Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Tofauti kubwa ya wakati ule na sasa ni kwamba viongozi wetu wa leo wamejiongezea mishahara na posho wakati enzi za Mwalimu alijipunguza mshahara kwa asilimia 20% wakati wanafunzi wa chuo kikuu walipogoma kupinga national service. Ningefurahi kumsikia Kikwete akisema anajipunguza mshahara wake kwa asilimia 20% na kuwataka wabunge wafanye hivyo na kuondoa posho. Inawezekana?

Sasa Kikwete ajipunguzie mshahara kwa asilimia 20....hiyo asilimia 20 ni ya mshahara kiasi gani? Kuna mtu anaujua mshahara wake?
 
Da mwalimu amekuwa mkali, amenikuna aliposema eti mie nidai kwa sabb ni president nilipwe laki! Du mwalim alikuwa analipw sh 10 wakati ule ee!
 
Sasa Kikwete ajipunguzie mshahara kwa asilimia 20....hiyo asilimia 20 ni ya mshahara kiasi gani? Kuna mtu anaujua mshahara wake?
Good question. Wakati Nyerere anajipunguza mshahara tulijua mshahara wake ulikuwa 6000/- kwa mwezi. Sasa tangu enzi za Mkapa nasikia eti mshahara wa rais wa Tanzania ni siri. Upumbavu mkubwa.
 
Tatizo lililopo ni kwamba kuna unfair distribution ya cake that is why madaktari wanadai, coz km TANAPA mfanyakazi wa kawaida tu analipwa mil 4 kwa nn madaktari wasidai? Kinachotakiwa ni kurekebisha muundo wa mishahara kila idara ili kila mtu apate kidogo na kingine kiende katika kuboresha huduma za jamii.
Haiingii akilini mbunge( Majimarefu)kwa siku analipwa 330,000 posho nje ya marupurupu mengine, then doctor anaefanya kazi ambayo ni proffessinal alipwe laki 600,000 kwa mwezi. Lazima wagome.
Kikwete aanze kupunguza mshahara wake na marupurupu yakwake ya wanae akina Riz, ya mahawara zake nk,na panga lipite kwa mawaziri,makatibu, wakuu wa mkioa, wakurugenzi, wabunge na nyongeza wapewe madookta na waalimu
 
duh, hotuba mzuri sana, kwa wakati ule mishahara yote ilikuwa uniform kwa mashirika na taasisi zote, huu ubaguzi tulioanza sasa wa kudhani kada flani ni zaidi ya nyingine ndio unaleta matatizo, Fedha kwa wabunge zipo, walimu hakuna, serikali kuu hakuna ( ila hapa analipya sitting allowance kwenye vikao).... hapo ndio tatizo
 
Wakuu za Jumatatu nafikiri si mbaya. Nilikuwa nasoma kitabu kimoja nikakuta nukuu za JK wa kwanza. nimezipenda sana kwa kweli. Mimi si mpenzi sana wa kuanzisha threads lakini kwa hii inanibidi tu niwape na nyie muone huyu mzee alivyokuwa anaona mbali sana. Nime-scan na nina-attach hapo chini. This Man was more than a wise Man. Hata kama wengine hatumkubali na hata tungemchukia vipi, mwalimu atakumbukwa siku zote. Kuna mambo ambayo aliyasema miaka ile na yanatokea sasa hivi hapa Duniani. RIP JK Nyerere.
 
Attachments

Mwalimu Julius Kambarage alisema " wazanaki wanasema hivi (akashika pua yake mara mbili na kuiachia kisha akaendelea) wazanaki wanasema hivi "UBUBISUBISU OBUWERE EKIRO KIRIMBURA"(watu wakacheka) maana yake "Mfichaficha maradhi kilio kitamfichua."
 
Umbumbumbu wa kyompyuta nao mzigo. Iko kwenye PDF na nimejitahidi kuiconvert kwenye text au word inanitoa kamasi mkuu. Ngoja nitajaribu au wajuzi wakija watafanya.
 
Mwalimu Julius Kambarage alisema " wazanaki wanasema hivi (akashika pua yake mara mbili na kuiachia kisha akaendelea) wazanaki wanasema hivi "UBUBISUBISU OBUWERE EKIRO KIRIMBURA"(watu wakacheka) maana yake "Mfichaficha maradhi kilio kitamfichua."
Ni kifo ama kilio?

Ama ni lugha ulimaanisha Kilio=kifo=msiba?

Nadhani ni "Kifo humuumbua"
 
Nashukuruni sana kuiziweka baadhi ya hotuba za huyu mzee hapa kwani zinanivutia visivyo kawaida na kama kuna mtu mwenye nazo au anaejua sehem naezazipata aniwekee hapa pls
 
Nyerere alikuwa kichwa haswa hawa wengine wamepwaya sana.
 
Nashukuruni sana kuiziweka baadhi ya hotuba za huyu mzee hapa kwani zinanivutia visivyo kawaida na kama kuna mtu mwenye nazo au anaejua sehem naezazipata aniwekee hapa pls
Kama jinsi mwenyewe alivyotuusia, tuchukue mazuri yake na yale mabaya yake tuyaache. ... usibebe kila kitu ...changanya na zako.
 
Hakika mzee alikuwa kichwa si hawa wanaokuja na maneno mengi na mwishowe wanaishia kuonekana vituko tu maana hakuna chochote wanachokiweza hata hotuba zao hazipendezi hata kusikliza km unataka kuwasikiliza bora usiklize mziki wa taarabu maana hawakawii kurusha vijembe mara mbayuwayu mara watoto wanaopata mimba ni vihelehel vyao yaani wizi mtupu.
 
Jamani hee hapa kwenye JF pawekwe sehenu maalum, watu wenye hizi speech za mwalimu waweke nadhani zitatusaidia sana
 
Wakuu za Jumatatu nafikiri si mbaya. Nilikuwa nasoma kitabu kimoja nikakuta nukuu za JK wa kwanza. nimezipenda sana kwa kweli. Mimi si mpenzi sana wa kuanzisha threads lakini kwa hii inanibidi tu niwape na nyie muone huyu mzee alivyokuwa anaona mbali sana. Nime-scan na nina-attach hapo chini. This Man was more than a wise Man. Hata kama wengine hatumkubali na hata tungemchukia vipi, mwalimu atakumbukwa siku zote. Kuna mambo ambayo aliyasema miaka ile na yanatokea sasa hivi hapa Duniani. RIP JK Nyerere.

I have read the article. There are some truth in it. However, some of his ideas are flawed. How could he blame the rich for misfortune of poor people or nations.

There's many factors why people are poor, and distribution of wealth between rich and poor is small part of the equation.

Furthermore, in the first paragraph he says that we have knowledge and resources to solve world poverty. My question to guys, his bad policies left the country heavyly indebted. So where was his knowledge and resources?
 
"Sioni sababu kwanini nisifike" eti kwa kuwa mama yake alifika miaka 100.
 
Back
Top Bottom