How does WhatsApp Make Money?

Jack HD

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
851
Reaction score
1,168
Habari wana MMU,

Oooh sorry nilipitiwa kidogo, hamjambo Vichwa??

Hebu naomba tuelimishane leo kuhusiana na jinsi Whatsapp inavyoingiza pesa.

Tuanzie hapa!!

WhatsApp ilivumbuliwa rasmi na Bwana Brian Acton na mwenzie Jan Koum mnamo mwaka 2009 kama mbadala wa utumiaji wa huduma za message kwa gharama nafuu. Miaka mitano baadae Facebook Inc waliinunua Whatsapp kwa Dola Bilioni 19. Accounts za Whatsapp chini ya menejiment mpya tokea Bwana Mark Zuckerberg ainunue iliweza kukusanya mapato ya kiasi cha Dola 1.3 Milioni ndani ya kipindi cha miezi tisa tu. How is this possible? Is it enough?

Kwanini najiuliza hayo maswali hapo juu?


Ikumbukwe chanzo pekee ambacho whatsapp walikuwa wakikitegemea kabla ya kununuliwa na facebook ilikuwa ni subscription fees ambapo kwa baadhi ya nchi bila $ 1 ulikuwa huwezi kudownload whatsapp. Na kwa nchi nyingine ilikuwa mwaka wa kwanza ni bure lakini kila mwaka utakaongezeka baadae lazima ulipie $ 1. Kwa kipindi hiki Whatsapp ilikuwa na takribani watumiaji Million 700 duniani kote, hivyo kufanya mapato ya whatsapp kwa mwaka kuwa Dola millioni 700 kwa mwaka katika kipindi hicho.

January, 2016 Facebook walitangaza kusitisha kucharge subscription fees kwa watumiaji wa Whatsapp na Whatsapp ingeweza kupakuliwa na kutumika bure kabisa. Hii ilipelekea whatsapp kupoteza mapato yake ya Dola millioni 700 kwa mwaka kama iliyokuwa ikiyapata awali kwa njia ya subscription fees.

Jambo lingine la kushangaza ni kuwa hakuna Ads kwenye Whatsapp. Ikumbuke kuwa hii ni njia kubwa ya kujipatia fedha kutoka kwa makampuni na wafanyabiashara ambao hufanya online marketing. Mtandao kama WeChat ambao ni maarufu zaidi nchini China wananjia zao za kuingiza mapato. Mfano wao mbali na kuwa na ads wana online games pia. WeChat inakadiriwa kuwa na watumiaji wasiopungua milioni 846 na katika robo tatu ya mwaka wa fedha uliopita walikadiriwa kukusanya jumla ya Dola bilioni 6. Baado naendelea kujiuliza Whatsapp wao wanafanyaje?

Kupitia financial statements za Whatsapp ambazo ni confidential, Forbes wamekadiria kuwa mpaka kufikia mwaka 2020, mapato ya Whatsapp kutoka kwa kila mtumiaji yatakuwa ni $ 4.

Mpaka kufikia March, 2017 Whatsapp ilikuwa na watumiaji takribani Bilioni 1.2 Duniani kote. Hivyo basi, Kama namba ya watumiaji ikiendelea kukua kwa wastani ulele maana yake, kufikia mwaka 2020 Whatsapp itakuwa ikikusanya mapato ya zaidi ya Dola Bilioni 5 kwa Mwaka

Kutokana na Hali hii, kuna wataalam wa masuala ya fedha na uchumi walijitokeza hadharani kusema kuwa Facebook waliiover value WhatsApp na kulipa fedha nyingi zaidi kwa Whatsapp, huku wakidai Whatsapp inaendelea kuwepo kwa kusaidiwa na mapato yanayoingizwa na Facebook. Kichwani najiuliza maswali mengi sana. Mzungu si mjinga wa kutoa pesa yote hiyo kununua Whatsapp na kufuta subscription fees, kuna kitu watakuwa wamelenga for the longrun. Si hivyo tu, wangeweza kuweka Ads na kujipatia pesa nyingi zaidi, lakini hawajafanya hivyo. Wana maana gani? Kiukweli tunaweza kusema its completely free, lakini wao wanaingiza mapato kutokea kwetu, how is this possible? Are we the products?

Vichwa, hebu naombeni majibu yenu tafadhali!!
Jack HD
 
WhatsApp wanapata hela sana.
Kila unapotuma sms,kuangalia video,kutuma nyimbo nk kuna kiwango cha mb huwa unatumia.whatsapp wanachofanya ni kurekodi kiwango chako cha mb na kukibadilisha kwa kukipa thamani flani ya fedha,whatsapp hupata fedha hizo kutoka kwenye makampuni ambayo huusika na kuuza uduma za internet.
Hivyo basi kadri unavyotumia mb nyingi ndo wao wanavyopata fedha.
 
Hata mm binafsi kuna kipindi nilifikilia hvyo lakini nilipata ukinzani wa Mawazo yangu mwenyewe. Kwahyo pesa zenu za vocha huwa zinawafikia Whatsapp indirectly kupitia mb tunazotumia. Kwahyo Tigo wanawalipa social network zote Kwa mb nitakazotumia kusurf kwenye app ama website zao??
 
Mmhh kuna namna HAWA jamaa wanaingiza pesa maana kuna cost wanaingia ktk kuendesha wasap
 
Kabla ya kuuzwa kwa Facebook watsapp walikuwa wanapata pesa kupitia licence ambazo walikuwa wanatoza kwa mataifa yote dunia kasoro mataifa ya Africa! Yaani ulikuwa ilikutumia watsapp ilikuwa lazima ulipie Ada ya kila mwaka!

Baada ya kununuliwa na Facebook, Mmiliki wa facebook alitoa tozo ya Ada hiyo na kuifanya watsapp kutumiwa free ulimwenguni kote! Kwasasa Facebook wanatumia data za watsapp hususani number za simu katika kuboresha huduma za mitandao yao ya facebook na instagram.

Pia Facebook wanampango wa kutengeneza API ya watsapp ambayo wanaplan ya kuifanya itumike kibiashara zaidi na wataweza kupiga pesa nyingi sana kupitia API Hiyo. (imagine ukiweza kununua access ya kubroadcast kwa watanzania wote wenye watsapp message flani) Kwa maelezo zaidi kuhusiana na API tafadhari google!
 
Cc chief mkwawa
Jiulize ni kwanini millard ayo hukupa url ya habari fulani badala ya kukupa habari yote kny blog yake?hii ina maana akikupa habari yote yeye hatapata faida hivyo itakubidi utumie vi mb vyako vya kukopa uiangalie hiyo habari huku yeye mwisho wa siku anaenda kuchukua cheki yake voda,ttcl,air tel,smart,zantel au tigo...hivyohivyo kwa whats mark zurckerberg hupokea mshiko wa nguvu toka kwa hayo makampuni.
 


Hapana mkuu si sahihi! Haipo hivyo mkuu..
 
Watu wasichoelewa kuwa user informations are so important than we think. Unaweza kusema kuwa Whatsapp was over valued, but that is only financially, kiundani wao wanaweza kuona kuwa they under valued whatsapp according to it potential. In short FB wamenunua user infos na wanazitumia kwa kuboresha products zao. Vile vile for security issues ikiwemo tracing!
 
navyoelewa millard anakupa url ili uende kwenye wrbsite yake ili umuongeze watembeleajia na sio kama unavyodhani kwamba analipwa kwa makampuni ya simu
haipo hivyo
 
There are so called satellites and optical-fibre cables.
Lets say Voda buys 500Mbs from Satellites or OFCs ISPs/dealers and for them to get benefits they give you 500Mbs for just 500Tsh in a limited time...ni kama unavo chukua mikate kwa Bakhresa kwa 800Tsh na kutembeza kitaa kwa 1000Tsh ili upate faida.


Lets say the 500Mbs that you get from vodacom you use 1Mb to browse Whatsapp and Whatsapp will notify a large ISPs say Google that somebody used 1Mb to browse our site then Google will send these infos to your ISPs say. Vodacom that these infos says somebody used 1Mb to browse whatsapp and Vodacom will pay the money to whatsapp per 1Mb...everybody from Google to ISP get about 4%,5% until all ur money have divided including givernment taxes the cycles goes there and comes again whereever your browsing will be charged...But the method seems slowly to make money thats why others adds some services like Ads and whatever.
 
Umefanya hiyo research Mkuu?? Una reference ya hii kitu??
 
Haijawahi kuwa hivyo hata siku moja anayekupa mb ni kampuni ya simu siyo whatsapp iweje apate %
 
Millard ayo anapata ela kupitia matangazo (addons) whatsapp haina addons.
Pia kuna matangazo ambayo anayaweka moja kwa moja toka kampuni husika kitu ambacho whatsapp haina so point yako haiapply hapa.
 
Not true
 
Kuna biashara kubwa ya uuzaji wa taarifa ambayo hizi mitandao ambazo unafanya subscription ya kujaza taarifa zako. Taarifa hizi hutumiwa na makampuni makubwa ya marketing kwaa ajili ya kufanya promotion zao
So hata whatsapp pia nahisi ni miongoni mwa makampuninyanayouza taarifa so usishangae hupati adds kwenye simu yako directly kupitia whatsapp ila kuna algorithms ambazo zina learn user behaviour inakua rahisi ku predict ni user wa mambo gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…