Hotuba za Mgombea urais kupitia CHADEMA ni nzuri sana, haziwezi katu kurushwa live!

Hotuba za Mgombea urais kupitia CHADEMA ni nzuri sana, haziwezi katu kurushwa live!

Acheni utani Tundu Lissu anatisha. Ni nani ashawahi kuchukua Mic na kusema hadharani tena zaidi ya mara moja kuwa "Magufuli asituone wajinga" isipokuwa Lissu? Nani ashawahi kusema hadharani kuwa Magufuli ni mbinafsi na kajenga uwanja wa ndege kijijini kwakwe na kufuga wanyama pori kwake isipokuwa Lissu? ( naamanisha hadharani na sio bungeni wala kwenye mitandao. Lissu akiongea tu mara moja TCRA, Abbas, Msigwa, Polepole, Kichaa Musiba, TBC, wakuu wote mikoa na wilaya pomoja na Kafulila (Tumbili) wanahaha kujibu lakini mwisho wa siku wooote wanajikuta wametofautiana. Yaani wanachanganyikiwa wanakurupuka tu.
Ujasiri amezidi mara mbili. Kwa kweli anatisha sana
 
Tulia dawa iwaingie vizuri.
Hotuba za kusema Tanzania kuna korona huku nae akiwa hana barakoa, hakai umbali wa mita moja.. Kama ipo si atulie kwake huko.. mbona vyama vyengine havisemi hivyo..? Huko ni kutafuta Kiki tu...

Halafu hotuba za kuisema serikali tu ni hotuba au michambo!
Hawezi mwaga sera zake bila kuitaja CCM au kumtaja Rais.. Sasa unapiga kampeni kwa kupaka tope wengine ili.. kwanini asisimame kwa hoja zake tu mpaka aponde ni Kama vile mtu mwenye kisasi!

Hizo hotuba zake zimejaa uchambaji tu na ndio maana vyombo vya habari vinamkimbia.. kwanini kina Membe hawakimbiwi..? Huyu mshikaji anatafuta tu huruma ya watu.. siasa Tanzania hazijaanza leo huo Uhuru wa kuchamba hawezi upata na kama Uhuru wa habari ndio upo hivyo basi kazi ipo!!..

Mbona mwenyekiti wake hupewa kipaza sauti hata kwenye sherehe za kitaifa na huwa hateti kama yeye!.. yule anakaa la moto mdomoni.

Nakubali Lissu anazo hoja za mashiko kabisa ila tatizo uwasilishaji wake tabu tupu.. atulie ajue anasema nini kwa lugha ipi na kivipi hoja anazo tatizo wenge Sasa
 
Jamaa anavutia kumsikiliza. Muwe mnatuma humu tumsikilize. Pia hakikisheni viongozi wenu na wanachama wenu na wapenda demokrasia wanashare hizi hotuba kwenye social media zao ambazo zina followers wengi.
🙏🏾
 
Ujasiri amezidi mara mbili. Kwa kweli anatisha sana
Ndomaana jana katikisha kibuyu cha bibi (wale tuliosoma zamani tunajua kilichompaka jamaa aliyeiba kibuyu cha bibi chenye karanga). Eti anataka mdahalo na Magu. Mimi nasema Magu aje na TCRA, TBC crews wote, Abbas, Polepole, Mwinyi junior, Musiba, G. Msigwa, mahindi ya kuchoma, jogoo na Chalamilla halafu Lissu asiruhusiwe kuingia na mtu yeyote hata na note book. Akimshinda kwenye huo mdahalo nahama nchi saa hiyohiyo
 
Ukitaka twende kwa mifano hiyo Basi pia ni halali kumtongoza mke wa mtu kwa kusema mabaya ya mume wake..!
Hapa hatuzungumzii dini maana kwenye dini huyo shetani ni adui.. Sasa kwenye siasa mbona hata wao waliyachanganya 2015 lowasa walimteta hapo kabla Kama ni fisadi lkn alipohamia kwao wakamsafisha na kumpa nyadhiza kubwa ya kugombea urais!.. Sasa ipi ilikuwa mantiki yao ya kuupigia kelele ufisadi Kama baadae wakaja kumkumbatia fisadi..??

Kikubwa sio tu kuisema serikali ya ccm bali unaisemaje..? Yeye amekomalia kila siku ccm na rais!.. Sasa wenyewe ccm wamseme nani..?
Hotuba zake zielekee zaidi kutatua shida tulizonazo kama taifa na sio kila siku kutuhubiria ccm.. kwani anafanya kampeni kwaajili ya ccm au ya taifa..?
Ccm kachukua nchi kafanya yake hata Kama ni kuikosoa si kwa michambo.. tz siasa hazijaanza leo na kuikosoa serikali hakujaanza leo achunge kauli zake namna ya ukosoaji ambao Mimi nauita ni uchambaji.
Kwanini utongoze mke wa mtu nikukosa maadili
 
Back
Top Bottom