Tuna wasomi kama wao , tuna vitabu kama wao, tuna vyuo vikuu kama wao ,tuna serikali kama wao ,tuna watu kama wao wanaume Kwa wanawake . Tunazaana kama wao ,tunakula kama wao,tunakunya kama wao ila tuna Rasilimali nyingi kuliko wao . Chaajabu tuna umaskini mkubwa kuliko wao.
Mzee umeongea kwa uchungu sana ila kuna point moja muhimu sana ambayo umei-miss. Ni kweli kabisa wenzetu wameendelea kutokana na sababu hizi ulizozitaja hapa, wakati sisi bado.
Hata hivyo, kinachopelekea sisi tuwe katika hali hii sasa pamoja na kuwa na reosurves nyingi mno ni WAO UKIUNGANISHA NA UWINGI WA RESOURCES AMBAZO SISI BADO TUNAZO
Nasema ni wao kwa sababu gani? Ni kwa sababu wao walishafikia sehemu waka-exhauxt resources zote walizokuwa nazo na ambazo ndiyo zilipelekea wakaweza kufikia hatua ya maendeleo waliyonayo sasa. Hii ni hatua moja nzuri mno kwenye maisha na ninawapongeza sana kwa hilo.
Still, baada ya kufikia hapo, they came to a HALT, huku wakituona sisi bado tunapiga makasia nyavu zetu zikiwa zimejaa samaki, huku za kwao zikiwa ni tupu.
KWA HALI HII, HAPA HATA KAMA NI MIMI, LAZIMA TU NITAFUTE NAMNA YA KUSHIRIKIANA NA WEWE HATA KAMA SI KWA HIARI YAKO
Tatizo tulilonalo sasa ni la kidunia, kwamba resources zimebaki sehemu moja ya dunia huku watu wakiwa wapo kila mahali duniani. Ni lazima tu resources hizo zitumike kwa kila mtu bila kujali nani anamiliki resources hizo. Kwa hiyo issue kubwa kabisa inayotuletea shida sasa hivi sisi ikiwa ni pamoja na wale walioendelea, ni resoiurces kuwa sehemu moja ya dunia huku zikiwa zinamilikiwa na wale ambao hawana nguvu, huku wenye nguvu wakiwa hawana.
Hapa uwezekano wa asiyekuwa na nguvu KUTOKA KIMAISHA pamoja na kuwa ndiye anayemiliki resources, unakuwa ni mdogo sana