Kauli ya Mwalimu Nyerere Kuhusu Lowassa: NEC
Dodoma 1995
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu
safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake
basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema
aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf
(Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni
tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa
Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza
uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na
ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado
akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi
hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu
hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine
safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua
huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari
kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee
kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi
na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa
mgombea wetu." - Mwl. Julius Nyerere, NEC
Dodoma, Juni 1995
MYTAKE
JE TUNA MUASISI MWL NYERERE AU TUNAMPINGA? THINK CRICTICALLY.[/QUOTEmwl,Hivi kumbe kwa ccm kumuenzi mwalimu ni kumkataa lowasa?kuyauza mashirika ya umma,kuwauwa tembo,kuiba kupitia escrow,epa,meremeta,na kuingiza madawa ya kulevya havihusiani na kumuenzi mwalimu nyerere?wacha kujiaibisha na kutumia vibaya jina la mwl,leo hii ccm mnarithishana vyeo kwa watoto wenu na familia zenu mbona nyerere hakuwahi kufanya hayo mambo?