Jack HD
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 851
- 1,168
Habari wana MMU,
Oooh sorry nilipitiwa kidogo, hamjambo Vichwa??
Hebu naomba tuelimishane leo kuhusiana na jinsi Whatsapp inavyoingiza pesa.
Tuanzie hapa!!
WhatsApp ilivumbuliwa rasmi na Bwana Brian Acton na mwenzie Jan Koum mnamo mwaka 2009 kama mbadala wa utumiaji wa huduma za message kwa gharama nafuu. Miaka mitano baadae Facebook Inc waliinunua Whatsapp kwa Dola Bilioni 19. Accounts za Whatsapp chini ya menejiment mpya tokea Bwana Mark Zuckerberg ainunue iliweza kukusanya mapato ya kiasi cha Dola 1.3 Milioni ndani ya kipindi cha miezi tisa tu. How is this possible? Is it enough?
Kwanini najiuliza hayo maswali hapo juu?
Ikumbukwe chanzo pekee ambacho whatsapp walikuwa wakikitegemea kabla ya kununuliwa na facebook ilikuwa ni subscription fees ambapo kwa baadhi ya nchi bila $ 1 ulikuwa huwezi kudownload whatsapp. Na kwa nchi nyingine ilikuwa mwaka wa kwanza ni bure lakini kila mwaka utakaongezeka baadae lazima ulipie $ 1. Kwa kipindi hiki Whatsapp ilikuwa na takribani watumiaji Million 700 duniani kote, hivyo kufanya mapato ya whatsapp kwa mwaka kuwa Dola millioni 700 kwa mwaka katika kipindi hicho.
January, 2016 Facebook walitangaza kusitisha kucharge subscription fees kwa watumiaji wa Whatsapp na Whatsapp ingeweza kupakuliwa na kutumika bure kabisa. Hii ilipelekea whatsapp kupoteza mapato yake ya Dola millioni 700 kwa mwaka kama iliyokuwa ikiyapata awali kwa njia ya subscription fees.
Jambo lingine la kushangaza ni kuwa hakuna Ads kwenye Whatsapp. Ikumbuke kuwa hii ni njia kubwa ya kujipatia fedha kutoka kwa makampuni na wafanyabiashara ambao hufanya online marketing. Mtandao kama WeChat ambao ni maarufu zaidi nchini China wananjia zao za kuingiza mapato. Mfano wao mbali na kuwa na ads wana online games pia. WeChat inakadiriwa kuwa na watumiaji wasiopungua milioni 846 na katika robo tatu ya mwaka wa fedha uliopita walikadiriwa kukusanya jumla ya Dola bilioni 6. Baado naendelea kujiuliza Whatsapp wao wanafanyaje?
Kupitia financial statements za Whatsapp ambazo ni confidential, Forbes wamekadiria kuwa mpaka kufikia mwaka 2020, mapato ya Whatsapp kutoka kwa kila mtumiaji yatakuwa ni $ 4.
Mpaka kufikia March, 2017 Whatsapp ilikuwa na watumiaji takribani Bilioni 1.2 Duniani kote. Hivyo basi, Kama namba ya watumiaji ikiendelea kukua kwa wastani ulele maana yake, kufikia mwaka 2020 Whatsapp itakuwa ikikusanya mapato ya zaidi ya Dola Bilioni 5 kwa Mwaka
Kutokana na Hali hii, kuna wataalam wa masuala ya fedha na uchumi walijitokeza hadharani kusema kuwa Facebook waliiover value WhatsApp na kulipa fedha nyingi zaidi kwa Whatsapp, huku wakidai Whatsapp inaendelea kuwepo kwa kusaidiwa na mapato yanayoingizwa na Facebook. Kichwani najiuliza maswali mengi sana. Mzungu si mjinga wa kutoa pesa yote hiyo kununua Whatsapp na kufuta subscription fees, kuna kitu watakuwa wamelenga for the longrun. Si hivyo tu, wangeweza kuweka Ads na kujipatia pesa nyingi zaidi, lakini hawajafanya hivyo. Wana maana gani? Kiukweli tunaweza kusema its completely free, lakini wao wanaingiza mapato kutokea kwetu, how is this possible? Are we the products?
Vichwa, hebu naombeni majibu yenu tafadhali!!