House girl wangu anatumia vidonge vya HIV

House girl wangu anatumia vidonge vya HIV

Niliomba ushauri siyo matusi. Kama huna la kunishauri kaa kimya.
Wewe ni mpumbavu...
Yaani mtoto uzae wewe afu alelewe na mwanamke mwingine, si bora usingezaa tu.
 
Ilitokea hii miaka ya nyuma, waliteketea watoto kwa kufanyiwa kusudi.
Ndio Ivo Kaa makini maana hii pia imetokea kwa jamaa yng baada ya kugumdua kaathirika na anakua akitumia miswaki ya watoto wake pia
 
Maslahi ya mtoto vs. Unyanyapaa.

Nadhani hapo ni wewe kupima, kwa kawaida mtoto hawezi kuambukizwa simply kwa kulelewa na mtu mwenye maambukizi. Ndio maana hata mama mwenye maambukizi anaweza kuzaa na kulea mtoto asiye na maambukizi. Lakini kuna elimu inayoambatana na namna ya mama kumkinga mtoto wake. Kama dada hana elimu yoyote basi anaweza kumwambukiza hata kwa bahati mbaya, ukizingatia mtoto mchanga ni rahisi kuambukizwa magonjwa.

Lakini kuna uwezekano pia wa dada kumwambukiza kwa makusudi mtoto, hii inategemea na nyie mnavyoishi naye hapo nyumbani. Tumeshaona akina dada wa kazi wakiwafanyia vitendo vya kikatili watoto, kwa hiyo sio ajabu akiamua kumwambukiza kwa makusudi kama njia ya kulipa kisasi kwenu.

Mwisho wa siku maamuzi ni yako. Nenda kampime mtoto. Kama yupo salama, basi tafakari, je dada wa kazi anaweza kumwambukiza kwa makusudi?? Je kuna mazingira ambayo mtoto anaweza kuambukizwa kwa bahati mbaya? Kama majibu ni hapana basi maisha yaendelee.

Kama mtoto tayari anamaambukizi jizuie usifanye maamuzi utakayojutia baadae.
Achukue huu ushauri wako. Aachane na mambo ya wana harakati
 
Imejitokeza kwangu mwaka huu. Mdada wa kazi 16yrs anajituma, bidii zote na anampenda mtoto.
Alizaliwa nao, kumrudisha tukaona huruma maana pacha wake yupo salama yeye ndio aliathirika.
Nilichofanya kuna mkwe wangu hana watoto, so tulimpeleka kule mpaka leo yupo nae na anasimamia kunywa dawa.
 
Amani iwe kwenu nyote. Nimegundua kuwa house girl wangu anae nilelea mtoto wangu mchanga anakunywa vidonge vya HIV kwa siri. Je hawezi kuwa amemwambukiza mwanangu? Kama jibu ni hapana, mwanangu atakuwa salama kweli au niachane naye msichana huyu? Naomba ushauri wenu.
Mwambie umetambua, unathamini na kuheshimu uamzi wa kuzingatia matumizi ya ARV. Mpokee katika hiyo hali, mwongoze katika kumlea mwanao kwa usalama. Atakuheshimu sana.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Muondoe hapo nyumbani kwako haraka lakini kidiplomasia, ukichelewa kuna siku shemeji ako, au mdogo wako au baba yako au ba mkwe wako atakuja kula tunda kimasikhara na kama sio wao kuna siku utamuuzi sana na atakuja kupunguzia hasira zake kwa mwanao, tena atamwambukiza kwa makusudi.
 
Muondoe hapo nyumbani kwako haraka lakini kidiplomasia, ukichelewa kuna siku shemeji ako, au mdogo wako au baba yako au ba mkwe wako atakuja kula tunda kimasikhara na kama sio wao kuna siku utamuuzi sana na atakuja kupunguzia hasira zake kwa mwanao, tena atamwambukiza kwa makusudi.
Naupokea ushauri wako naufanyia kazi
 
Atamaliza familia mpe mtaji akaanze maisha mengine mapya
 
Mimi naushauri mzuri mwambie kesho ajiandae anarudi kwao kwanini nimefanya nini mwambie mama ameamua kukaa na mwanae so haija haja ya wewe uendelee kuwa hapa ila hakikisha kaenda kwao na umsaidie kimfungulia kimtaji cha kujiendeleza na ukampime mtoto wako afya yake
 
Back
Top Bottom