Anaendelea kwa kueleza: "Hapa Tanzania kwa sasa rushwa haina aibu, nchi inanuka rushwa. Tunataka kiongozi anayejua, kuamini na kufanya hivyo; na aweze kuwaambia kuwa Ikulu ni mahali patakatifu, sikuchaguliwa na watanzania kuja kupageuza pango la walanguzi!!! Uchaguzi siku hizi uchaguzi unakumbatia matumizi ya pesa.
Kutokusanya kodi ni sifa moja ya serikali zinazokula rushwa, serikali corrupt haikusanyi kodi, itabaki kufukuzana na watu wadogo. Huwezi kutumikia mabwana wawili, Mungu na Fedha. Siku hizi kulisemea azimio la Arusha inabidi uwe na moyo kama wa mwendawazimu. Azimio lile liweka miiko ya uongozi, lakini wenzetu wameenda huko Zanzibar wameliua, na hawajaweka mbadala, na matokeo yake mambo yanakwenda kiholela tu. Ameongeza kwa kusema hakuna serikali popote duniani inayoendeshwa bila miiko, na huwezi kupewa kazi ya nchi halafu unaendesha maisha ya kihuni".