipanua katika majimbo mengine, na kibaya zaidi inawashukuru mafisadi ambao hata CCM yenyewe haijawashukuru. Wapinzani tuna safari ndeeeeeeeeeefu.
 
Back
Top Bottom