Hili hata mimi huwa nalishangaa, kwanza ilitakiwa iwepo Library au center maalum ya Mwalim Nyerere na itangazwe, walitakiwa wawe na offical social network accounts , wana tupia vi picha hapo na ishu mbali mbali.
Cha kushangaza utaskia kuna taasisi ya mwalim Nyerere na kabisa wapo watu wenye Masters zao wana fanya kazi hapo, ndio ujinga wa wobongo.
Nyerere jina kubwa sana yet watu wanao simamia kumbu kumbu zake hawafanyi kazi ya maana kuiendeleza historia yake nzuri.
Wajifunze hata kwa mzee Mohammed said mbona wajomba zake walisaidia kupigania uhuru japo kidogo lakini jamaa ana wapa promo kubwa tu.
Yaan inasikitisha hatuna bunifu kwenye kumuenzi Rais Nyerere yaani hata Mugabe anatushinda kwenye kumkumbuka rais wetu wenyewe.