Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wiki hii nzima Hizbullah wamekuwa wakirusha makombora mfululizo kuzipiga kambi za jeshi kaskazini ya Israel.Kinachoshangaza majibu ya makombora hayo yamekuwa hafifu sana kutoka kwa Israel ukiondoa yale ya kupiga gari na pikipiki zilizobeba baadhi ya makamanda wa Hizbullah.
Miongoni mwa silaha mpya walizoanza kuzitumia Hizbullah ni makombora ya kutungulia ndege ambapo ndege za Israel za kivita kwa kutambua silaha hizo zimelazimika kurudi zilikotoka.
Kwa upande wao Houth baada ya kuzindua kombora la Hypersonic wiki iliyopita ambalo halikukamatika mpaka likatua mji wa kusini wa Eliat. Leo tena wapiganaji hao wametumia droni ya baharini ambayo imeipiga meli inahofiwa huenda ikazama. Droni kama hizo ni silaha mpya ambazo zimeanza kutumiwa na Ukraine katika vita vyake na Urusi.
Hali hii kama ukilinganisha na mchezo wa masumbwi ni kama vile bondia asiyekuwa maarufu anavyoweza kumrushia bondia anayetetea taji lake ngumi katikati ya mchezo na washangiliaji kuanza kupata kiwewe wa bondia huyo akionekana kuyumba huku na kule.
Habari kama hizi huenda zikabezwa au zikawaudhi akina Imeloa,Maghayo,MK254 na wenzao lakini kwa mwenye macho mwengine atakuwa ameona tofauti iliyoanza kujitokeza katika vita vinavyoendelea mashariki ya kati.