Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
13,265
Reaction score
4,735
Hotuba ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere mara tu baada ya kuwa Waziri Mkuu kufuatia ushindi wa TANU ambao ulikipa ridhaa chama hicho kuunda Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Serikali ya Tanganyika mwaka 1961.

HOTUBA YA KWANZA YA MWALIMU NYERERE


Gazeti-Mtanzania; Ijumaa Oktoba 14, 2005.
 
Hotuba ya Mwalimu Nyerere Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma - 1995

[video=youtube_share;GAEpisZ3Cuk]http://youtu.be/GAEpisZ3Cuk[/video]
 
Hotuba ya Nyerere, Azimio la Arusha

 
Hotuba ya mwalimu Nyerere South Africa


 
Hotuba ya mwisho ya Baba Wa Taifa,Mwalimu Julius K. Nyerere aking'atuka Madarakani


 
Hotuba ya Mwalimu Nyerere March 14, 1995


 
Last edited by a moderator:
hotuba ya mwalimu julius k. Nyerere aliyitoa sikukuu ya wafanyakazi duniani,
mbeya mei 1, 1995.


 
Wakati ule mawaziri walikuwa 11! Hivi tuna wangapi siku hizi?


Bado tupo nyuma tu leo 2010 (49 years later) japo ''tumefanikiwa'' kuanzisha shule za Kata
 
RIP JKN,ni hotuba ya zamani lakini ni kama vile mpya,Umeishika nchi ikiwa haina chochote yaani masikini kwa kila kitu,hata ukatufikisha hapo ulipofikia,ulikuwa mjasiri sana pamoja na umasikini wetu lakini ulidiliki kutoa elimu ya bure,ulifanya kipindi hicho bila hata wawekezaji..duh
we gonna remember u ever in our life.
Wakati wengine wanajua umhinu wa umoja na wanatumia njia zozote zile ili kuungana .i.e EU,ASEAN etc lakkni sisi leo ndio tunalilia kila sku utanganyika na uzanzibar:nono:Busara zako hakika tutazikumbuka daima.
:rip:
Hotuba ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere mara tu baada ya kuwa
Waziri Mkuu kufuatia ushindi wa TANU ambao ulikipa ridhaa chama hicho
kuunda Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Serikali ya Tanganyika mwaka
1961.
 
 
"Utajiri wa Tanganyika, bado uko ardhini"

Usipoweka misingi mizuri kwenye ardhi umekwisha, je tungeamua kuchimba madini yetu wenyewe leo hii tungekuwa wapi? tungeshindwa kujenga mtambo wetu wenyewe wa MegaWatt 1000? Tungeshindwa kujenga barabara zetu? tungeshindwa kununua vifaa vya kufundishia katika shule zetu? tungeshindwa kuhakikasha hospitali zetu za umma hazikosi dawa?


Je tunaitumia Ardhi yetu tuliyopewa na mwenyezi mungu inavyotakiwa? tatizo lipo wapi?

Watu tunao, Ardhi tunayo,
Uongozi bora ????? Siasa safi ??? - HAPA NDIPO KWENYE MATATIZO YA TANGANYIKA YALIPO tusitafute mchawi. Miaka 50 ya uhuru hamna kitu cha kujivunia as a NATION kazi yetu ni kuagiza bidhaa toka kwa wenzetu hata kuendeleza kiwanda cha baskeli cha SWALA na kile cha magari TAMCO scania & Nyumbu Tumeshindwa.



 
Wadau nisaidieni, hivi viongozi wa sasa wana uthubutu wa kusikiliza hotuba za Nyerere maana zinachoma kweli mf ile inayohusu serikali legelege isiyokusanya kodi. Naomba kuwasilisha
 
Hawawezi kusikiliza kabisa kwanza hawana muda wa kusikiliza hotuba, wao wako busy na kujilimbikizia mali tu hotuba wametuachia sisi wanyonge tusikilize wenyewe!
 
Usijali kwani watake wasitake. HOTUBA HIZO ZITAWAHUKUMU SIKU MOJA. Mungu hatatuacha tuteseke daima. Ole wao wenye madaraka sasa wakati utakapofika
 
WanaJF!

Tukiwa na hekaheka za kujua nini kitajili kutokana na huu mgomo wa Madaktari kwa upande mmoja, na kauli ya serikali kwa upande wa pili. Nimeona tujikumbushe Hayati Mwl. J.K Nyerere nae alitoa msimamo gani au maelezo yepi katika hii migomo ya Wafanyakazi kudai maslahi. Karibu usikilize kisha tuchangie maoni.

Wakatabahu!
 

Attachments

Tofauti kubwa ya wakati ule na sasa ni kwamba viongozi wetu wa leo wamejiongezea mishahara na posho wakati enzi za Mwalimu alijipunguza mshahara kwa asilimia 20% wakati wanafunzi wa chuo kikuu walipogoma kupinga national service. Ningefurahi kumsikia Kikwete akisema anajipunguza mshahara wake kwa asilimia 20% na kuwataka wabunge wafanye hivyo na kuondoa posho. Inawezekana?
 
Bwana SaidAlly wakati ule wa Nyerere tulikuwa hatujachimba Madini yetu kwa kiasi cha kuwasaidia wananchi kama leo
na Mwl. Nyerere aliweza kuongea toka moyoni candidly watu au wafanya kazi wakamuelewa kwa sababu alionekana ni mtu wa kawaida sana kipato, tofauti na viongozi wetu wa leo matajiri wanao eleweka waziwazi.
 
Jasusi na DATOGA!

Na imani mmemsikiliza Mwalimu. Nakubaliana na mchango wenu mko sahihi kabisa.

Ukimsikilize huyu Mzee wetu, unaona kabisa anachosema ndio anachomaanisha.
Tofauti na viongozi wetu wa sasa imani kwao hatuna maana wanakimbilia kutupa data ambazo ki-uhalisia haziingii akilini.

Simply kama jana PM kajieleza kwa upande mmoja tu wa kilichopo lakini ameshindwa kufafanua kwanini anafikiri madaktari wameibuka na hayo madai. Siamini kwamba Madaktari ni wajinga kiasi hicho wasijue pato la nchi pamoja na taratibu za bajeti, wanaona viongozi wao wanayofanya hayaendani na hiyo hali haisi wanayoisema kuwa ni ngumu.

Sijui nani atakaeibuka mwenye nia safi na uchungu wa nchi hii atusaidie kwakweli inasikitisha sana.
 
Yoote tisa kubwa kuliko yote nchi yetu ni ya MADAI - Tunadai tunadai tunadai hasa wasomi ktk nchi maskini ambayo hao wanaodai ndio unaotuongezea umaskini maana makabati yao hayajai na hayatajaa hivi karibuni. Nadhani mimi pengine ni mjamaa ktk hali hii..
 

Hahaha....Mzee kweli alikhereheka sana na madai ya wasomo. Nadhani hajawahi kurudia neno moja mara nyingi namna hiyo maishani mwake katika hotuba moja...wanadai, wanadai, kila siku ni kudai na kudai.....hizo pesa ntazipata wapiiii mieeee....hahaha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…