Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Ahsante kiongozi. Tataizo ni kwamba waTz wengi wenye uwezo ni waoga! Kama si kuogopa fitna, basi ni ushirikina!
 
Nili`sema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama ChaMapinduzi isingekuwa ni jambo la

kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri chaupinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu
badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanyanikapendekeza tuanzishe mfumo wa
vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kinginekizuri ambacho kingeweza kuiongoza
nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama ChaMapmduzi kusafisha uongozi wake
kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katikauchaguzi ujao.
Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalilizozote za kuondoa kansa ya uongozi
ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasiahalisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi,
Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozimbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo
nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasiwasi!
Wazalendo Watanzania hawana budi wapende kuona demokrasiahalisi ndani ya Chama Cha
Mapinduzi: Hii ina sura mbili.
Kwanza, ni lazima kurudisha tena uhuru na utaratibu wakujadili masuaIa yore makubwa na kufikia
uamuzi baada ya mjadala. Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kutoa
maamuzi muhimu. Kwa sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja;vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi
kuliko adha yakutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibumpinzani katika mjadala. Viongozi hawa
wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; na hawatakuwa nahaja ya kutumia akili. Kichini chini
baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho. Na kamatukiacha utamaduni wa woga
ukazagaa tutakuwa tunakaribisha udikteta.
Uhuru hauji wala haudumishwi ila kwa kuwa tayari kulipagharama zake; na vitu vyote vyenye
thamani kubwa gharama yake ni kubwa. Chama Cha Mapinduzilazima kiendelee kujenga utaratibu na
utamaduni wa kuchambua masuaIa makubwa katika mijadala,nakufikia uamuzi baada ya uchambuzi
na mijadaIa ya kidemokrasia na ya wazi wazi. Na wanachama waChama Cha Mapinduzi kwa vitendo
vyao lazima waanze kupiga vita utamaduni wa woga na fidhuliya viongozi.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi hakina budi kitazame upyautaratibu wake wa kuchagua viongozi wake
wakuu. Na muhimu zaidi na la haraka zaidi, Chama ChaMapinduzi hakina budi kitazame upya
utaratibu wake wakuteua mgombea wake wa kiti cha Urais waJamhuri ya Muungano. Nasema hili ni
jambo muhimu na la haraka zaidi kwa sababu uchaguzi wenyeweni mwakani tu. Hili lisipofanyika
upesi na kwa makini, yanaweza yakafanyika makosayatakayofuta kabisa uwezo wetu wa kufanya
hivyo baadaye.
Nina hakika kwamba utaratibu wetu wa sasa wa kuteua mgombeakiti chit urais sasa umekwisha
kupitwa na wakati. Mimi nilikuwa nikiteuliwa na HaImashauriKuu ya Taifa baada ya kupendekezwa
na Kamati Kuu bila mshindani. Na ndugu Ali Hassan Mwinyialiteuliwa katika mazingira ya siasa
ambayo hayakuwa tofauti sana. Hapakuwa na washindania urais.Ni Kamati Kuu yenyewe iliyoamua ni
nani wafikiriwe; na mmoja wao, nakumbuka, alikuwa hatakihata kidogo; tukalitoa jina lake.
Lakini sasa mambo ni tofauti. Washindania urais wapo, tenamoto moto. Chama kinajua hivyo, na
wananchi wanajua hivyo. Chama Cha Mapinduzi hakina budikitafute utaratibu mzuri wa
kuwashindanisha wataka urais hawa kwa njia ya wazi wazi.Tutafanya makosa makubwa tukikubali
kuteua mgombea urais kwa kutumia mzengwe. Njia ya mzengweilitufaa tu wakati tulipokuwa hatuna
washabiki wa urais. Na inaweza kufaa kama mnataka kumteuamwenzenu ambaye mnaamini kuwa
ndiye anayefaa, lakini hapendi misukosuko ya kushindaniauongozi.
Hivyo sivyo mambo yalivyo sasa. Sasa tunao washabiki, tenawashabiki wa kweli kweli! Kwa hiyo hali
ya sasa inataka ushindani wa wazi wazi, na ni vema Chama ChaMapinduzi kitafute utaratibu mzuri wa
kuwashindanisha hivyo. Ni muhimu zaidi kuwataka wanachama waCCM watoe maoni yao kuhusu
Rais wetu wa baadaye, kuliko kuwataka watoe maoni yao kuhusuSerikali ya Tanganyika, jambo
ambalo walikuwa wala hawalifikirii. Chama kisisite kutafutautaratibu wa kushirikisha wanachama
katika suala hili, kabla vikao vya juu havijafanya uamuzi wamwisho.
Ni vizuri katika suala kama hili mwongozo wa awali ukatokanana wanachama wenyewe baada ya
kupitiwa na wataka urais. Katika uchaguzi wa madiwani, chamakimeanza kutumia utaratibu wa
kutafuta kwanza maoni ya wanachama kabla ya kuomba vikao vyajuu kufanya uteuzi wa mwisho.
Utaratibu huu ni muhimu zaidi kwa kutupatia mgombea uraiskuliko mgombea udiwani.
Nchi yetu bado changa. Tusione haya kuendeleza taratibuambazo zinaonekana kuwa zinafaa, na wala
kubadili zile ambazo japokuwa huko nyuma zimetufaa, lakinisasa "zimepitwa na wakati." Ndivyo
tulivyofanya kuhusu mfumo wa chama kimoja; tusiogope kufanyahivyo kuhusu mageuzi ya kuleta
demokrasia zaidi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Inawezekana kwamba demokrasia peke yake ambayo kwa sasaitaendelea kuwa na maana kwa nchi hii
wakati tunasubiri kupata mpinzani mzuri na makini nje yaCCM, ni demokrasia ndani ya CCM.
Wanachama wa CCM wana wajibu wa kukitazama upya chama chaona kuona jinsi ya kuongeza
demokrasia ndani yake. Wajibu huu si kwa chama chao tu, niwajibu wa uzalendo kwa manufaa ya
Tanzania nzima.
 
Baadhi ya hotuba za Baba wa Taifa Marehemu Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambazo ni i muhimu kabisa hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwezi oktoba ni ile isemayo "MTU ANAYESAKA URAIS KWA VIPESA PESA NI WA KUOGOPA KAMA UKOMA. Bila kusahau ile inayosema "MTU YEYOTE ANAYEUTAKA URAIS WA NCHI HII AJIULIZE KWANZA ATAIFANYIA NINI TANZANIA NA SIYO TANZANIA ITAMFANYIA NINI"
Ebu chukua muda kuitazama hii video ya LOWASSA, hivi kweli hizi hotuba za Baba wa Taifa LOWASSA huwa anazisikiliza kweli? Lakini labda LOWASSA yeye kajifanya kiziwi, si anautaka urais bwana, je sisi tunaomshobokea tunazisikiliza hizi hotuba za mwasisi wa Taifa hili?

https://www.facebook.com/video.php?v=858386550867465
 
Hata JK alitumia pesa kuingia Ikulu, Mwacheni mzee wa watu mtamuua kwa pressure, wanasema mzee yake fimbo Nyerere apumzike kwa amani.
 
Namna ya pekee ya kumuenzi mwasisi wa Taifa letu ni kumchinjia baharini LOWASSA
 
Kwa nini wote waliofeli interview ya urais wakati wa Nyerere wanamzunguka huyo mzee wanarudi tena?,ona Malacela naye alikuja wakamtoa kiujanja sasa Lowassa wanamwogopa nini?Lowassa urais hapati.
 
Lowasa na ccm wasahau uongozi wa taifa letu. Kikwete wenu amewafungia mlango.
 
Baadhi ya hotuba za Baba wa Taifa Marehemu Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambazo ni i muhimu kabisa hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwezi oktoba ni ile isemayo "MTU ANAYESAKA URAIS KWA VIPESA PESA NI WA KUOGOPA KAMA UKOMA. Bila kusahau ile inayosema "MTU YEYOTE ANAYEUTAKA URAIS WA NCHI HII AJIULIZE KWANZA ATAIFANYIA NINI TANZANIA NA SIYO TANZANIA ITAMFANYIA NINI"
Ebu chukua muda kuitazama hii video ya LOWASSA, hivi kweli hizi hotuba za Baba wa Taifa LOWASSA huwa anazisikiliza kweli? Lakini labda LOWASSA yeye kajifanya kiziwi, si anautaka urais bwana, je sisi tunaomshobokea tunazisikiliza hizi hotuba za mwasisi wa Taifa hili?

https://www.facebook.com/video.php?v=858386550867465
Lowasa hawezi kusikiliza hotuba ya Mwl kwa sababu hakuwahi kumuheshimu.
 
Hotuba nzuri sana,aliyoyasema ndiyo yanayotekea sasa.
 
napenda kuona TEAM MEMBE ikiwa bize. Wanatumia teknolojia ya kisasa kuwafikia watu direct kupitia twitter, youtube whatsapp, facebook,instagram,

TEAM LOWASA bado mna kazi kubwa sana ku catch up na Team Membe

TEAM JANUARY MAKAMBA nilitegemea wangekuwa mstari wa mbele kwenye kutumia kampeni za teknolojia lakini naskia January watu wake hawako happy na menejimenti inayoongozwa toka South Africa
 
Back
Top Bottom