How did you feel the last time you saw your Ex?

How did you feel the last time you saw your Ex?

osmaney

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2017
Posts
1,042
Reaction score
998
Hello guys 🖐

Kama kichwa kichwa kinavyojieleza, leo nisirefushe Sana maelezo, main body nimekuachia wewe, conclusion nitakuja kuimalzia Mimi.

Karibuni👇
 
Nilifeel good Sana,

Beatrice-Huyu nilachanaye Kwa vita, Vurugu,Matusi na Maneno Chungu nzima,

Huwa sipendi kuchana kwa Magonvi sana katika Mahusiano Japo ni ngumu,Nilimtafuta tukayamaliza vyema...Baada ya Muda nikisakia kaolewa,
Mara ya Mwisho Twaonana alikuwa na Mtoto moja,huku akiwa na kichanga Tumboni (Mimba)...Basi nilifurahi tukasalimiana freshh stori za hapa na pale na ucheshii.

Hakika nilifeel gudi.


Eliza-Huyu Nilikutanaye baada ya Miaka kadhaa yupo na Afya njema akiaambatana na mtoto wa kiume,Aliniona akaniita tukafurahi kusalimiana safii sana...!


Note:Huwa siendelezi Mawasiliano sana na Ma'Ex,Huwa nawaacha Waendelee na shughuli zao lakini kama Tukikutana basi tunafurahi na kubadilisha Tafakuri..!
 
Baada ya kuniona alinengua tabasam lake lilelile la mara zote!,sura yake tamu bado ilikuwa ikimea Kama uwaridi lenye unyevunyevu wa maji murua toka peponi..!
Ka mwanya kake kakichokozi kalinisabahi kwa mbwembwe kama mwali aliepoteza mume wake na kisha kumuona tena!!..

Ilibidi nigande kwa sekunde takribani tano nikiusabahi mwili wake uliokuwa wakibunifu,Tena uliohubiri ufundi stadi wa kazi ya alie juu!.
Sio siri ex yule alijaaliwa yani palipokuwa panahitajika kubonyea palibonyea Kama ilivyotakikana na palipotakiwa kutuna palituna kiufundi stadi uliotukuka!!..

Ni sauti yake tamu tu ndo ilinigutua kutoka ktk ubutwaa!.. na vile alivyoniita jina langu kwa sauti ya huba iliyojaa tashtwitwi za mahaba nilijiona ninahatia kwanini nilimuacha mtoto mzuri kama yeye.. Sasa hapo ndipo moyo ukaniambia "Pasha kiporo!!"
Na hapohapo ndo nikasikia sauti ya jogoo akiwika! Kumbe nilikuwa naota kamongo mimi.. hakuna siku ambayo nilijichapa kwenzi Kama siku hiyo kwa kuota kukutana na ex wa ndotoni..😜
 
Mimi niliachana na ex wangu kama miezi kadhaa imepita lakini ile hisia ninayoipata nikimkumbuka Mungu wangu nisaidie dah!!!!

Akaona solution ni kuhama mkoa ili uhusiano uishe lakini bado hali imezidi kuwa mbaya kwangu, nikaona nitafute kifaa kingine lakini bado hali imezidi kuwa mbaya zaidi


Mungu si athumani kanipigia anadai mbilinge mbilinge akizikumbuka zinamfanya ashindwe kufanya kazi huko aliko na mimi huku kazi zimesimama ghafla,

Haya mapenzi duniani humu mateso tu.....

I miss you Aboki [emoji2962]
 
Back
Top Bottom